Yule Shangingi akanichuna kifedhuli..!

Thubutuu..........Ningemtafuta tena, ningelazimika kuiweka familia reheni.........Mbona nilibadilisha hadi namba ya simu. Mwanamke alikuwa nuksi kweli yule!

Labda alivyokuwa anakutafuta ukawa haupatikani, akajua shefa langu liko Marekani (kama ulivyolikoga) limepeleka ripoti ya vyura wa kihansi..! likirudi litanitafuta....! nikalichune tena.

 
Mtambuzi kama Pimbi vile...Hufanikiwi kwenye dili zako..pole sana ila tamaa co nzuri...mshahara wenyewe kiduchu unaisha cku moja tuu??lol
 
Kwanza ni mchana, halafu katikati ya mji, hoteli yenyewe nyota 5, wazo la kwake (inawezekana kufika ilibidi uulizie haswaa), ukajificha (hukutaka hata kujua atafikaje) na bado unakafikiri utagonga mzigo? Mbafu kabisa otherwise hii story imechagizwa na madhara ya mning'nio!
Mkuu!
Asikwambie mtu, kama uwezo wako ni mdogo katika kukicontrol kichwa cha chini, hautafikiria chochote katika ubongo wako zaidi ya maamuzi yaliofikiwa na kichwa cha chini....!

 
Kwanza ni mchana, halafu katikati ya mji, hoteli yenyewe nyota 5, wazo la kwake (inawezekana kufika ilibidi uulizie haswaa), ukajificha (hukutaka hata kujua atafikaje) na bado unakafikiri utagonga mzigo? Mbafu kabisa otherwise hii story imechagizwa na madhara ya mning'nio!
Aliyekwambia ilikuwa ni mchana ninani?
Umesoma vibaya wewe, hebu rudia tena....................
Kuhusu wazo la Hoteli ya Nyota tano, Hizi wewe unadhani mtu aliyejipa ujiko wa kuwa consultant wa Vyura wa Kihansi kwa ushirikiano na serikali ya Marekani Miadi yake anakutana na watu Tandale kwa Mtogole? Acha masihara bana.....................
 
Mtambuzi kama Pimbi vile...Hufanikiwi kwenye dili zako..pole sana ila tamaa co nzuri...mshahara wenyewe kiduchu unaisha cku moja tuu??lol
Hivi wewe unadhani mshahara wa fundi mchundo ni kiasi gani?
 
Pole sana hizo zinatukutaga wengi.........................ila nilishajifunza!!
 
Nafikiri huyo dada alikusaidia sana ili isimfanye uzinzi na kumdhalilisha mama Ngina wako, huwezi jua labda uliepushwa na majanga mabaya mabaya ya magonjwa na mitego mingine na ungempata siku ile labda tusingeweza kuwa nawe leo hii! Loh, nani angetupa simulizi kama hizi??
 
Kwa umri ulinao sasa, hiyo imebaki kuwa historia tu! Aisee kumbe ndo maana wengine huamua kukutana nao maeneo ya uswazi ili kuepuka gharama za mwanzo wakati mtu unamfanyia EIA mtu wako, eeeeeeh!
 
Kwi kwi kwi teh teh teh, wanakuonea wewe siku zote. Inabidi ukaonane na sangoma akuzinguwe!
 
Duu hii nimecheka sana aisee, sasa five star ulitegemea utalipa shilingi ngapi?

Mie nilijua tutapata bia moja moja tu kisha tuhamie viwanja vya Uswazi kuendeleza kimtindo.....................!
 
Hivi kweli unataka niamini kuwa alivyonitosa ni heri yangu wakati kanichuna kifedhuli na kuingia mitini bila hata kuonja utukufu wake! Kwa kweli amenionea sana, lakini Mungu atanilipia.....................
una visa wewe.siku nyengine utakavyoviona barabarani,wewe vimezee mate tu,kisha endelea na safari zako
 
..Assume unakutana nae tena ndani ya Dala dala siku nyingine usioijua, Utafanyaje??!!
Nitashuka kwenye hilo daladala na kusubiri daladala lingine...........Sitajisikia vizuri kupanda basi moja na ibilisi yule.........!
 
Back
Top Bottom