Yule Shangingi akanichuna kifedhuli..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yule Shangingi akanichuna kifedhuli..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Mar 26, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, na ndio nilikuwa nimetoka Benki kuchukua mshahara wangu wa kwanza baada ya kusota kwa takriban mwaka mmoja bila ajira. Kwa mwaka huo mmoja niliokuwa nje ya ajira baada ya kupigwa kile kinachoitwa Ridandansi, nilikuwa nimepigika kweli kweli kwa msoto. Nilikuwa nimekomba akaunti yangu yote kwani kwa mahesabu yangu ya haraka haraka, nilikuwa nina mahitaji mengi pale nyumbani ya kutekeleza achilia mbali madeni niliyokopa kwa marafiki zangu na kwenye dula la Mangi jirani na ninapoishi.

  Ama kweli ibilisi ni ibilisi tu, nikiwa ndani ya dala dala nilimkumbuka mwanamke mmoja niliyekutana naye juma lililopita wakati nikitokea Morogoro Kikazi, huyu mwanamke alikuwa ameumbika hasa, alikuwa maji ya kunde na amejaaliwa kweli kuwa na kalio kubwa kama mtungi na kiuno kama cha nyigu. Nilikuwa nimekaa naye siti moja na alionekana kuwa mcheshi sana kwangu. Tuliongea mambo mengi sana na alinijulisha kwamba anaye mchumba lakini kuna mgogoro huko kwa wakwe zake watarajiwa, kwani hawakutaka kijana wao amuoe kwa sababu ya tofauti za kidini. Yule kijana ni Mkristo mlokole na huyu dada ni Mwislamu. Na mimi sikulaza damu kama kawaida yangu nikajikuta namtupia nyavu zangu, na bila kusita yule mwanamke alinasa sawia.

  Alinitajia jina lake kuwa anaitwa Saniah na anaishi Mbezi ya Kimara na wazazi wake lakini anafanya kazi kwenye taasisi moja ya UN. Lakini hakunitajia taasisi hiyo. Tulikubaliana tukutane juma lijalo, na nilipanga iwe hivyo kwa sababu nilijuwa kuwa kipindi hicho nitakuwa nimepokea mshahara. Alinidadisi kama ninafanyia wapi na mie kwa kutaka ujiko nilimpiga fix kwamba mimi ni consultant wa kuchunguza vyura wa kule Kihansi kwa ushirikiano na Serikali ya Marekani na nilimdanganya kwamba wiki ijayo nitasafiri kwenda nchini humo kuwasilisha ripoti yangu. Kumbe mimi ni fundi mchundo ambaye niko choka mbaya.

  Ni wiki hiyo nilipopata mshahara Wangu ndipo nikamkumbuka mwanamke yule. Nilimpigia simu na baada ya kusalimiana nilimuomba tuonane kama tuliyoahidiana, alinijulisha kwamba mchumba wake anatarajia kurudi siku ile kutokea nchini Rwanda alikoenda kikazi hivyo asingeweza kuungana na mimi. Nilijitaidi kumshawishi amdanganye huyo mchumba wake kuwa ana dharura na asingeweza kuonana naye lakini akakataa akidai kwamba walikubaliana ampokee. Ilibidi nikubaliane naye. Lakini muda mfupi baadae alinipigia simu na kunijuza kwamba mchumba wake ameahirisha safari na atarudi siku inayofuata, alinitaka tukutane kwenye Hoteli moja maarufu ya nyota tano iliyoko katikati ya jiji hili la Dar. Nilipanda daladala na kugeuza kuelekea mjini kwani mwanaume tamaa ya ngono ilinitawala na nilikuwa nimepania kweli kumfaidi mwanamke yule aliyeumbika hasa.

  Niliwahi kufika kabla yake na haukupita muda mrefu na yeye akafika, lakini kabla ya kukaa aliniomba nimpe shilingi elfu ishirini akamlipe dereva taxi aliyemleta. Nilimpa zile hela akaenda kumlipa dereva taxi kisha akarudi na kuungana na mimi. Alinikuta nikiwa nakunywa Bia yangu, lakini na yeye akaagiza Gordons Gin na soda aina ya Tonic Water na barafu. Mie pale nilipokaa nilianza kupiga mahesabu ya gharama za vile vinywaji........maana bei za hotel za nyota tano ni pasua kichwa kweli.

  Haukupita muda yule mwanamke akaniambia, “Vipi honey hatuli, mwenzio nina njaa,” Mh, mie pale mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi, nikajua leo nimelivaa Gubeli, lakini kwa tamaa yangu ya ngono , nikajisemea moyoni, “ngoja tukale kisha niondoke naye akanilipe alivyokula.” Tuliingia kwenye mghahawa wa ile Hoteli na tulipoletewa Menu, jasho lilinitoka, bei ya vyakula ilikuwa iko juu kweli. Lakini nilijipa moyo kwani nilikuwa na mshahara wangu mfukoni.

  Tulitoa oda ya vyakula vyetu , na wakati tunasubiri vyakula vije mwenzangu akaagiza chupa ya mvinyo, ambayo bei yake ilikuwa si kidogo... Mweh! Mie nikajua leo nimepatikana. Ingawa alikuwa akiongea na mimi kwa bashasha, lakini akili yangu ilikuwa mbali kweli nilikuwa nawaza nitamwambia nini mama Ngina. Nitamwambia mshahara nimeupeleka wapi? Nadhani alihisi hali niliyokuwa nayo. “Honey you seems to be uncomfortable, what is wrong?” aliniuliza. Kwa kujifaragua nilimwambia ninawaza kama ripoti yangu itakubaliwa na serikali ya Marekani kwani ni mradi mkubwa sana ambao una thamani ya mamilioni ya dola. Lakini moyoni nilikuwa naumia kweli kwa gharama anazonipa.

  Haukupita muda chakula chetu kililetwa na baada ya kula kabla bili haijaletwa simu yake iliita na alionekana kushtuka, aliipokea na nilisikia sauti ya kiume upande wa pili, aliniomba radhi na kusogea pembani, nadhani ili nisisikie anaongea nini na huyo mwanaume. Nilitulia pale kwenye kiti, nikimsubiri arudi ili tuondoke nikajivinjari naye kabla ya kurudi kwa mama Ngina.

  Alirudi na kunibusu shavuni na kuchukua mkoba wake kisha akaniambia mchumba wake amekuja na amemwambia wakutane nyumbani, nilipomuuliza, mbona aliniambia kuwa ameahirisha safari na singekuja siku hiyo. Akanijibu kuwa mpenzi wake amezoea kum-surprise. Aliniomba radhi na kuniahidi kukutana na mimi siku inayofuata, akaniambia atanijulisha kwa simu tukutane wapi, hata hivyo aliniomba nimpe tena elfu ishirini ya taxi, ili amuwahi mchumba wake, nilizitoa zile hela huku roho ikiniuma. Aliondoka na kuniachia msala wa bili ya kulipa. Nilijikuta nikitoka pale Hotelini nikiwa nimebakiwa na shilingi elfu arobaini tu mfukoni. Nilitembea kuelekea kituoni huku nikiwa na mawazo kichwani. Nashukuru nilifika nyumbani salama, maana kwa jinsi nilivyokuwa na mawazo, nadhani ningegongwa na gari au boda boda.

  Nilifika nyumbani na kujitupa kitandani. Nilimwambia mama Ngina sijisikii vizuri na sitakula kwani nahitaji kupumzika.

  Niliamka asubuhi nikiwa bado na lindi la mawazo kichwani. Nitamwambia mama Ngina mshahara umekwenda wapi, yale madeni ninayodaiwa, nitawaambia nini wanaonidai? Niliwaza. Nilisimama dirishani nikichungulia nje, wanangu Ngina na Ngadu walikuwa wakicheza na wenzao kwa furaha huko nje lakini walikuwa wamevaa viguo vilivyowaacha makalio yao yote nje kwa kuchakaa..................

  Niliwahurumia wanangu, na nilijikuta nikibubujikwa na machozi kwa majuto.............Ama kweli majuto ni mjukuu...............
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Naomba msome tu, na msitoe maoni tafadhali.......................
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mzigo haukuugusa?
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Duu kali...mimi sikusoma kabisa maana ni ndefu. It doesnt make difference either. :)
   
 5. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mzee una mambo.
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Na wewe usinikumbushe machungu...........Nimeshasema sihitaji maoni yenu, we soma kisha chapa mwendo..............LOL
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kibelaaaaaa...wenzio nyavu zangu zomecheuwa, wikiendi yangu itakuwa....
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nimesoma nimechapa mwendo baba Ngina,,,,,
   
 9. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mtambuzi yaani huishi vituko, lakini katika stori yako kuna mafunzo makubwa sana.
   
 10. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Sitoi maoni ila nakupa pole kwa kuingizwa mjini.
   
 11. k

  kisukari JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  haiwezekani,uelezee halafu tusitoe mawazo.tamaa mbaya,na uwezi jua,yule dada kuondoka pengine ni heri yako.ridhika na uliekuwa nae,maana huyoi dada nae ni muhuni,ingawa alikwambia tangu mwanzo kuwa ana mtu
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Sijasoma ila najua naenda kusoma uongo wako mkuu!
  Halafu najua hautafanikiwa duu kama kawaida yako!
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli unataka niamini kuwa alivyonitosa ni heri yangu wakati kanichuna kifedhuli na kuingia mitini bila hata kuonja utukufu wake! Kwa kweli amenionea sana, lakini Mungu atanilipia.....................
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nilijua tuu wewe mtambuzi haufanikiwi tuu!
  Nitaacha kusoma mpaka utoe uliyofanikiwa bwana!
   
 15. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu!
  Hapo dada alikuchezea game!
  Hesabu alikutoa pesa ya texi, akanywa,akala na mwisho akakuchoropoa tena pesa ya usafiri.
  Pole sana mkuu!
   
 16. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na vipi ulimtafuta tena siku nyingine? au ndio tamaa ya ngono ikapotea ghafla!
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Thubutuu..........Ningemtafuta tena, ningelazimika kuiweka familia reheni.........Mbona nilibadilisha hadi namba ya simu. Mwanamke alikuwa nuksi kweli yule!
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  yaani kanikomba pesa zangu zote za mshahara na kuniachia wanangu wakitembea makalio nje kwa uchakavu wa nguo..............
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  hahahaaaaaaaaaa loh:A S-frusty2:
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha yaani nimejikuta naangua kicheko kwa sauti..duniani kuna mengi sawa sawa na bahari ..Mtambuzi mmh.
   
Loading...