Yule mlokole akaniletea kidamisi…………!

Kumbeee...............hapa sina mtoto, yaani unajua mbinu zote hizo................!
Hhahahhaha,pole baba siku hizi tupo kidigital zaidi,
Vijana wa kisasa anapokusaliamia anasubiri tu jibu ili ajue namna ya kukutia mkonon ukijibu kisela naye anaendeleza ivo ivo,ukisema bwa asifiwe utasikia amina dada habari ya uzima yaani huwa wanakua weshajipanga mbaya!!!
 
Hahahahahahaa nadhani hii itakua one of my favourate threads nilizowahi kusoma hapa jf, imenichekesha to the max! Asante
 
Unajua Da, AshaDii, uso umeumbwa na haya, we DCM zima linakukodolea macho na kukuzomea, hata kama ukijitia hamnazo, lakini ni lazima utajisikia fedheha......................
ha ha ha ha ha ha................, yani sina mbavu babaangu, nikitoka naenda kumwambia mama.
 
Unajua Da, AshaDii, uso umeumbwa na haya, we DCM zima linakukodolea macho na kukuzomea, hata kama ukijitia hamnazo, lakini ni lazima utajisikia fedheha......................
ha ha ha ha ha......... nikitoka naenda kumwambia mama.
 
ungejtambulisha mimi ni nabii na mtume .............................................
 
Hahahahaha!pole sn mdingi wangu a.k.a Gustavo!hakika ulipatikana,tatizo ulikua hujipangi baba,pale alivoanza kuleta habari za bwana na ww ungejidai ni shemas wa kanisa fulan na kuenda naye ki upako zaidi ungeambulia japo kukaribishwa kanisan mdogo mdogo ungepata no ya cm na mambo yangeendelea!hahaha shukuru hakukuwekea mikono kichwan na kuanza kunena kwa lugha!
kumbe hiyo ndo gia ya kuwaingia? bas nami nitaitumia
 
uanniuzi we kila sehemu hufanikiwi tuuu!? kwanini hujawai sema ulikofanikiwa bwana wewe hadithi zako mwishoni ni aibu tuu!
 
Nikasema nashukuru sana, ‘za kazi?’ Alijibu kwamba, kwa uwezo wa Bwana ni nzuri. Hilo neno ‘Bwana’ sikulizingatia. Najuta ni kwa nini sikulipigia mstari.

Ndo nimeanza kusoma, nipo hapo, nimecheka hadi basi.., Mkuu unatisha, Ngoja niendelee ntacoment baadaye..!
 
Sina mbavu jamani, looh! Wanaume ndo mjifunze kutoparamia kila mwanamke apitae mbele yako. Ntampa my wife iyo technique
 
Yule binti alicharuka zaidi wakati nashuka kwenye basi kwa kudai kwamba, nilikuwa nimeshindwa. 'Ameshindwa Ibilisi, ameshindwa kwa nguvu za Bwana, anaona aibu.'

Hahahahahahaaa., what a transformation, toka Gustave to Ibilisi, duh.. :scared:


Mstari mmoja tu ungemmaliza! "nimekupenda kwa jina la Yesu"!

Hapo still angeharibu, Walokole hutumia huu mstari, "Nimefunuliwa kuwa wewe ndo utakuwa mke wangu" hapo hata Binti wa mchungaji unabeba..!
 
yaani mkuu wakati naisoma hii thread yako nlitaka nkuulize hivi konda alifanya kimbwanga gani maana hawa watu kwa kurukia mambo hawajambo kabisa ila imejijibu yenyewe.pia nlitaka kukuuliza vp umbali wa safari c uliona karibia nusu cku ila kwa bahat ulifanya uamuz wa kushuka migo.dah pole sna nadhan ucku ulikua ukilala maneno ya yule dada na movie nzima ulikua ukiiwaza.
 
Mimi haya mambo ya ukware niliyaanza kitambo kidogo,na ndio maana siishi kusimulia masaibu niliyokutana nayo ujanani.

Nakumbuka siku hiyo nilikuwa natokea zangu Kariakoo narudi nyumbani Tegeta jioni ya saa 11 hivi. Kama mjuavyo kwa hapa jijini Dar usafiri mida ya jioni unakuwa na kasheshe zake, na kama huna ubavu unaweza kujikuta unakosa siti na ikakulazimu usimame, kitu ambacho nilikuwa sikipendi.

Baada ya kupimana msuli na abiria wenzangu nilibahatika kupata siti na kwa bahati nzuri nilibahatika kukaa na mtoto mmoja mbaye naweza kusema Mungu alimjaalia hasa kwa uzuri. Kwa sababu ndio zangu kuunganisha hesabu kwenye daladala nilishukuru sana. Niliomba foleni ianzie Faya ili safari ya Tegeta iwe ndefu, iwe ya saa 3 badala ya dakika 50 au saa nzima.

Ile kukaa tu, nikatupa salaam ya kiungwana, ‘habari yako sista.’ Yule dada alijibu kwamba hajambo. Nikasema nashukuru sana, ‘za kazi?’ Alijibu kwamba, kwa uwezo wa Bwana ni nzuri. Hilo neno ‘Bwana’ sikulizingatia. Najuta ni kwa nini sikulipigia mstari. Naomba niwaambie vijana wa Dar wajue kwamba, msichana akijibu salaam na kuingiza mambo ya ‘Bwana,’ ni lazima mtu ajiulize maswali.Basi tulipofika Jangwani nilishukuru kuona kuna foleni ya aina yake.

Nilisafisha koo na kuanza kufanya mazoezi ya namna ambavyo ningemwaga sera zangu za kumkaribisha ibilisi. Hatimaye nilipata njia. ‘Samahani, kama ninakufahamu, sijui tumewahi kuonana wapi, Tegeta, labda, au pale maeneo ya njia panda ya Wazo.’
Yule binti alitulia kidogo na kujibu kwa kifupi, ‘bahati mbaya, ninaishi Makongo.’ Niliona nimepungukiwa na vituo, hivyo kama ni kumwaga sera ingebidi nianze haraka. ‘Ahaa. Oke, naona tumekuwa tukikutana huku huku mjini, sijui unafanyia wapi mwenzangu?’ Niliuliza. Yule binti akajibu, ‘sifanyi kazi, nasoma chuo cha biashara.’ Niliona mitego yangu inapachuka kila nikitega.

Nilitulia kidogo na kutafuta pointi nyingine. ‘Sijui mwenzangu unaitwa nani, mimi naitwa…..’ Nilitaja jina langu na kabla sijaendelea, nilisikia: ‘Kwa jina la Yesu ushindwe, ni nguvu za giza zimekuzunguka. Huwezi kunitia majaribuni….’ Alikuwa akipaza sauti, halafu alikuwa akiongea kwa sauti kama ile itumiwayo na wahubiri wa kilokole wakemeapo mapepo. Kama kwamba hiyo haitoshi, alisimama na kutoa kitabu chake kitakatifu. Halafu aliendelea kunishutumu kwamba mimi ni ibilisi ambaye namjaribu mtu wa Mungu. ‘Huwezi kupambana na mwamba, huwezi kabisa, kwa nguvu zake baba ushindwe na uuone mwanga.’Kama mjuavyo watu wa Dar wasivyo na dogo, Basi zima lilivunja shingo.

Kuna waliokuwa wakishabikia kwamba, nimezoea kutongoza hovyo, kama vile walikuwa wananijua. Konda alikuwa akishabikia kweli, na alimtaka yule binti wa Kilokole anitoe katika Giza la upotevu, ili mradi kulikuwa na kila aina ya shutuma na kushangilia. Nililazimika kusimama na kusogea mbele kiaina, maana dhihaka na kejeli vilizidi.


Basi lilipofika Magomeni, nilisogea mlangoni na kushuka fasta. Yule binti alicharuka zaidi wakati nashuka kwenye basi kwa kudai kwamba, nilikuwa nimeshindwa. ‘Ameshindwa Ibilisi, ameshindwa kwa nguvu za Bwana, anaona aibu.’ Washabiki au wapambe walikuwa wakishangilia kwa nguvu ili kumchagiza yule binti wa kilokole aendelee kunikemea. Nilijilaumu kimoyomoyo kuhusu kosa lile.

Mpaka leo nikiwaona mabinti waliokaa kilokolelokole, nawapitia mbali.

Nimecheka mpaka basi, wewe ni mwehu, stori inachekesha mbaya kabisa kama nakuona vile.. Sijui kwa nini haukushindwa na kulegea kuileta hapa, by the way nashukuru sana kwa kuniongezea siku zangu za kuishi.
 
yap unge anza na bwana asifiwe ungewini mkuu,labda pia ungemuomba akuonyeshe pale anapoabudia na wewe pia utie timu pale siku moja kuabudu.ungemega kilaiini
 
Back
Top Bottom