Yule mlokole akaniletea kidamisi…………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yule mlokole akaniletea kidamisi…………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Mar 19, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mimi haya mambo ya ukware niliyaanza kitambo kidogo,na ndio maana siishi kusimulia masaibu niliyokutana nayo ujanani.

  Nakumbuka siku hiyo nilikuwa natokea zangu Kariakoo narudi nyumbani Tegeta jioni ya saa 11 hivi. Kama mjuavyo kwa hapa jijini Dar usafiri mida ya jioni unakuwa na kasheshe zake, na kama huna ubavu unaweza kujikuta unakosa siti na ikakulazimu usimame, kitu ambacho nilikuwa sikipendi.

  Baada ya kupimana msuli na abiria wenzangu nilibahatika kupata siti na kwa bahati nzuri nilibahatika kukaa na mtoto mmoja mbaye naweza kusema Mungu alimjaalia hasa kwa uzuri. Kwa sababu ndio zangu kuunganisha hesabu kwenye daladala nilishukuru sana. Niliomba foleni ianzie Faya ili safari ya Tegeta iwe ndefu, iwe ya saa 3 badala ya dakika 50 au saa nzima.

  Ile kukaa tu, nikatupa salaam ya kiungwana, ‘habari yako sista.' Yule dada alijibu kwamba hajambo. Nikasema nashukuru sana, ‘za kazi?' Alijibu kwamba, kwa uwezo wa Bwana ni nzuri. Hilo neno ‘Bwana' sikulizingatia. Najuta ni kwa nini sikulipigia mstari. Naomba niwaambie vijana wa Dar wajue kwamba, msichana akijibu salaam na kuingiza mambo ya ‘Bwana,' ni lazima mtu ajiulize maswali.Basi tulipofika Jangwani nilishukuru kuona kuna foleni ya aina yake.

  Nilisafisha koo na kuanza kufanya mazoezi ya namna ambavyo ningemwaga sera zangu za kumkaribisha ibilisi. Hatimaye nilipata njia. ‘Samahani, kama ninakufahamu, sijui tumewahi kuonana wapi, Tegeta, labda, au pale maeneo ya njia panda ya Wazo.'
  Yule binti alitulia kidogo na kujibu kwa kifupi, 'bahati mbaya, ninaishi Makongo.' Niliona nimepungukiwa na vituo, hivyo kama ni kumwaga sera ingebidi nianze haraka. ‘Ahaa. Oke, naona tumekuwa tukikutana huku huku mjini, sijui unafanyia wapi mwenzangu?' Niliuliza. Yule binti akajibu, 'sifanyi kazi, nasoma chuo cha biashara.' Niliona mitego yangu inapachuka kila nikitega.

  Nilitulia kidogo na kutafuta pointi nyingine. 'Sijui mwenzangu unaitwa nani, mimi naitwa…..' Nilitaja jina langu na kabla sijaendelea, nilisikia: 'Kwa jina la Yesu ushindwe, ni nguvu za giza zimekuzunguka. Huwezi kunitia majaribuni….' Alikuwa akipaza sauti, halafu alikuwa akiongea kwa sauti kama ile itumiwayo na wahubiri wa kilokole wakemeapo mapepo. Kama kwamba hiyo haitoshi, alisimama na kutoa kitabu chake kitakatifu. Halafu aliendelea kunishutumu kwamba mimi ni ibilisi ambaye namjaribu mtu wa Mungu. ‘Huwezi kupambana na mwamba, huwezi kabisa, kwa nguvu zake baba ushindwe na uuone mwanga.'Kama mjuavyo watu wa Dar wasivyo na dogo, Basi zima lilivunja shingo.

  Kuna waliokuwa wakishabikia kwamba, nimezoea kutongoza hovyo, kama vile walikuwa wananijua. Konda alikuwa akishabikia kweli, na alimtaka yule binti wa Kilokole anitoe katika Giza la upotevu, ili mradi kulikuwa na kila aina ya shutuma na kushangilia. Nililazimika kusimama na kusogea mbele kiaina, maana dhihaka na kejeli vilizidi.


  Basi lilipofika Magomeni, nilisogea mlangoni na kushuka fasta. Yule binti alicharuka zaidi wakati nashuka kwenye basi kwa kudai kwamba, nilikuwa nimeshindwa. 'Ameshindwa Ibilisi, ameshindwa kwa nguvu za Bwana, anaona aibu.' Washabiki au wapambe walikuwa wakishangilia kwa nguvu ili kumchagiza yule binti wa kilokole aendelee kunikemea. Nilijilaumu kimoyomoyo kuhusu kosa lile.

  Mpaka leo nikiwaona mabinti waliokaa kilokolelokole, nawapitia mbali.
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,060
  Likes Received: 24,064
  Trophy Points: 280
  Hehehehee!

  Mzee mwenzangu leo umenichekesha kwa sauti mbele ya mkoloni wangu!

  Dah!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Shikamoo babu..kweli ujana wao ilikuwa kasheshe tupu...

  Naona una mengi ya kutujuza
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hamkutamaniana tu, hakuna cha ulokole hapo.
   
 5. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa jina la yesu ushindwe.........!
   
 6. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hahahahaha!pole sn mdingi wangu a.k.a Gustavo!hakika ulipatikana,tatizo ulikua hujipangi baba,pale alivoanza kuleta habari za bwana na ww ungejidai ni shemas wa kanisa fulan na kuenda naye ki upako zaidi ungeambulia japo kukaribishwa kanisan mdogo mdogo ungepata no ya cm na mambo yangeendelea!hahaha shukuru hakukuwekea mikono kichwan na kuanza kunena kwa lugha!
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  hahahaha..... Mtambuzi Una mambo wewe!!! Hata hivo ulikata tamaa haraka saana.... Sijui maybe nakosea ila ninavoelewa kama binti wa kilokoke akianza kukemea na kukuombea na hali hujamaliza mistari ina maana "Kakufeel" na anaogopa ukiongeza tu nguvu hapo anaweza potelea kwa shetani.... :wink2:
   
 8. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  mweeh pole.
   
 9. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Pole sana mkuu,sasa waliokaa kilokole lokole tutawajuaje maana kuna wengine kutongoza ni kama sehemu ya maisha,yaani kusipite sketi au gauni hata bila kuangalia hata sura! te te te
  Ila nafikiri ulijifunza mengi sana siku hiyo,pole sana.Lakini na wewe ungebadilisha gea ya kuingilia,yaani na wewe ungepiga neno au ungemkemea shetani kwa sauti kama yake,angepoa na ugeanzia hapo.Kama ni kwenda kanisani kwake basi watu wanaenda umbali huo mkuu
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  you hv made my day loh!!!!

  sasa acha nichakarike kutafuta riziki
   
 11. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  'Kama mjuavyo watu wa Dar wasivyo na dogo, Basi zima lilivunja shingo.Kama naona muvi hii
  OTIS
   
 12. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu! hao wanamegana wenyewe kwa wenyewe! Siku nyingine ukikutana na inshu kama hiyo nena nayo kwa lugha, itaeleweka tu!
   
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Unajua Da, AshaDii, uso umeumbwa na haya, we DCM zima linakukodolea macho na kukuzomea, hata kama ukijitia hamnazo, lakini ni lazima utajisikia fedheha......................
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hiyo mbinu ungenifundisha wakati ule damu inachemka ingenisaidia sana..........bahati mbaya ushauri wako umekuja too late, nishajitwalia jiko mie...............
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  mabinti wa Kilokole wana salaam zao, ukimsikia binti anasalimia kwa kusema "SHALOOM" Basi huyo mpitie mbali, jua anatembea na "Bwana"
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kumbeee...............hapa sina mtoto, yaani unajua mbinu zote hizo................!
   
 17. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu unaijaribu uone kama inafanya kazi.. Shake well before use" ukione iko mwake mbuzi kashaelekea kibla unajifanya ulikuwa unamtania.
   
 18. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Alikuwa anakutega
   
 19. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Umenivunja mbavu npo icu! Hahahahahahahahahahaaaaaa.a.a.a.a.
   
 20. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya ndugu yangu pole sana kwa hayo yaliyokukuta............
  Kuna watu wanaosema hakuna mabinti wa kilokole wenye msimamo nafikiri wewe unaweza kua shaidi mzuri sana
  Asante
   
Loading...