Yuko wapi SELELI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yuko wapi SELELI?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kennedy, Mar 18, 2012.

 1. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,251
  Likes Received: 2,931
  Trophy Points: 280
  Aliyewahi kuwa Mbunge wa Nzega kwa tiketi ya CCM, Mh. L Seleli pia aliyehusika katika uchunguzi wa Kampuni tata ya kufua umeme wa Dharura RICHMOND. Baada ya kuangushwa katika uteuzi wa Ubunge uliogubikwa na fitna pia zengwe kubwa,amekuwa kimya na habari zake hazikiki tena. Hii inaashiria wazi siasa ni mchezo mchafu au ndiyo kusema SELELI hayupo nchini. Mwenye habari za huyu mtu tafadhali naomba anijuze pia anashughulika na masuala gani?
   
 2. i

  iMind JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Nilifurahi alivyopigwa chini, maana alikua anajiita mbunge wa maisha as if amewafanya watu wa nzega woote misukule wake.
   
 3. m

  moshingi JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu iMind swali alilouliza mleta mada hujalijibu bali umeweka chuki zako tuu dhidi ya Mh. Selelii...
  Swali lililoulizwa ni yupo wapi kwa sasa??? kama hujui ni vema ungebaki kimya kama wengine
  Lakini kwakuwa umetaja mabaya yake labda nikusaidie kumbukumbu ya mazuri yake;
  - Alishiriki kwenye tume ya bunge dhidi ya Richmond, wakati ripoti ilipowasilishwa bungeni EL alipewa
  nafasi ajitetee lakini akadai kuwa ripoti ilikuwa imejaa uzushi, hapo ndipo ujasiri wa SELELII ulipoonekana,
  alisimama na kumtaka EL athibitishe penye uzushi vinginevyo aombe radhi na kufuta kauli yake...ndipo spika
  alipoona mtumzima anaumbuka akaingilia kati na kumuokoa EL ambaye tayari alikwishawekwa kwenye kona..
  - Aliibua kashfa ya Serikali kufanya matumizi ya fedha ambazo bado bunge lilikuwa halijazipitisha, kitendo hiki
  kiliwaudhi sana vigogo wa chama chake na ndicho kilipelekea mizengwe kwenye uchaguzi ambapo alibwagwa,
  katibu mkuu wa ccm alipoulizwa kuhusu SELELII alijibu kuwa hana mvuto....hofu ni kwamba hasikiki kabisa, maana wenzake katika kamati wamepewa vyeo mbalimbali kama vile unaibu waziri, ukuu wa mkoa n.k, YUPO WAPI KWA SASA?
  Mwenye taarifa atujuze...
   
 4. S

  Shansila Senior Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ametoswa baharini,chezea ccm?
   
 5. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Alipoteza mvuto
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  mwulize Kigwangala
   
 7. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Siasa aka ****! i dnt buy, and am sorry 4 that.
   
 8. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  usicheze na Mafia ya CCM,imemchinjia baharini; huoni wakina Sendeka wote kwisha wanaimba wimbo wa Lowassa!!
   
Loading...