Mkuu samahani, nani amekuambia unaweza kuwa tajiri kwa kuwa mkulima Tanzania? Asilimia zaidi 80 ya wakulima nchi hii wanalima kilimo cha kutegemea mvua, sasa huo utajiri unadhani wataupata kwa kilimo hicho? Hao watu wa kwenye hiyo mikoa wenye unafuu wengi ni wafanya biashara na sio wakulima. Ama hujawahi kusikia ule msemo wa kejeli wa watu wa mjini kama maisha yamekushinda mjini rudi shamba ukalime. Yaani wanamaanisha kazi inayofanywa na watu walioshindwa na maisha ni kulima!! Ama unataka nikulitee picha ya wakulima hapa jukwaani uone hali zao.?
Kwahiyo unataka kusema huko Mwanza, Geita na kwingineko ni wafanyabiashara wazuri? Wanafanya biashara gani?
Wakati takribani Watanzania 80% wanaishi vijijini... hivi vijiji vya Mwanza au Geita nao wana uchumi unaotegemea biashara hata ionekane haiwezekani wakawa maskini kuliko Pwani, Lindi na Mtwara?
Ndo maana watu walikuwa wanaipinga ile taarifa! Ndugu zangu wa Mwanza walipoambiwa nao ni maskini wakaishia kuangalia "mabugando" ya Mwanza mjini na ku-conclude how come Mwanza iwe maskini na mabugando yote haya huku wakisahau zaidi ya 80% ya watu wa mkoa wa Mwanza wanaishi vijijini... kilimo kikibuma, nao wanabuma! Sasa ikiwa kilimo kimebuma, pamba imebuma... unatarajia hiyo zaidi ya 80% wanaishi vipi?
Ngoja tuelimishane kidogo! Kuna mambo mawili kwenye hizi ripoti za uchumi... mosi; pato la mkoa na pili hali ya umaskini!
Linapokuja suala la pato la mkoa, always Mwanza na hata Geita na Shinyanga zitakuwa juu tu na mikoa kama Lindi, Pwani na Mtwara itakuwa chini kwa pato la mkoa! WHY? Because Mwanza, Geita na mikoa mingine kama hiyo ina massive foreign na local investments hususani kwenye sekta za madini! Kutokana na hilo, mapato ya hiyo mikoa LAZIMA yatakuwa juu! Swali linalofuata: Je, asilimia kubwa ya hayo mapato yanaenda kwa nani?! Jibu ni kwamba asilimia kubwa inaenda kwa wawekezaji, asilimia nyingine inaenda TRA na sehemu ndogo inayobaki ndiyo inazunguka kwenye uchumi wa mikoa hiyo na kutafsiri kiwango cha maendeleo(sio pato tena) ya mikoa husika!
Sasa kv wananchi wengi wanaishi vijijini na wanaofaidika na hiyo migodi ni wachache sana! Na ikiwa vijijini kilimo kimebuma kama ilivyobuma pamba! Ukichanganya na high population ya kanda ya ziwa; then, hapa huhitaji kuwa economist ku-anticipate hali ya maendeleo kwenye mkoa ambao una very high population but no dependable cash crop! Mwanza wala Geita sio wafanyabiashara!
Kinyume chake, si Lindi, Mtwara wala Pwani zenye massive foreign and local investments. Kutokana na hilo pato la mkoa kwa hiyo mikoa ni dogo na hata TRA hakuna cha maana wanachopata hadi pale gas business itakavyochanganya!!
Lakini wakati hakuna foreign investments, kama ilivyo kwa mikoa mingine ya Tanzania, majority hapa nao wanategemea kilimo. Nimetaja korosho na ufuta mazao ambayo, ingawaje ni kweli korosho nayo inajikongoja lakini haijabuma kama ilivyobuma pamba! Mtu wa Pwani mboga bila kitunguu kwake ni taabu tupu... kwahiyo unakuta vitunguu navyo ni kilimo kinacholipa sana kwenye hii mikoa! Watu wa Pwani mboga bila nyanya ataila kwa shida... kwahiyo unakuta nyanya nayo ni moja ya vilimo venye pesa sana kwenye ukanda huu!Miaka 20 iliyopita bush kwetu walikuwa wanapenda sana kulima mpunga lakini siku hizi majority ya vijana huwezi kukuta eti analima mpunga zaidi ya nyanya na vitunguu!!
Sasa wakati sehemu kubwa ya mapato ya madini yanaishia kwa investors; asilimia kubwa ya mapato ya kilimo yanabaki kwa mkulima mwenyewe! Na ukizingatia hii mikoa haina population kubwa, usishangae kukuta by average wanawapiga gap Mwanza kimaendeleo (sio pato la mkoa)!
In few years to come, Lindi na Mtwara zitakuwa zinashindana na Dar kwa pato la mkoa (na usishangae Dar ikapigwa gap) lakini bado Lindi na Mtwara zitaendelea kuwa maskini compared to Dar for years.
Ukitaka kufahamu effect ya pesa inayoenda moja kwa moja kwa moja kwa mwananchi na ile inayoenda kwa mwekezaji angalia mkoa wa Kilimanjaro. Kilimanjaro ni moja ya mikoa yenye pato dogo sana ukilinganisha na umaarufu wa mkoa wa huu! Nadhani hata katika 10 bora ya kuchangia pato la Taifa hawapo! WHY? No big investments in Kilimanjaro!
Lakini kwa kuwa Kilimanjaro wanafanya sana biashara kubwa na ndogo. Na kwa kuwa sehemu kubwa ya mapato ya biashara hii inaenda kwa wafanyabiashara wenyewe ambao ni wana Kilimanjaro... ndo maana unakuta ingawaje mchango wake kwenye pato la taifa ni mdogo, lakini maendeleo ya watu ni makubwa kwa sababu sehemu kubwa ya pato la Kilimanjaro linatengenezwa na wananchi wenyewe na pesa kwenda moja kwa moja kwao wenyewe na sio investments za tajiri mmoja mwenye li-investment likuuuuuuubwa kama ilivyo kwenye investments za migodi!!