Yuko wapi Ridhiwani Kikwete?

Yuko wapi Ridhiwani Kikwete?

1472468563669.jpg
muangalie enzi za JPM
 
Dah siamini kama hata Kaka February nae kakaaa kimya hivyo aiseeeee, dah siasa hizi, hivi na yule dogo aliyetukana sana kipindi kile na kuweka clip kwenye social media kaishia wapi? Yule sijui alikua chipukizi wa Taifa...kibonge hivi
Anakwambia wao ndio serikali, hahaha! Ingekuwa ni mtoto wa kapuku angeitwa mchochezi na kuishia nyuma ya nondo tu.
 
Hivi lengo lako ni kuuliza alipo riziwani au kusema watu wa pawani ni maskini kwa sababu wanakaa vibarazani?.

Maana naona umechanganya habari mbili zisizowiana.

Riziwani ni mbunge wa chalinze na siyo pwani sasa unapotaka asimame aitetee pwani kana kwamba ni mbunge wa pwani napata mashaka na uzi na uelewa wako.
Hv Chalinze iko mkoa wa Moro?
 
Mkuu unakosea pwani ni nafuu kukiko mwanza unajua sio kwamba pwani wanakaa wazaramo na wakwere tu au kuwa mwanza wanakaa wasukuma tu ukweli kanda ya ziwa masikini kuliko pwani
 
Yuko huku instagram leo.
  • ridhiwani_kikweteLeo tarehe 29 August 2016 nimeshiriki uzinduzi wa bodi ya Maji ya Chalinze.Pichani nikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Mwenyekiti wa Bodi Mchumi Abdul Pagali, Eng.Christer Mchomba mkurugenzi Mtendaji wa CHALIWASA na wajumbe wengine wa Bodi hiyo.
 
View attachment 389718
Sikusikii tena kwenye media kama ilivyokuwa enzi za utawala wa baba yako nini kimekupata?

Nilisikia wanatangaza mikoa masikini Tanzania yote kutoka kanda ya ziwa sikukuona hata ukitokea kuwatetea Wanachi wa pwani ambao wanaishi kwenye umasikini wa kutupwa

Hivi kweli ulikubali kuwa Mwanza ni masikini kuliko Pwani?

Wanachi wa pwani wanaoshinda vibalazani wanapiga story ndio waje wawe matajiri kuliko Mwanza ??

Nini tatizo umepotea kwa media?
Hata bunge lililokuwa Giza sikuona jitiada zako kuwasemea wanyonge wa pwani?

Au tumbua majipu imekukumba?

Au ulitaka nafasi ya uwaziri ikakosa ukasusa??

Bado sijaelewa nini Tatizo?


KATULIA KAMA MAJI YA MTUNGI..KAMA JANUARY MAKAMBA...WOTE KIMYA WANAOGOPA
 
Vyote mkuu
Shida yako sio Ridhiwan bali una kale kaogonjwa ka kejeli kwa watu wa eneo fulani! Angalia lugha uliyotumia... wapenda kukaa vibarazani! Lakini ushahidi usio shaka ni kwamba hata huko wasikokaa vibarazani nao ni masikini wa kutupwa! Elimu hawana sawa tu na hao watu wa pwani! Na kwavile mmekaririshwa kwamba wale ni wanya kahawa na kukaa vibarazani; basi hata mnapoletewa tafiti kwamba huko kwenu ni masikini wa kutupwa huwa hamtaki kukubali kwavile mnaishi kwa kukariri!! Kuna mtu niliwahi kumuuliza kwamba Lindi, Mtwara, na Pwani kote huko wanalima korosho na ufuta bila kusahau nazi! Tofauti na pesa za madini ambazo asilimia kubwa huenda kwa wazungu, pesa za korosho, ufuta na nazi zinaenda moja kwa moja mifukoni kwa wakulima! Swali ambalo niliuliza na sikupata jibu ni je; huko ambako mnakataa kwamba sio masikini mnalima nini!? Hilo jibu hadi leo sijapata!!

Sasa wewe endelea na porojo za kusema hawa ni watu wa vibarazani na ndio maskini wa kutupa lakini "sisi ndio matajiri...!" Endelea na hizo fikra lakini wenzenu wanapiga mzigo kimya kimya huku wengine mkiendelea kuonea fahari historia!! Fanya kupekua pekua kumbukumbu za miaka 3 iliyopita halafu angalia ikiwa hiyo mikoa unayoamini kwamba wao wapo vizuri huwa wanasalimika na uhaba wa chakula kila mwaka!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom