Yuko wapi kijana mtanashati January Makamba?

Hili ni fundisho kwamba utumishi wa umma
hauna shujaa,yeyote anaweza kuutumikia umma
au akatupwa nje,mimi nikikumbuka figisufigisu
za siasa katika uchaguzi uliopita,binafsi
nilijifunza kwamba sio wote waliozifanya
walikuwa na lengo la kutumikia umma
bali wengine walikuwa na mambo yao wanayalinda.

Endapo maslahi yaliyokuwa yanalindwa
kwa kuhakikisha chama hakipotezi dola
hayasimamiwi tena bali nchi imerudi
mikononi mwa umma si ajabu
tutakosa kuwasikia wanasiasa wengi tu,

Ninachojifunza hapa ni kwamba
endapo itatokea ukapewa nafasi
ya kuutumikia umma,tenda haki
hata kama mtu awaye yote atakulaumu
historia itakulinda,kinyume na hapo unafutika mazima.
 
Kama alioleta hii thread sio mke wake basi ni dada ake february marope!! Huwezi kaniambia hawana undugu na mhusika!
 

POLITICALLY NOT political, ni gramer tu
 
January Makamba ni Mwanasiasa Mwerevu sana na hata ule uwaziri kapewa kimkakati zaid sio wa kiutendaji! Sina ruhusa ya kuzungumza malengo waliyompangia CCM ila kawekwa eneo ambalo anaepushwa na kashfa mbalimbali za kupikwa au kutengenezwa!
 
Mleta mada sijakuelewa unaposema wizara mfu
una maana gani? Kama hiyo wizara ni ngumu
kuiongoza ndo maana aliwekwa huko
aonyeshe umairi wake wa kiutendaji.
Kama hafurukuti basi alikuwa anabebwa
na wizara zilizokuwa hai tukadhani ni ubunifu wake.

Mchezo huu naufananisha na baadhi ya shule
hapa nchini,unakuta zinasifiwa kwa kufaulisha
lakini ukienda kuangalia namna wanavyochagua
wanafunzi kujiunga na shule,wanachaguliwa
wale wazuri tu,Hapa tukiwasifia waalimu ni sifa za bure.
kwani hao wanafunzi walihitaji jitihada kidogo
kuwapiga msasa ili wafaulu.

Kwa hili nampongeza rais kwa kufanya
mgawanyo mzuri wa mawaziri
kufuatana na uwezo wao,wale walioonekana
vichwa kawapa wizara ngumu ili waonyeshe uwezo
wao,wanaoshindwa kutenda tunajifunza
kwamba walibebwa na mbeleko siku za nyuma.
 
Edit: Shouting=Shooting!

Otherwise, thanks for your good input.
 
Nimeshangaa wewe kumwona mtu mmoja tu katika serekali hii ya awamu ya 5. Je, umemwona nani mwingine akisema chochote chake ka si kuambiwa cha kusema?
Acha Makamba ale mshahara wake kiulainii bila kazi. Till 2020
 
Nikizingatia haki uliyonipa kwenye mstari wa mwisho kabisa katika post yako naomba namimi nichangie.

Post yako imekaa mkao wa mtu aliyeagizwa hivi ili kuamsha hisia za watu kuwa February anabaniwa au hakutendewa haki kwenye wizara aliyopangwa na mkuu. After all sifa nyingi ulizommwagia sio zakwake.

MY TAKE
February hakuwa happy baada ya Ngosha kumteua mtu mwingine kuwa PM coz alijiaminisha yeye ndio angepewa hiyo post kwa jinsi alivyostruggle kwenye election ( Kumbuka habari iliyotrend kwenye media kuwa alikuwa anamtisha rais kwa yeye kupost picha za nguruwe na nyani kwenye wall yake insta)

Few month later akapata scandal yeye na dada yake Mwa.... kuhusu kuwadhulumu wazungu bills kwa ahadi ya kuwapa uwekezaji mkubwa.

NAHISI Ngosha aliamua kumuadhibu kwa kumtupa kwenye hiyo wizara ili asijegombana na mzee Ma-rope Senior
 
Muacheni amalizie mda wa mapumziko kwa kazi kubwa aliyoifanya wakti wa usaguz
 
Asante kwa kuitambua sifa yake kuuu.. Katika taifa hatuitaji mtu kama huyu maana anaweza kuleta maafa makubwa sana. Siku zote muogope mutu asie tenda haki hata kama katenda vibaya kwaniaba ako wew. Like wise anaweza kukugeuka wew. Dogo janja ni mtu wa mafingo fingo mengi+ kishirikina basi ndo balaa hapo. sorry kama ushirikina utaonekana kama udaku
 
Hata katibu mkuu wa chama Magufuli kagoma.?
Endapo kama January angekuwa waziri mkuu basi mh.rais angefeli sana kwa kuwa falsafa za makamba haziendani na za magufuli hata kidogo.Ila alimsaidia sana Magufuli kufika alipofika leo na Magufuli amejihisi kuwa hatokuwa mbora wa fadhila asimpomteua,ila naye magufuli kama kalazimishwa vile kwa teuzi ya January na Mosses wa Nape.?
 
kwanza wewe ni kanjanja. 'is makamba political banned' ndio nini. awamu ya tano haihitaji wasanii ila kazi tu.
makamba ni msanii kazi ndio anajifunza.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…