Yuko Chuo Kikuu ila anataka kurudia mtihani wa CSEE kama PC

Yuko Chuo Kikuu ila anataka kurudia mtihani wa CSEE kama PC

Ugali Supu

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
252
Reaction score
261
Nimekutana na jamaa m1 yuko chuo kikuu ila kwa sababu ajira ni ngumu anataka arudie mtihani wa kidato cha nne kama PC ili asafishe cheti asome certificate au diploma yeyote ya AFYA.

Anaomba ushauri wenu wakuu.
 
Watanzania tupunguze kuomba ushauri jamaniiiiiiiii hasa huku mitandaoni.. kwa nini uombe ushauri wakati data zote za maamuzi unazo wewe.

Kwa mfano huyo jamaa yako yeye ndio anajua umri wake, anajua ana malengo gani, anajua kipato cha familia yao/yake. anajua kwa nini kabla ya hapo alifeli hayo masomo.

Sasa sisi tumshauri nini akae afikilie mwenyewe na kufanya maamuzi.
 
Inawezekana tu.
Awe na nia,Na anaweza.

Ingawaje inaweza onekana kama amechelewa,Bt Penye nia pana njiaaaaaa....
 
Nimekutana na jamaa m1 yuko chuo kikuu ila kwa sababu ajira ni ngumu anataka arudie mtihani wa kidato cha nne kama PC ili asafishe cheti asome certificate au diploma yeyote ya AFYA. Anaomba ushauri wenu wakuu.

Kama sio wewe basi tuna muomba huyo jamaa hapa tumpe ushauri moja kwa moja ili naye aweze kuulizwa na kuuliza maswali/ mtengenezee ID hapa jf.
 
Mwambie asome tu, nchi hii ni ya kipekee!!
 
Chuo Kikuu Halafu Hajui Lolote
Ccm Imeiharibu Nchi Na Wananchi
Lakini Unarudiaje Nyuma Wakati Huko Mbele Umepevuka Kufanya Uamuzi Sahihi
 
kasome broo asee nafasi zipo nyingi sana na kazi za kutosha, wanaoropoka kazi hamna hawajui statistics za afya zilivo

mfno tanzania yetu yoooote ina daktari 10 tu wa figo nchi nzima
 
Aache ujinga hata sisi huku Afya tunataka tuhamie sekta nyingine sababu mshahara mdogo alaf kazi nyingi.
 
Watanzania tupunguze kuomba ushauri jamaniiiiiiiii hasa huku mitandaoni.. kwa nini uombe ushauri wakati data zote za maamuzi unazo wewe.. Kwa mfano huyo jamaa yako yeye ndio anajua umri wake, anajua ana malengo gani, anajua kipato cha familia yao/yake. anajua kwa nini kabla ya hapo alifeli hayo masomo. sasa sisi tumshauri nini akae afikilie mwenyewe na kufanya maamuzi.

Haombi ushauri huyo, anaomba comment zijae kwenye thread yake.
 
Ukimaliza kwenye afya ukakuta hakuna nafasi.Utaanza tena? Anyway uamuzi ni wako.
 
kasome broo asee nafasi zipo nyingi sana na kazi za kutosha, wanaoropoka kazi hamna hawajui statistics za afya zilivo

mfno tanzania yetu yoooote ina daktari 10 tu wa figo nchi nzima

Sasa huyo anaenda kusoma udaktari wa figo kwa cheti cha form four? kwanza hao wa figo wako7 na sio10, watano muhimbili, mmoja bugando na mmoja kcmc
 
kaka unaweza ukafa wewe nafasi yako akachukua yeye. acha kukatisha tamaa mtu asee

Usifikirie ulipo tu,fikiria miaka ijayo atakapomaliza hizo ajira zitakuepo?

Mwaka jana wanafunzi kadhaa waliomaliza masomo ya udaktari wameshindwa kufanya internship kutokana na serikali kutokua na fedha za kuwalipa, na wanaofanya wanasign mkataba wa kukubali ucheleweshwaji wa malipo sasa huyo anayeanza kusafisha cheti cha form four akija kufika huko itakuaje, aendelee tu na degree yake aliyokua anasoma.
 

Attachments

  • 1441813158341.jpg
    1441813158341.jpg
    65.2 KB · Views: 293
Hivi ukishafika Chuo kikuu ndio hupaswi kusomea vitu vingine hata kama ni kwa level ya Certificate?

Kuna kina Mugabe angeamua kuendelea kwenye fani moja nadhani kwa degree alizonazo ingebidi waongeze level nyingine baada ya u Professor.

Elimu haina mwisho, Mwambie apambane!
 
Back
Top Bottom