Young Lunya kapigwa za uso na Young Killer

Kinumbo

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,742
4,932
Zimepita siku 5 baada ya Young Lunya kuachia ngoma yake mpya ya freestyle session 5, wimbo huo kwa asilimia kubwa amemdiss Rapa Young Killer. Young Killer nae baada ya kupita siku 3 akajibu mapigo kwenye diss track aliyo ipa jina la freestyle session 6.

Killer kwenye diss track kamchana ile mbaya Lunya, nimeona jana wasafi wanamuuliza kama atajibu mapigo lakini kagoma. Kumdiss Killer kwenye track ni kujitafutia matatizo tu.

Sikiliza hapa hilo dude

 
Killer ni lyrist mzuri na nilitegemea kuona lyrical zaidi kwenye diss yake. Cha ajabu katumia muda mwingi kuchana matusi kuliko kupangilia mashairi.

Young Lunya sina shida naye maana huyu tangu kitambo simuelewagi uchanaji wake, anajitahidi kuwa na flow nzuri ila anacho flow hakieleweki.

Lunya angekuwa anaandikiwa mashairi mazuri angekuwa mbali zaidi kwasababu anajua kunata na beat.

Killer ni mchanaji mzuri ila diss yake haiendani na uwezo wake, hajaitendea haki Tamaduni.
 
Ipo hivi, anayejibu siku zote ana nafasi ya kum-out shine aliyetangulia. Kwa sababu anapata muda wa kupangilia mambo yake na pengine kutunga matusi mapya. Lakini pia, ameshapata content ya kumlambisha mwenzake.

Kwa namna yeyote, anayefuatia ana nafasi kubwa sana kuonekana kamzidi mwenzake. Labda awe kilaza tu.

Mimi hayo mambo ya muziki wa kufoka siyajui, ila nina uhakika atakayejibu mapigo ana nafasi kubwa ya kuonekana kashinda. Hata huyo sijui Killer akitoa track, kisha atokee wa kumjibu basi ataonekana kapigwa knock out.
 
Back
Top Bottom