Yaliyojiri kwenye Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281
==== Kutohudhuria kwa Lady Jay Dee na Mzee Yusuph ============
Yaani hawa watu wawili wanadharau sana,tena huyu JIDE ndo haswaa kila mwaka siku ya tuzo haji anaagiza watu tu wamchukulie tuzo. Hii binafsi naichukulia kama dharau kubwa kwa mashabiki wake wanaopoteza bundle/hela na mda kumpigia kura. Hii ndo nafasi nzuri ya kuwashukuru mashabiki kwa kusapoti kazi yake, sikumbuki mara ya mwisho huyu dada kuhudhuria ni lini na kama ni emergence basi hii ni too much.

#NAWASILISHA



====== Diamond Platnumz kuchukua Award nyingi zaidi ============
Tuzo za Kill zilipogeuka kuwa tuzo za DIAMOND baada ya kujizolea zote saba alizokuwa akiwania. Ni historia ambayo sio rahisi kuiweka na sio rahisi kusahaulika.

Binafsi namkubali kijana huyu kwa bidii zake. Naipenda pia historia ya maisha yake. Nadhani yafaa asapotiwe kwa namna moja ama nyingine afike mbali zaidi ya hapo.

Ni mwanamziki anayekutana na mengi na kuyashinda (japo mengine ya kujitakia.) Ana bidii, ana wivu wa maendeleo na malengo na uchu wa kushinda.,

Ushauri
1. Ajitahidi zaidi ya hapo
2. Ukipata muda jipige msasa kaung,eng,e ama wema akusaidie katuishen kiaina maana unaanza kufanya kazi na watu mbalimbali ambapo itakulazimu tu kutumia ung'eng'e.
3. Kwenye Website yako,vtafuta mtu anayeweza kiingereza inapotakiwa kuandika kiingereza.Maana ku sentesi moja niliona leo asubuhi kuhusu shoo flani mwanza du!!,.,,Eti,People started fainted!!"",Ukiwa na maana kwamba watu walianza kuzimia!!,past tensi haziambatanishwi hivo.
4. Punguza kujishow kila siku ama kupost vitu visivo na maana.nawala sio lazima picha 20 za tukio,weka 6-10,zatosha.Pia sio kila ukipigiwa simu unapokea hat za vichochoroni,jaribu kuwa adimu,sio kila siku kwenye ma-Blog ,diamond kasema hivi ama kafanya hiv.
5.....
mengine wataongezea wadau

Hongera sana Diamond Platinum tukopamoja kwenye MTV awards
wacha movie iendelee


==== THT kutong'ara kwenye Awards ========
'HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA' NA MWENYE MACHO HAAMBIWI ONA,,jana tumeshuhudia namna gani NGUVU YA UMMA inaweza kuleta mabadiliko.
tulishazoea,na ilikua kama kawaida sasa, MIAKA KADHAA ILIYOPITA UGAWAJI WA TUZO ZA KTMA ulikua unazingirwa na UTATA MKUBWA.lakini kubwa kulikoo ni pale vijana wa kutoka kundi la THT walipokua wananyakua TUZO nyingi ambazo hawastahili. we all know that RUGE na genge lake ndo alikua anawapa zile tuzo.Hili liliwezekana kwasababu wao ndo walikua wanahodhi mchakato mzima na waoaa ando walikua wanapendekeza majina na kuwakweka kwenye category mbalimbali,,,

mwaka huu hali imekua tofauti kidogo kwani wananchi walipewa nafasi ya kupendekeza majina ya wasanii watakoaingia kwenye category mbalimbali.LAKINI PIA TUME YA KUSHUGHULIKIA MIPANGO YOTE YA UGAWAJI WA TUZO HIZI ILIKUA COMMITED KIDOGO TOFAUTI NA MIAKA MINGINE,,,hali hii imemewafanya AKINA RUGE NA MAGENGE YAKE KUSHINDWA KUPENYEZA VIBARAKA WAO WA THT kwenye KTMA.

TEAM ANAKONDA,,,kwa kweli hili ni bao la kisigino,,kubali ukatae hili ni pigo kwa ruge na wenzake. kitendo cha LADY JAYDEE KUCHUKUA TUZO WAKATI MWANA FA HAJAPATA HATA MOJA NI PIGO KUBWA SANA.

NB,,nimefurahi sana FID Q KUCHUKUA TUZO JANA.


========= Mpoki Kuisema team Wema ==========
Meneja wa Muigizaji maarufu wa Bongo Movie Wema Sepetu amewaacha midomo wazi watu waliokuwa wamehudhuria Tuzo ya Muziki ya Kilimanjaro katika ukumbi wa Mlimani City jana baada ya kupaniki na kujikuta anajibu mapigo kwa Mc wa sherehe hiyo Silvery Mjuni anayefahamika zaidi kwa jina la Mpoki.

Meneja wa Wema aitwae Martin Kadinda amejikuta ameshindwa kuzuia hisia zake kutokana na masihara ya mpoki pale alipowaambia kuwa timu Diamond ni kikundi kinachoongoza kupost picha hata zisizo na msingi kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram,

Mpoki aliwaambia -Diamond na wafuasi wake akiwemo Wema,Martin Kadinda,Rommy Johnson kuwa -wanapost kila wakati kwa mfano wakiwawanakula, wamelala ndipo Martin Kadinda alipomwambia mpoki kuwa atafute namna nyingine ya kutafutia pesa.

Kauli ya Kadinda iliwashangaza wengi kwani licha ya kuwa Mpoki alikuwa anazungumza kimasihara lakini jambo lake linaukweli kwa kiasi kikubwa japo Kadinda alikuwa mwepesi kupanik na kushindwa kukubaliana na ukweli huo

======== Mpoki aonekana kuharibu sherehe za Awards ========
Wana jamvi ni wazi sherehe za utoaji wa tunzo(KTMA) ulikuwa umepooza kutokana na kukosa Macs wazuri hivyo kufanya hata wale walio fanywa ma MCs(Mpoki na Shadee) walizifanya zichangamke kidogo hasa Mpoki.

Ukweli ulio wazi waandaji walishindwa kutafuta MaMCs wazuri ili kuendana na sherehe husika ndio maana hata madhaifu na makosa makubwa ya Mpoki yanaweza yasionekane.

Wana jamvi kama mtakumbuka hii ni mara ya pili kwa Mpoki kushiki kama MC kwenye sherehe hizi.Kama mtakumbuka ilikuwa ni mwaka juzi na sherehe ilipendeza zaidi ya hapa maana walijua pakumuweka Mpoki.

Kwenye utoaji wa Tunzo mwaka juzi kulikuwa na Ma Mcs watatu kama kumbukumbu ziko vyema alikuwa Taji Liundi,Mpoki na Mdada nime msahau jina.


Mpoki alikuwa hatumiwi kuwa karibisha watu kutangaza mshindi bali alikuwa ana kuja kipindi cha mapumziko kuwa burudiisha watu na kukaribisha watumbuizaji tuu na walio kuwa wana baki pale juu ya stage walikuwa ni Ma MCs wawili tuu na kwakweli watu walivunjika mbavu na hakuna aliye kerwa hata chembe.

Kwa jana waandaji walichemsha kumfanya mpoki kama mmoja wa Ma MCs wanao karibisha watangazaji tunzo.
Mpoki si MC ni Mchekeshaji hivyo alitakiwa kupewa muda wake kama mwaka juzi na hii dosari imerudisha nyuma maendeleo ya sherehe hizi na
hapa waandaji mmepiga hatua mbili nyuma.

Hakuna asiye fahamu kuwa watu tunao waalika kuja kutangaza washindi wa tunzo ni watu waheshima na si vyema wakataniwa au kufanyiwa mizaa inayo pitiliza kama aliyo kuwa ana fanya Mpoki.

Kwa utani anao fanya Mpoki ni vigumu mtu mwenye heshima zake kwenye jamii kukubali kwenda kutoa Tunzo kama Mpoki atakuwa MC kwenye sherhe hiyo maana anajua atafanyiwa mizaa na ni wazi baadhi ya matamshi ya Mpoki yana kera sana na kuchukiza.

Maneno kama Mrefu kama mkojo, Mngoni wa kwanza kuzaa na mzungu,tapeli,bahiili sidhani kama yalifaa kupelekwa kwa Wageni wanao tangaza Washindi, kwakweli mengi yana wadhalilisha.

Najua wengi wataona kuwa hakukuwa na tatizo lakini tujiiulize ni wangapi watakubali kwenda kutangaza mshindi next time kama Mpoki atakuwa MC?

Ni vyema waandaji mkajiandaa kwa kutfuta Ma MCs watako mudu sherehe kubwa kama hizi si kina Shadee na Mpoki.

Mpoki ana Umuhimu wake kwenye hizi sherehe lakini si pale.



Mwisho nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa dhati Fid q na Diamond.

Karibuni wana jamvi.


=========== Mpoki Aonekana kupendezesha sherehe za Awards ============
maoni ya wadau wengi tuliokuwepo katika tuzo na wale waliofatilia mubashara (LIVE) katika luninga zao ni kwamba bila ya huyu Mzungu wa Dubai, Mujuni a.k.a Mpoki wa Ze Komedi, kungekuwa na show mbaya sana kuwahi kutokea katika ukanda huu wa afrika mashariki
waimbaji wengi waliimba Off key, Video zilikuwa Nyeupe (Washed out), Mbwembwe kibao bila lolote la msingi, Awards za kupeana kama kawaida etc etc.
na wewe uliyefatilia kama wengine ni Kweli VIBOMU vya Mpoki ndo vilinogesha show?

======== Utabiri wako juu ya Awards hizo ==========
Kama mnavyojua muda mchache kutoka sasa, watatangazwa washindi wa KTMA waliofanya vizuri 2013. Hebu tutoe utabiri wetu, nani na nani watangara siku ya leo.

========= Mganga wa Diamond kuumbuka ==========
Yule kijana alioteka vyombo vya habari kwa kusema yeye ndio amempa diamond umaarufu na kwa kuwa diamond amemkana hivyo hatokuja kupata tuzo tena.

Watu wengi walimuamini yule mganga tapeli na wakasema ndio mwisho wa diamond kimuziki.

Diamond amezibitisha utapeli wa huyo mganga kwa kuchukua tuzo 7.
Siri ya diamond ni kupiga kazi nzuri, menejimenti nzuri bila kusahau wema sepetu na diamond amekiri ilo

======== List ya Washindi wa KTMA ======
1. Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikishana ni wimbo wa
Muziki Gani - Ney Mitego Ft. Diamond.

2. Tuzo ya Msanii Bora wa Hip-hop imeenda kwa
Fid Q.

3. Wimbo Bora wa Hip-hop kwa mwaka 2014 ni
Nje ya Box - Nikki wa Pili Ft Joh Makini na Gnako.

4. Tuzo la Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili vya Tanzania ni
Bora Mchawi - Dar Bongo massive.

5. Msanii Bora Chipukizi Anayeibuka ni
Young Killer.

6. Wimbo Bora wa Zouk kwa 2014 ni
Yahaya - Lady Jaydee.

7. Wimbo Bora wa Afro Pop ni
Number One - diamondplatnumz.

8. Kwa mwaka 2014, Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall ni wa
Chibwa Ft. Juru.

9. Wimbo Bora wa Reggae imechukuliwa na
Niwe na Wewe - Dabo.

10. Wimbo Bora wa Taarabu kwa mwaka huu ni
Wasi Wasi Wako - Mzee Yusuf.

11. Tuzo ya Kikundi Bora cha Taarab imechukuliwa na
Jahazi Modern Taarab.

12. Mwimbaji Bora wa Kike - Taarab ni
Isha Ramadhani.

13. Mwimbaji Bora wa Kiume - Taarab ni
Mzee Yusufu.

14. Washindi wa Wimbo Bora wa Kiswahili Bendi kwa mwaka 2014 ni
Ushamba Mzigo - mashujaa band.

15. Mwimbaji Bora wa Kike - Bendi ni
Luiza Mbutu.

16. Mwimbaji Bora wa Kiume - Bendi ni
Jose Mara.

17. Rapa Bora wa Mwaka - Bendi ni
Ferguson.

18. Tuzo ya Bendi ya Mwaka imechukuliwa na
Mashujaa Band.

19. Mwimbaji bora wa kike kizazi kipya ni
Lady JayDee.

20. Mwimbaji Bora wa Kiume - Kizazi Kipya kwa mwaka huu ni
diamondplatnumz.

21. Wimbo bora wa R&B ni
Closer - Vanessa Mdee.

22. Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya ni
Weusi.

23. Msanii bora wa kike Taarabu ni
Isha Mashauzi.

24. Wimbo Bora wa Afrika Mashariki ni wa
Tubonge - Jose Chameleone

25. Mtunzi Bora wa Mwaka - Taarabu ni
Mzee Yusufu.

26. Mtunzi Bora wa Mwaka - Bendi ni
Christian Bella.

27. Mtunzi Bora wa Mwaka - Kizazi Kipya imeenda kwa
Diamond.

28. Mtunzi Bora wa Mwaka - Hip-hop ni
Fid Q.

29. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Bendi
Amoroso.

29. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka- Kizazi Kipya ni
Man Water

30. Hall of Fame - Individual ni
Rehan Bitchuka.

31. Hall of Fame - Institution ni
Masoud Masoud.

32. Video Bora ya Muziki ya Mwaka ni
Number One - Diamondplatnumz.

33. Wimbo wa Mwaka ni
Number One- Diamond

34. Mtumbuizaji Bora wa Kike wa Muziki ni
Isha Ramadhani.

35. Mtumbuizaji Bora wa Kiume wa Muziki ni
Diamondplatnumz
 
Kwenye Hip Hop kuna mchuano mkali sana wa nani atakua msanii bora wa Hip Hop
 
Huwa hakuna tuzo hapo ila ni zawadi tu kwa wadau wa clauds fm, hivyo tegemea wasanii wanaopata support ya Clouds fm na THT kuibuka vinara.
 
Huwa hakuna tuzo hapo ila ni zawadi tu kwa wadau wa clauds fm, hivyo tegemea wasanii wanaopata support ya Clouds fm na THT kuibuka vinara.
Nadhani kitakachowafanya wasanii unaowasema watashinda sio kwa direct support ya clouds ila ni indirect kwa clouds kuwapromo wasanii wenye uwezo mdogo na kubania wasanii wenye uwezo mkubwa na kuwapatia mashabiki ladha ya wasanii wanaowapanga wao.
 
Msanii bora wa kike tunzo inaenda kwa jide , nadhan jide mwaka huu atapat tunzo zaidi ya moja
 
Diawema ataondoka na awards nyingi kuliko wote,wema ana kisimeti bwana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom