Tupac Shakur na Notorious B.I.G Marafiki waliogeuka maadui na Kuharibu Taswira ya Hip Hop Duniani

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,582
2,000
1_MFAWB_emNljzmM-zEi9h8Q.jpeg
Kwa kizazi cha nyuma kidogo na kizazi cha hip hop nadhan washasikia sana habari za wanamuziki hawa wawili Tupac Na Biggie au B.I.G kuanzia Urafiki wao na baadaye Uhasama uliopelekea Vifo vyao. sitaki kuuza sana chai kuhusu walizaliwa wapi na kukulia wapi.najikita katika mahusiano yao kama marafiki,maadui na mwisho vifo vyao na game nzima ya Hip Hop.Tupac na Biggie walianzaje ushkaji?

mara ya kwanza kabisa Tupac anakutana na Biggie ilikuwa mwaka 1993 huko Los angeles. USA. Biggie alikuwa akiparty na washkaji kadhaa..wakati huo angalau si haba Tupac alikuwa ametoka tayari kiaina, kwenye game anafahamika.na tayari alikuwa ameashaanza kukomaa na game sana…so Biggie akaomba kwa mshkaji mmoja ambaye alikuwa ni Muuza Unga mitaa ya kati ....kuwa amkutanishe na Mchizi Tupac. Basi washkaj wakakutanishwa ,wakapeana tano na mwishowe Tupac akaona amwalike Biggie maskani kwake. Biggie akatia timu mpaka kwa Tupac. Anasema huko alishirikiana na washkaji kibao pamoja na Tupac ku fanya mambo mengi mengi na mwishowe pia pamoja masela waka share majani,msuba,ganja.… wakiwa high ile kinoma noma Biggie anasema Tupac alivuta bag flan hivi toka kabatini rangi ya kijani. Hilo bag lilikuwa limejaa miguu ya kuku na miguu ya swala (bastola na machine guns) anuai. Wakawa wakishangaa shanga jamaa jinsi alivyokuwa na mashine nzuri kabisa ambazo zilikuwa za kisasa.. na wakiwa katika hali hiyo wakawa wanachezea chezea zile guns kule uani wakikimbizana na kutishiana. Bahati nzuri hazikuwa loaded yaani hazikuwa na njugu ndani.

Basi Mchizi Tupac baadaye akaingia jikoni kupika msosi ..ingekuwa huku maybe angeenda kusonga ugali mkubwa sana na nyama choma.na si unajua tena watu wakishavuta msuba na hamu ya kula sometime huwa inaongezeka sana.. So Tupac akaingia jikoni ili afanye makaratee mezani. kucheck kwenye jokofu lake kulikuwa na nyama, akakaanga na vyepe kadhaa na mkate waka kaa chini wakapiga msosi… daahh..ilikuwa kama party flan hivi amazing na washkaji tupu. Hakukuwa na mademu. Na hapo ndo urafiki wa Biggie na Tupac ukawa umeanza.

EDI Mean anasema walipomwona mara ya kwanza Biggie walimwona kama ni rapper flan hivi mchovu… kipindi hicho Tupac na wana wake walikuwa na Group lao walilokuwa wakiliita OUTLAWZ. Tupac akamzawadia Biggie chupa ya Hennessy… kifupi ilikuwa ni siku ya kuparty sana kwa masela. Na usiku ulipofika Tupac akamkaribisha Biggie alale kwenye kochi. Hii ikawa ni kama kawaida kila Biggie akienda California alikuwa anaenda kulala kwa msela kwenye kochi lake.Siku moja Tupac akiwa ametia Team New York akaenda mpaka maskani ya Biggie akamchukua wakiwa pamoja kwenye Limousine Nyeupe. Tupac akawa anatembea tembea naye mitaa ya kati.

Na hapo ndo wakaenda Mpaka kwenye concert moja huko Madison Square Garden mwaka huo 1993 wakawa wakifanya free style…..hapo biggie akiwa ameshika Mic anaflow nakumbuka alichana mistari “ oh my God I’m dropping shit like a pigeon/I hope you re listening/smacking babies at their christenin” jamaa ni kama alipagawa kinoma yaani…. Ya know what am sayin? Cool.

Sikiliza hapa washkaji wakichana Mistari kwenye hiyo concert


So mbali na tukio hilo bado Biggie hakuwa nafahamika sana nje ya Brooklyn,Tupac ambaye alikuwa tayari anafahamika kinoma akiwa ameuza album yake kufikia mauzo ya Platinum, wakati huo huo ni mwigizaji ndo alikuwa kama anamwongoza Biggie kinamna flani. Biggie na wachanaji kadhaa waliokuwa wanachipukia.. you know.. underground rappers walikuwa wanakusanyika studio au chumba cha hotel kumsikiliza Tupac akiwapa Darsa kuhusiana na game. Tupac alikuwa anasimama kati kati yao na kuanza kuwapa darsa …haya maneno aliyasema Mshkaji wa tupac EDI Mean “ kila mtu alikuwa nasikiliza kwa makini sana mshkaji akishuka madini ile kinoma noma…tukimfuatilia kwa makini maana yeye alikuwa ameshatusua kwenye game” ila Tupac akawa anaweka msisitizo sana kwa Biggie akionesha kumkubali zaidi.

Tupac anadai yeye ndo alichangia sana kumfanya Biggie awe na style aliyokuwa nayo ya kuandika mistari.."Nilikuwa na mwambia mshkaji kuwa …kama unataka kutengeneza mapene,unapaswa urap kwa ajili ya mademu. Usiimbe kwa ajili ya machizi. Mademu watanunua nyimbo zako…na machizi huwa wanataka kile ambacho mademu hutaka” anasema Tupac huku akitabasamu kidogo.na kama ushahidi Biggie akawa anafuata Ushauri wa Tupac...hapa katika kuonesha alivyombadilisha kuna nyimbo huwa anazitaja za kipindi cha nyuma kabisa. Nyimbo kama “party and bullshit” hii ilikuwa nyimbo ya kigumu hasa ilikuwa jiwe ile kinoma yaani..na analinganisha nyimbo kama “big poppa” hii nyimbo mademu waliipenda haikuwa jiwe kama ile ya kwanza…ilikuwa nyimbo flani hvi kisponge. Biggie akaona ni bora awe karibu zaid na huyu mwana so akaomba naye aungwe kwenye group lingine la Tupac lililokuw alikifahamika kama Thug Life…. Tupac anasema “ nilimfundisha mchizi,alikuwa kama luteni wangu, msaidizi wangu kwenye game”

Lakini kabla wimbo wa “ready to die “ haujatoka Biggie alikuwa anawasi wasi kuwa usingefanya vizuri ukichukulia kuwa alikua amesaini label ya “BAD BOY. Iliyokuwa ikimilikiwa na meneja wake Sean Puffy combs a.k. Pdiddy ilikuwa bado haijakamata sana kwenye game. Na akaona kama atachelewa akijilinganisha na Tu Pac. Akawa kama analalamika flani hivi kwa mshkaji wake..yaani akitaka Tupac awe Meneja wake. Akitegemea kuwa Tupac angemsaidia kupanda kwenye chati kwa haraka sana kama yeye alivyokuwa.

Tupac alikataa hilo ombi la Biggie na kumwambia “ hapana , endelea kuwa na Puffy atakufanya uwe star”

Mwaka 1994

Mwka 1994 wakishoot film ya Above the Rim tupac alikuwa amezungukwa na kundi la warembo wakigumu akimfanyia modelling mmoja ya character wake Biride. Huyu alikuwa mchizi aliyekuwa anajihusisha na programu mbali mbali za basketball…huko alikutana na Mhaiti mmoja aliyekuwa anajulikana kama Jacques au Jack Mhaiti Agnant. Wakiwa klabu moja huko Manhattan.

Tupac aligundua yule mchizi mhaiti alikuwa amezungukwa na warembo kibao wakigida champeni na mvinyo toka kila kona ya dunia.Tupac akaomba atambulishwe kwa yule mchizi ambaye alikuwa ni mtu wa madawa ya kulevya mhuni kinoma.basi wakafahamiana na wakawa washkaji. Ikawa mara nyingi wanakuwa pamoja kwenye bar yake jamaa ilikuwa inafahamiaka kama Queens Bar. Huko huyo Mchizi wa Kihaiti alikuwa anawaleta wana nzengo mbalimbali kuperfom wakiwemo akina Shaba Ranks, Mjamaika Buju Banton, Madonna n.k (na Tupac alishawah kuwa anamchapa nao Madonna…(alisha mla) my nigger alikuwa anatembeza kichapo kila ikitokea fursa kwa mademu)

Aliyewakutanisha Tupac na Madonna alikuwa Rosie Perez miaka ya 1993 wakiwa wamehudhuria soul train awards los angeles. Biggie ambaye naye alikuwa na masela,washkaji kibao wa Kihaiti alimwonya Tupac kuwa akae mbali na Jack Mhaiti maana jamaa alikuwa ni gang way hasa doesn’t give a **** ..you know what am saying? So Biggie mwenyewe tu alikuwa ana mhara yule Jack akaona amtonye mwana kuwa huyo jamaa si mtu mzuri sana. Ila Tupac alipenda sana ile kampan maana naye akaanza kujiona sasa anaogopwa na kutambulika kama ni mchizi mbabe ile kinoma. Huko akafahamiana na watu wengi sana na hasa alikuwa akizimia swaga za Jack za kuvaa Madini kibao shingoni,bling bling,vidole vya thaman (pete za thaman) n.k Tupac akawa anaye anaanza kuiga swaga za jack Mhaiti. Tupac alikuwa anapenda sana kutambulika…yaani akiwa sehemu anataka maachizi na mademu watambue yupo na wawe wana mgwaya.

Party katika Klabu ya Manhattan

Tupac na Mchizi siku moja walikuwa wakiparty katika klabu ya manhattan mwaka 1993 ilikuwa November…. Tupac akakutana na binti mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Ayanna Jackson alikuwa na miaka 19. Walikuwa wanacheza pamoja pale klabu na baadaye wakaondoka pamoja kwenda kwenye hotel aliyokuwa amefikia Tupac iliyokuwa ikiitw Le Parker Meridien Hotel ili akamchape nao. Siku nne baadaye wakakutana tena hotelin safari hii hakumkuta Tupac peke yake..alimkuta na masela akina Jack Mhaiti na Charles huyu alikuwa jamaa ndo anaratibu mizunguko yote ya Tupac na jamaa mwingine ambaye hakutambulika kwa jina. Yule binti anasema wale jamaa “walimpiga mtungo” na kumlazimisha awanyonye mashine zao.kifupi walimbaka. Tupac anadai yeye aliondoka bedroom walipoingia wale wengine na akapitiwa na usingizi so anadai hakushiriki. Yule bint aliita polisi.tupac,jack na Charles wakakamatwa.polisi pia walikuta kuna bunduki ambazo Tupac alidai zilikuwa ni za Biggie.

Tupac anashtakiwa kwa kosa la kubaka na Beef lake la Mhaiti
Tupac akashtakiwa kwa kubaka na pia kusodomize,pia kukutwa na silaha kinyume na sheria. Na hizo silaha inasemekana alikuwa amemtoa yule bint Ayanna Jackson kama zawadi kwa washkaji zake wamchape nao. Tupac alikataa hili ingawa baada ya kuhukumiwa alikuwa akijilaumu kwa kuwa hakuweza kumlinda Jackson asibakwe na jamaa zake. Jack yeye akakubal makosa mawili na kuepuka kwenda Jela…. Tupac akiamini kuwa yule Mhait alimsnitch wakati akihojiwa na gazeti la New York Daily News alimwambia mwandishi kuwa Jack alimuuza.( Jack Mhaiti na Aynna Jackson walikanusha jambo hili.)

Tupac kumlaumu Mchizi kama Jack kwenye vyombo vya habari alikuwa amekosea sana…sema tayari naye alishaanza kujiona kama amekuwa Mbabe sababu tu ya ile kushinda shinda na Jack.Alishajiona naye ni Mwamba akitembea mitaani amevaa Bling bling za thamani sana kibao kibabe. Akiamini hakuna mtu ambaye ange mess naye… yaani sasa watu wasingemletea ya kuleta maana alishajiona naye amekuwa Mbabe flani hivi kitaa.

Akiwa anasaidia ndugu zake kifedha na pia pesa zilitumika kulipa mawakili wakati wa kesi yake…accounts zake zikaanza kukonda…mapene yakawa yanakata… na mwishoni mwa mwaka 1994 alikubali kurecord mstari mmoja kwa ajili ya rapper mmoja aliyekuwa akiiitwa Little Shawn ambaye alikuwa karibu sana na Pufyy na Biggie. Na mwaliko huu ulitoka kwa Meneja wa Little Shawn bwana Jimmy Henchman Rosemond… ambaye huyu alikuwa amefahamiana ana Tupac kupitia Jack Mhait na tupac akataka alipwe USD 7,000. Just imagine. Jama alishaanza kuwa choka mbaya kiuchumi.

Shambulio dhidi ya Tupac
Basi November 30 mwaka 1994 Tupac akawa anawasilli Quad Recording studios huko Times Square. Alikuwa ameenda na washkaji watatu na kati ya hao hakukuwa na bodyguard wakakutana na masela watatu ambao hawakuwafaham wakiwa wamevaa mavazi kama ya jeshi. Hii ilikuwa ni fashion huko Brooklyn ambako ndo makazi ya Biggie. Hivyo tupac akaamini kusingeweza kuwa na so lolote lile.akajisikia fresh aliposikia Lil Cease ambaye alikuwa pia ni rapper mshkaji wa Biggie alipowaambia kwa saut kuwa Biggie pia alikuwa Ghorofani akirecord. Na Puffy alikuwepo huko pia.

Lakini kabla Tupac na masela wake hawajapanda kwenye ngazi wale jamaa wakatoa miguu ya kuku (9mm guns) na kuwaambia walambe mchanga..yaani walale chini. Badala yake Tupac akataka anaye atoe mguu wa Kuku..jamaa wakamshoot na kumpa kichapo hasa, wakamnyang’anya madini aliyokuwa amevaa..kumbuka kipindi hicho Tupac ni mtu wa Bling Bling sana.then wakamwacha hasa baada ya Tupac kujifanya ame danja. Jamaa wakaondoka.akajivuta vuta akaapanda lift na kuelekea juu..mlango ulipofunguliwa aliona kundi akiwepo Puffy , Biggie na Henchman. Tupac anasema aliwaona kama wote wameshtuka na kujisikia kama wamemkosea hivi. Ingawa Puffy anadai kuwa hakuna kibaya walichofanya zaidi ya kumwonesha upendo na kusikitishwa na tukio lile.

Tupac akawa anaaamini kuwa lile tukio halikutokea tu ..lilipangwa. anasema walikuwa wanamchukia… anadai alipigwa risasi tano moja ikiwa kichwani , nyingine ilipita kwenye Mapumbu ingawa wachunguzi wanadai kuwa ni kama aliji shoot yeye mwenyewe. Bill Courtney huyu alikuwa polisi mstaafu wa NYPD yeye anasema ile ilikuwa ni kumpa onyo siku nyingine asifanye masikharana watu kama akina Jack Mhaiti..maana kumtaja kwenye Magazeti alikuwa amemharibia sana mshkaji wa Ngada. So ile ilikuwa wanatoa funzo.Kumbuka pia Biggie alimwonya mapema sana Tupac kuwa kaa mbali na Mchizi…unajua watu wa Ngada hawana urafiki wa kudumu.

Henchman alikaririwa akimwambia Tupac kupitia Vibe 2005…..”hakuna aliyekuja kukupora kitu, walikuja kukutia nidhamu”

Puffy na Biggie walikataa kabisa kuhusika na tukio hilo na walidai hawakuwa hata na taarifa kama lingekuwepo. Jack Mhaiti naye alikataa kuhusika na tukio hilo… na aliendelea kuwa na kesi mbalimbali mpaka mwaka 2007 aliporudishwa kwao.

Tarehe 1 december Tupac aliingia Mahakama ya New York akiwa amevaa bandeji na akisukumwa kwenye kiti cha matairi na siku hiyo akahukumiwa kufungwa kwa kesi ya Ayanna Jackson.ya ubakaji hukumu ikapunguwa kuwa ya mwaka mmja na nusu na pia kuwa angewekewa dhamana ya USD Million 3.

Jamaa alikuwa choka mbaya hakuweza kupata hizo pesa.so wakawa wamemweka kwanza segerea ya huko iliyokuwa ikifahamika kama Clinton Correctional Facility….. na hapo aliichia album yake ya “Me Against the World “ mara baada ya kuanza kutumikia kifungo chake. Alikuwa tayari ameshachoka na usanii sanii kwenye music industry ila sasa kawa anapewa pewa maneno ya kidaku na washkaji hasa gerezani kuwa Biggie alikuwa anajua mchongo mzima way eye kuja kushambuliwa pale studio.

"me against the world"

nilikuwa nmemfanyia mengi sana zaidi ya yeye kugeuza kichwa na kujifanya hajui kuwa machizi walitaka kunipasua kichwa” alizungumza Tupac baadaye. “Na hata kama Biggie haku panga, hakunichomea bas angalau alipaswa afaham nani alifanya hilo jambo kwa sababu hilo jambo lilitokea kitaani kwake kabisa….hawa machizi walikuwa ni wana wa pale pale kitaa

Akiwa segerea Tupac akamwambia mkewe Keisha Morris kumpelekea ujumbe Suge Knight….. huyu alikuwa ndo kichwa cha Death Row Records kuwa alikuwa majalala so anaomba apigwe tafu. Amsaidie kumlipia ada za mawakili na pia kuwa nyumba ya mama yake ilikuwa inakaribia kuuzwa.

Suge akamtumia Tupac Usd 15,000 na kuziweka katika kumbukumbu. Reggie Wright Jr huyu alikuwa ni Mkuu wa ulinzi wa Death Row anasema Tupac alifurah sana na akatuma ujumbe mwingine kuwa angependa aonane na Suge.

Basi Suge akawa akimtembelea na baadaye Death Row wakamsaidia kitu ambacho hakuna mwingine angeweza msaidia.kuachiwa huru. Mwanasheria wa Death Row David Kenner alisema angeweza msaidia Tupac wakate rufaa. Ukiangalia wanasema Suge hakuwa akijaribu kumweka Tupac chini ya Label yake…ila alikuwa anajaribu kumchukulia kama ni mwanagenzi..yaani mwanafamilia mwenzao. Na hii ilikuwa ni familia kubwa sana yenye nguvu katika hip hop.

Mpaka august 1995 Tupac alikuwa bado ananyea debe wakati suge alipoenda kumtembelea tena ..baadaye Suge alirudi New York City ambako tarehe 13 mwezi huo huo kulikuwa ni tamasha la hip hop la kila mwaka huko Madison Square Garden Paramount theater.Death Row walitumia zaidi ya Dollar 100,000 kutengeneza Stage show iliyokuwa inafanana na Seli au chumba cha gerezani.

Kifua chake kikiwa kimetuna suge alisimama jukwani na kupokea tuzo ya label yake kwa kutoa soundtrack bomba “above the rim” akiwa hapo akaonekana kama kuwa diss jamaa wengine akina Puffy Combs ambaye alikuw ani kiongozi wa Bad Boy na Biggie Smalls. Suge akasema” msanii yeyote anayetaka kutoka kimuziki,anayetaka kuwa nyota ambaye hataki kuwa na mashaka ya kuwa na watu wakali kwenye kuproduce video kali na anayetaka kuwa kwenye videos zote na records,kucheza n.k aje Death Row”

Ule ukumbi ukalipuka kumzomea. Kwa nini alifanya hivyo? Aliwaza hivyo Rapper wa death row akifahamika kwa jina la Nate Dogg.

Nini kilimfanya Suge atoe shambulizi kama hilo kwa Puffy?ukichukulia wao hawakuwahi kuwa na ugomvi na walikuwa wakiheshimiana vizuri tu. Na mara kadhaa walikuwa wakikutana kujadiliana namna ya kuwaepuka Feds yani US Federals katika shughuli zao. Mwaka 1995 Suge alikuwa amemwalika Biggie Smalls kuperform kwenye Kablu yake ya 662 huko Las Vegas. Ingawa kwa bahati mbaya hiyo show haikufanyika lakini hilo halikuharibu uhusiano wao.

Tupac ndiye aliye harib uhusiano wa Suge na Bad Boys.


Kutoka hapo Suge alisafiri mpaka gereza alilokuwa amefungwa Tupac. Huko Tupac si tu kuwa alikubali kufanya kazi na Suge bali alielezea jinsi ambavyo alikuwa na kinyongo na Biggie na akasema kabisa anaamini hawa walihusika na lile shambulio. Tupac akamwambia Suge “Nitaiharibu Bad Boys Records" Na hapo Suge akamhakikishia kuwa Maadui wake yeye Tupac watakuwa maadui wa Suge.

Kuanza kwa vita vya mistari kati ya East Coast and West Coast

Vita vya mistari kwenye nyimbo vilianzia kwenye Tuzo za Source. Ingawa hakukuwa na ushahidi wowote wa kuwa Biggie au Puffy walikuwa wanajua lile shambulio la Tupac mapema.yeye tupac alishatangaza vita dhidi yao.na tupac aliamini kuwa hili jambo lingetumika vizuri kumshawishi sana Suge kuongezea Beef katika mahusiano yao ambayo mwishoni yalisababisha vifo kwao wote wawili. Ndipo tupac akatoa wimbo wa “hit em up” ambapo humo aliwa diss kinyama Biggie na Puffy…na label yao ya Bad Boys. Aliwadiss kiroho mbaya. Alienda mbali zaidi katika wimbo huo akazungumzia jinsi ambavyo alikuwa anamkaribisha Biggie alale kwenye kochi lake kule home kwake na katika kuharibu akasema kuwa alimchapa nao mke wa Biggie( he fucked mke wa Biggie..hapa inasemekana alikuwa ni Faith Evans) hili jambo Biggie alipoulizwa alisema yeye hana la kusema kwa kuwa hakuwa na uthibitisho wowote katika hilo. Tofaut na Tupac. Biggie alionekana kuwa mbali kiasi na huu ugomvi.hakupenda sana hata kuzungumzia suala hili.
"hit em up" Tu Pac

[Intro: 2Pac]
I ain't got no motherfuckin' friends
That's why I fucked yo' bitch, you fat motherfucker!
(Take money) West Side, Bad Boy killas
(Take money) You know who the realest is
(Take money) We bring it too
(Take money)

[Verse 1: 2Pac]
First off, **** yo' bitch and the clique you claim
Westside when we ride, come equipped with game
You claim to be a player, but I fucked your wife
We bust on Bad Boys, niggas fucked for life
Plus, Puffy tryna see me, weak hearts I rip
Biggie Smalls and Junior M.A.F.I.A. is some mark-ass bitches
We keep on comin' while we runnin' for your jewels
Steady gunnin', keep on bustin' at them fools, you know the rules
Lil' Caesar, go ask your homie how I'll leave ya
Cut your young-ass up, leave you in pieces, now be deceased

Lil' Kim, don't **** around with real G's
Quick to snatch yo' ugly ass off the streets, so **** peace!
I'll let them niggas know it's on for life
Don't let the Westside ride tonight (ha ha ha)
Bad Boy murdered on wax and killed
**** with me and get yo' caps peeled, you know

[Hook: 2Pac]
See, grab your Glocks when you see 2Pac
Call the cops when you see 2Pac, uh

Who shot me? But you punks didn't finish
Now you 'bout to feel the wrath of a menace
Nigga, I hit 'em up!

[Interlude: 2Pac]
Check this out, you motherfuckers know what time it is
I don't even know why I'm on this track
Y'all niggas ain't even on my level
I'ma let my little homies ride
On you bitch-made ass Bad Boy bitches, feel it!


[Verse 2: Hussein Fatal]
Get out the way yo, get out the way yo
Biggie Smalls just got dropped

Little Moo', pass the MAC
And let me hit him in his back
Frank White needs to get spanked right for settin' traps
Little accident murderer
And I ain't never heard of ya
Poisonous gats attack when I'm servin' ya
Spank ya, shank ya whole style when I gank
Guard your rank 'cause I'ma slam your ass in the paint
Puffy weaker than the fuckin' block I'm runnin' through, nigga
And I'm smokin' Junior M.A.F.I.A. in front of you, nigga
With the ready power
Tucked in my Guess
under my Eddie Bauer
Your clout petty/sour
I push packages every hour; I hit 'em up!

[Hook: 2Pac]
Grab your Glocks when you see 2Pac
Call the cops when you see 2Pac, uh

Who shot me? But you punks didn't finish
Now you 'bout to feel the wrath of a menace
Nigga, I hit 'em up!

[Verse 3: 2Pac]
Peep how we do it, keep it real as penitentiary steel
This ain't no freestyle battle, all you niggas gettin' killed
With your mouths open

Tryna come up off of me, you in the clouds hopin'
Smokin' dope, it's like a sherm high

Niggas think they learned to fly
But they burn, motherfucker, you deserve to die

Talkin' about you gettin' money, but it's funny to me
All you niggas livin' bummy — why you fuckin' with me?

I'm a self-made millionaire
Thug livin', out of prison, pistols in the air (ha ha)
Biggie, remember when I used to let you sleep on the couch
And beg a bitch to let you sleep in the house?

Now it's all about Versace, you copied my style
Five shots couldn't drop me, I took it and smiled
Now I'm back to set the record straight
With my AK, I'm still the thug that you love to hate

Motherfucker, I hit 'em up!

[Verse 4: Kadafi]
I'm from N-E-W Jers' where plenty of murders occurs
No points or commas, we bring drama to all you herbs
Now go check the scenario: Lil' Cease
I'll bring you fake G's to your knees, coppin' pleas in de Janeiro
Little Kim, is you coked up or doped up?
Get your little Junior Whopper click smoked up
What the ****, is you stupid?
I take money, crash and mash through Brooklyn
With my click lootin', shootin' and pollutin' your block
With a 15-shot cocked Glock to your knot
Outlaw MAFIA clique movin' up another notch
And your pop stars popped and get mopped and dropped
All your fake-ass East Coast props brainstormed and locked

[Verse 5: E.D.I. Mean]
You's a beat biter, a Pac style taker
I'll tell you to your face you ain't shit but a faker

Softer than Alize with a chaser
About to get murdered for the paper
E.D.I. Mean approach the scene of the caper
Like a loc, with Little Ceas' in a choke
Gun totin' smoke, we ain't no motherfuckin' joke
Thug Life, niggas better be knowin'
We approachin' in the wide open, gun smokin'
No need for hopin', it's a battle lost
I got 'em crossed as soon as the funk is boppin' off
Nigga, I hit 'em up!

[Outro: 2Pac]
Now you tell me who won
I see them, they run, ha ha
They don't wanna see us

Whole Junior M.A.F.I.A. clique dressin' up tryna be us
How the **** they gonna be the mob
When we always on our job?

We millionaires
Killin' ain't fair, but somebody gotta do it

Oh yeah, Mobb Deep, you wanna **** with us?
You little young-ass motherfuckers
Don't one of you niggas got sickle-cell or somethin'?
You're fuckin' with me, nigga
You **** around and have a seizure or a heart attack

You better back the **** up
Before you get smacked the **** up
This is how we do it on our side
Any of you niggas from New York that wanna bring it, bring it!
But we ain't singin', we bringin' drama
**** you and yo' motherfuckin' mama!
We gon' kill all you motherfuckers!
Now when I came out I told you it was just about Biggie
Then everybody had to open their mouth
With a motherfuckin' opinion

Well, this is how we gonna do this: **** Mobb Deep! **** Biggie!
**** Bad Boy as a staff, record label and as a motherfuckin' crew!
And if you wanna be down with Bad Boy, then **** you too!
Chino XL, **** you too!
All you motherfuckers, **** you too!
(Take money, take money)
All of y'all motherfuckers, **** you, die slow!
Motherfucker, my .44 make sho' all y'all kids don't grow!

You motherfuckers can't be us or see us
We motherfuckin' Thug Life ridas,
Westside 'til we die!
Out here in California, nigga, we warned ya

We'll bomb on you motherfuckers! We do our job!
You think you mob? Nigga, we the motherfuckin' mob!
Ain't nothin' but killas
And the real niggas, all you motherfuckers feel us
Our shit goes triple and 4-quadruple
You niggas laugh 'cause our staff got guns under their motherfuckin' belts
You know how it is: when we drop records, they felt
You niggas can't feel it, we the realest
**** 'em, we Bad Boy killas!

tupac akasema ataua mpaka watoto wa Biggie.... kiuhalisia jamaa alikuwa kama mtu aliyejeruhiwa aliyejawa na chuki ile kinyama dhidi ya Biggie.
Kumbuka pia alishatoa kibao cha “Me against the World “ kipindi kile anaenda gerezani. Akimwaga machungu yake katika wimbo huo pia. Aliwachana sana Biggie na Puffy na Bad Boys kwa ujumla.


Notorious BIG akaamua kumjibu Tupac kwa wimbo “Who shot ya?” katika album ya Born gain
Who Shot Ya

The Notorious B.I.G.

As we proceed
To give you what you need
9 to 5 motherfuckers
Get live motherfuckers
As we proceed
To give you what you need
9 to 5 motherfuckers
Get live motherfuckers

Now turn the mics up (As we proceed)
Turn that mic up, yea that beat is knockin', need that mic up tho (To give you what you need)
Turn that shit the **** up (East coast motherfuckers)
Uh, what? (Bad Boy motherfuckers)
Turn it up louder
Yea, uh

As we proceed, to give you
What you need
J.M. motherfuckers
J.M. motherfuckers
9 to 5 motherfuckers

Who shot ya?
Seperate the weak from the ob-solete
Hard to creep them Brooklyn streets
It's on nigga, **** all that bickering beef
I can hear sweat trickling down your cheek
Your heartbeat sound like Sasquatch feet
Thundering, shaking the concrete
Finish it, stop, when I foil the plot
Neighbors call the cops said they heard mad shots
Saw me in the drop, three and a quarter
Slaughter, electrical tape around your daughter
Old school new school need to learn though
I burn baby burn like Disco Inferno
Burn slow like blunts with yayo
Peel more skins than Idaho potato
Niggas know, the lyrics molestin' is takin' place
Fuckin' with B.I.G. it ain't safe
I make your skin chafe, rashes on the masses
Bumps and bruises, blunts and Land Cruisers
Big Poppa smash fools, bash fools
Niggas mad because I know that cash rules
Everything around me two Glock 9s
Any motherfucker whispering about mines
And I'm Crooklyn's finest
You rewind this, Bad Boy's behind this

As we proceed
To give you what you need
9 to 5 motherfuckers
Get live motherfuckers

As we proceed
To give you what you need
East coast motherfuckers
Bad Boy motherfuckers

Get high motherfuckers
Get high motherfuckers
Smoke blunts motherfuckers
Get high motherfuckers
Ready to die motherfuckers
9 to 5 motherfuckers

I seen the light excite all the freaks
Stack mad chips, spread love with my peeps
Niggas wanna creep, gotta watch my back
Think the Cognac and indo sack make me slack?
I switches all that, cocksucker G's up
One false move, get Swiss cheesed up
Clip to TEC, respect I demand it
Slip and break the 11th Commandment
Thou shalt not **** with nor see Poppa
Feel a thousand deaths when I drop ya
I feel for you, like Chaka Khan I'm the don
Pussy when I want, Rolex on the arm
You'll die slow but calm
Recognize my face, so there won't be no mistake
So you know where to tell Jake, lame nigga
Brave nigga, turned front page nigga
Puff Daddy flips daily
I smoke the blunts he sips on the Baileys
On the rocks, tote Glocks at christenings
Hammer cock, in the fire position and

Get live motherfuckers
Ready to Die motherfuckers

Come here, come here
Open your fucking mouth, open your, didn't I tell you don't **** with me? Huh?
Didn't I tell you not to **** with me?
Huh? Look at you now
Huh?
Can't talk with a gun in your mouth huh?
Bitch-ass nigga, what?
(Get live motherfuckers)

As we proceed (Who shot ya?)
To give you what you need
9 to 5 motherfuckers
Get live motherfuckers
Get high motherfuckers (Who shot ya?)
Ready to die motherfuckers

As we proceed (Who shot ya?)
To give you what you need
9 to 5 motherfuckers
East coast motherfuckers
(Who shot ya?)
West coast motherfucker
West coast motherfuckers

As we proceed
To give you what you need
As we proceed
To give you what you need

Get live motherfuckers
Get live motherfuckers
9 to 5 motherfuckers
Get money motherfuckers

As we proceed
To give you what you need
9 to 5 motherfuckers
Get live motherfuckers
9 to 5 motherfuckers

J.M. motherfuckers
J.M. motherfuckers

As we proceed
To give you what you need

NANI NA KWA NINI ALIMUUA TUPAC?
NANI ALIKUJA KUMUUA B.I.G NA KWA NINI?

NITAENDELEA.
 

shirley myles

JF-Expert Member
May 19, 2018
917
1,000
Ila hapo kwenye outlaws si kweli,outlaws ilikuja baadae sana muda mchache kabla PAC hajafariki
 

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,582
2,000
Hujui kitu... Ungenyamaza au ungeuliza ila si kukosoa kitu usichokifaham. Mimi naandika kitu ninachokifaham. Sibahatishi.haya nayokwambia nayafaham. Kundi la outlawz alilianzisha tupac mwishon mwa mwaka 1995 baada ya kutoka jela. Sijui kama ulikuwa umezaliwa au ulikuwa na akili that time. Uliza kwa wenye uelewa.

Ila hapo kwenye outlaws si kweli,outlaws ilikuja baadae sana muda mchache kabla PAC hajafariki
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
39,631
2,000
hahaha Kumbe Big " ni kinyago " "kilicho chongwa na PAC ""... Iweje tena "" kikawa kinataka kumtisha " mchongaji "" wake ""...!??
 

shirley myles

JF-Expert Member
May 19, 2018
917
1,000
Nilikuwa nachana sana mistari toka enzi za akina saleh jabir. Mi mwana hip pop toka miaka ya naughty by nature, nas,warren g, Wu tang clan, beastie boys, salt n pepa n.k
Duh!!!! Heshima yako,hivi tape za naughty by nature mlikuwa mnazipataje kipindi kile wakati kulikuwa hamna internet
 

mzee wa liver

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
75,053
2,000
Hujui kitu... Ungenyamaza au ungeuliza ila si kukosoa kitu usichokifaham. Mimi naandika kitu ninachokifaham. Sibahatishi.haya nayokwambia nayafaham. Kundi la outlawz alilianzisha tupac mwishon mwa mwaka 1995 baada ya kutoka jela. Sijui kama ulikuwa umezaliwa au ulikuwa na akili that time. Uliza kwa wenye uelewa.
Mkuu uko sahihi kabisa
 

shirley myles

JF-Expert Member
May 19, 2018
917
1,000
Hujui kitu... Ungenyamaza au ungeuliza ila si kukosoa kitu usichokifaham. Mimi naandika kitu ninachokifaham. Sibahatishi.haya nayokwambia nayafaham. Kundi la outlawz alilianzisha tupac mwishon mwa mwaka 1995 baada ya kutoka jela. Sijui kama ulikuwa umezaliwa au ulikuwa na akili that time. Uliza kwa wenye uelewa.
Kweli mkuu nilikuwa nanyonya kipindi hicho upo sawa kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom