Young Killer(Msodoki) - Sinaga swagger (remix)

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,874
Hii mistari imeenda shule.


dubu!!

ukiona una changa moto
we unachanga unga mnatoa dongo
mungu wetu sote hawezi kubali pokea hongo
young killer ni mdogo mungu ni mkubwa
mswahili ni yule atayekosa kampani
hawezi kwenda na muda
why unachana wenzako
umekuwa kiburi haswa siku hizi unadharau umejisahau umekuwa mtata
maana toka damu huku mwanangu umekuwa sasa
nenda kafanye umalaya huku ukila zako bata
na ukipata basi usisahau utokako
ukikosa jifiche uone ni nani atakupa ta**
ili uzipate pesa uzwe hustler
maana hazishikiki wanazo viongozi wako ambao kustaafu mpaka wafariki
sijui nitapotezwa na nini
nnachojua kuwa dar hawana udongo wa kunitengeneza mimi
nimezaliwa na cheka furaha tumbo moja na mimi
ni yule mkaa kimya halafu unaponzwa na ulimi
amini, fanikio ilipo maadui wengi
na pasipo na pesa basi hakuna mapenzi
so kama haileti hela basi hai-make sense
no sweat kisela ukiona natema we meza tenzi
washenzi wanasema anakonda eti mwili unakosa ladha
wakanichome kwa makonda ya kwamba nakula ngada
huwezi jua huenda natumia labda
kwakuwa uchunguzi unaendelea kwahiyo msije kushtuka nkitajwa
brothers wanaongea sana mwisho watazima
hawajui kuwa uwoga ndio kitu nilichonyimwa
ila naogopa ukimwi coz ndo gonjwa lenye heshima
na toka nimebalehe sijabahatika kupima
nyie kima mi sijafunzwa kulelea vitu
mkizingua nawachana kama bifu iwe bifu
usiaminishwe we ni mkali hauna kitu
kubomoa mziki wetu ambao tunahangaika kuujenga kila siku
na hii kitu inanifanya niumie
nnapoona soko linabana wanaojua sana wengi wavulie
na usawa unakaba haswa
so inabidi utulie
yani usipigane ukang'ata yaani bora ukimbie
asikwambie mtu kitu babu kuishi na watu tabu
ukipendwa ringa ukichukiwa wewe jipe shavu
sikuhizi hakuna love maisha ni ya kipumbavu
dada zetu wanapewa mimba kisa chips kavu
mdogo wao naulizwa ni lini ntakuwa hero
maana sisomeki kwenye top 10 wala top 0
uzito ukifika kilo basi mwisho wa kusota
usingizi mbolea ndo maana ukishalala unaota
ushanikosa kaka chaka ulioingia ni kambi ya masoja
we kibaka mtumia nguvu kibao akili kisoda
acha uwoga hata hutofika mbali kama kuku aliyekula mchele jiona na yeye akaliwa na wali
sio madogo tu sikuhizi wanaogopa mpaka wakubwa
hii harufu ya gogo haja nnayotoa hapa ni kubwa
usipoteze muda kula msuba chanja mbuga
naienjoy maisha mungu anipe nini makmuga
nishavurugwa bosi nilipe nisepe
maumivu ya kazi mwisho furaha nipe nicheke
kwa hali ya magufuli nikihonga demu kiepe
ni lazima nimtembeze rugu kwa mledi kipepe
funga bakuli lako we mi sio mchizi wako
nasema chako ni changu , changu hakiwezi kuwa chako
unaforce niwe njia yako, unafanya nicheke
unalazimisha yai la chupa ya chai kulipikia kiepe
tofauti ya mi na wewe mimi na wewe
sasa majungu ya nini mtoto wa kiume mwisho uolewe
mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe
sa timu za nini mwisho kaburini unaingia mwenyewe
ukipenda ua basi unapenda na boga
shida kupenda kimoja ni ugonjwa usiokuwa na tiba
kwahiyo ukimpenda diamond unampenda na ali kiba
coz me na wewe ni raha na hawa wote ni shida
zinazofanya tu tugombe ni dawg ndo mpaka tunachukiana na mwisho tutoane roho
na kujifanya ma-ganster kumbe ndani bishoo
kupandisha mapresha mguu wa shingo na roho
we bishoo nani kwake yeye
unachukia nimemdiss joh kuliko hata alivyochukia yeye
naona umetumwa eeh basi utambue mi sio kinyonge
na mwanza hamnirudishi hata kwa kafara la ng'ombe
na sihofii chochote me nafika nitakapo
arusha napita fresh na my brother fidovato
tunapiga mitungi mwendo wa ganja na sato
na ukini-nukuu vibaya ni wewe na mungu wako
ndo naishia hapo
 
Hapa sasa haha!!

hii harufu ya gogo haja nnayotoa hapa ni kubwa
 
ukikosa jifiche uone ni nani atakupatako
Yaani ukikosa jifiche hakuna atakaye kupata.
 
unalazimisha yai la chupa ya chai kulipikia kiepe
 
Hii ni diss noma kabida kakusanya wote na kuwabwaga. Sijui nani mwana rap hapa atasimama na kuijibu.
Maana naona ile ya kwanza wote wamekaa kimya naogopa aisee. Dogo anatoa nondo zilizopotea muda mrefu.
 
Dogo ni talented anajua kuandika unaona kabisa kuna akili imetumika na kwenye ngoma zake kuna mistari konzi kibao,anahitaji kupewa miongozo tu kesho aje kua mkubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom