Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 48,448
- 115,581
.
Kikosi cha Yanga huenda kikaelekea mkoani Mwanza kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa, ikiwa mkoani Mwanza Yanga inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki, mmoja ukiwa wa Kimataifa dhidi ya timu kutoka Kenya
Yanga ina muda wa kutosha kujiandaa na mchezo dhidi ya ZESCO kwa kuwa kwa sasa ligi zimesimama kupisha michezo ya kalenda ya FIFA
Mchezo wa kwanza dhidi ya ZESCO utapigwa kati ya Septemba 13-15 jijini Dar es salaam na wa marudiano utacheza Zambia wiki mbili baadae.
Yangafulldoz.