Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20190830_054039.jpg
YANGA KUWEKA KAMBI MWANZA
.
Kikosi cha Yanga huenda kikaelekea mkoani Mwanza kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa, ikiwa mkoani Mwanza Yanga inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki, mmoja ukiwa wa Kimataifa dhidi ya timu kutoka Kenya

Yanga ina muda wa kutosha kujiandaa na mchezo dhidi ya ZESCO kwa kuwa kwa sasa ligi zimesimama kupisha michezo ya kalenda ya FIFA

Mchezo wa kwanza dhidi ya ZESCO utapigwa kati ya Septemba 13-15 jijini Dar es salaam na wa marudiano utacheza Zambia wiki mbili baadae.

Yangafulldoz.
 
20190903_080425.jpg
Uongozi wa klabu ya Yanga Jana Umetimiza ahadi yao ya kuwapatia wachezaji kiasi cha shilingi milioni hamsini baada ya kufanikiwa kuwaondosha Township Rollers ya nchini Botswana katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Saad Kimji amesema kwamba fedha hizo atakabidhiwa meneja wa timu hiyo kwa ajili ya kuziwasilisha kwa wahusika.

Kimji ameiambia @daboten kwamba lengo la uongozi ni kuona wachezaji wanatimiziwa mahitaji yao ili na wao waweze kuyafanya majukumu yao kwa ufasaha.

Kabla ya kuwavaa Township Rollers kwenye mechi ya pili uongozi wa Yanga ulitoa ahadi ya kuwapa wachezaji na benchi la ufundi kiasi cha shilingi milioni hamsini endapo wangefanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano hayo,jambo ambao lilitimizwa na wachezaji hao. - Yangafulldoz.
 
20190903_080841.jpg
SAFU YA ULINZI YA YANGA IMETIMIA "YONDANI-
.
Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani, amesema timu hiyo kwa sasa ina safu bora ya ulinzi ukilinganisha kipindi cha misimu miwili iliyopita

Tangu kuondoka kwa beki Vicent Bossue na baadae kustaafu Nadir Haroub, safu ya ulinzi ya Yanga iliyumba

Hata hivyo baada ya usajili wa wachezaji wapya, Yondani anasema ukuta wa Yanga umeimarika "Ukiangalia kiwango cha mchezaji mmoja mmoja, kwa maana ya Lamine, Godfrey na Sonso, ukigeukia kwa makipa, tuna kijana mdogo Metacha pamoja na Shikalo, wote wanayajua majukumu yao," amesema "Kwa muda mfupi na mechi tulizocheza, nafurahishwa na aina ya uchezaji wa mabeki katika zoezi la kuokoa mipira na kupunguza hatari langoni, hili linanipa faraja kuwa tuna uwezo wa kupata matokeo mazuri katika mashindano tunayocheza" "Hata kama mmoja wapo akikosekana, tuna uhakika waliokuwepo watatimiza majukumu yao vizuri. Msimu huu unaweza kuwa ni wa tofauti kwa Yanga hata kama tumeanza kwa kupoteza mechi ya ligi"

Walinzi wapya walioongezwa kwenye kikosi cha Yanga ni pamoja na Ally Ally, Ally Mtoni, Lamine Moro, Mustafa Suleyman na Muharami Issa 'Marcelo' - Yangafulldoz
 
Mikia yabidi mtushukuru kwani tumewapa ahueni ndani ya nafsi mana mlikuwa mnaelekea kupagawa.

Pia niwaambie ile ni ligi kuu jamani na bado kuna mechi kibao na ndio sababu hata Barca mechi ya kwanza ya ufunguzi wa la Liga alipoteza pia na wala haikuwa jambo la ajabu.

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
Asee kufungwa kwa Yanga na Ruvu hakupunguzi machungu ya Mbumbumbu/Mikia/Tundu/Gala/Kilomoni/Bi Hindu/Timu Muswati FC kutolewa kwenye mashindano ya kimataifa. Vimebahatisha Mara moja msimu ulopita vinapiga keleleeeee!. Hebu vituache sisi Wa kimataifa bwana.
 
Asee kufungwa kwa Yanga na Ruvu hakupunguzi machungu ya Mbumbumbu/Mikia/Tundu/Gala/Kilomoni/Bi Hindu/Timu Muswati FC kutolewa kwenye mashindano ya kimataifa. Vimebahatisha Mara moja msimu ulopita vinapiga keleleeeee!. Hebu vituache sisi Wa kimataifa bwana.
๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ Waambie Mkuu walijua kila siku ni Jumatatu.

Ile slogan yao ya iga ufe ikawahukumu Uwanja wa Taifa. Yaani Yanga alisuluhu na Township Rollers eti na wao wakasuluhu Taifa na Du Songo. ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ Hatimaye wakafa wao
 
Wanacheza na timu ya wananchi Septemba 14. Hivyo siku mbili au tatu nyuma watakuwa washatia timu.

Kulikoni Mkuu unataka ununue jezi yao? ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ
ninayo tayari nataka kwenda kuwapokea airport
 
Tena nakununulia kabisa na tracksuit kofia, viatu, soksi na hata "naniliu" ile ambayo haionekanagi vyote hivyo vikiwa na rangi ya timu yako unayoipenda sana Shadeeya

Ila najua siku mkitufunga hautanizodoa sanaa eeh mamii
Uuwiiii!!!! Nawaza tu mfanano wake utakuwaje hapo. ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Tena mlivyo na tambo siku ya kuwafunga sijui kama ntaweza kujizuwia kukuzodoa. ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ ๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ
 
Uuwiiii!!!! Nawaza tu mfanano wake utakuwaje hapo. ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Tena mlivyo na tambo siku ya kuwafunga sijui kama ntaweza kujizuwia kukuzodoa. ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ ๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ
KWa bahati nzuri huo msamiati wa kutufunga haupo kabisa msimu huu ujue? Jipangeni labda miaka ijayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom