Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atatumia mechi zilizobaki kujiimarisha kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael.

Nchimbi maarufu kama 'Duma', amesema amefuata ipasavyo program ya mazoezi aliyoachiwa na kocha hivyo yuko tayari kuuwasha moto pale ligi itakaporejea
Akiwa mmoja wa nyota wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga, Nchimbi amesema pamoja na wachezaji wengine, watahakikisha wanamaliza msimu kwa kishindo

"Binafsi nimekuwa nikifanya mazoezi kujiweka sawa, nimefuata program ya Mwalimu hivyo nimefurahi ligi kurejea na niko tayari kwa asilimia 100," alisema
Nchimbi ni mmoja wa wachezaji ambao wamejihakikishia namba kwenye kikosi cha Eymael akiwa na uhakika wa kuendelea kukipiga na mabingwa hao wa kihistoria licha ya ujio wa nyota kibao wanaotarajiwa kusajiliwa dirisha la usajili litakapofunguliwa.

@Yangafulldozz.
Daaa nampenda sana Nchimbi na nadhani ndiye mchezaji anayeweza kutoa 100% ya work rate kwenye timu yetu. Anajituma sana na hakati tamaa,namtabiria mema huko mbele
 
Daaa nampenda sana Nchimbi na nadhani ndiye mchezaji anayeweza kutoa 100% ya work rate kwenye timu yetu. Anajituma sana na hakati tamaa,namtabiria mema huko mbele
Yah!! Na kama mechi zile mbili za watani wa jadi alikuwa mwiba kwani beki za simba zilipata sana tabu.

Na kama sio janja janja ile mechi ya raundi ya kwanza yule mama alimnyima penalti ya wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom