Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20190920_100921.jpg
Kama ilivyokuwa Botswana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela anatarajiwa kuongoza msafara wa maafisa wa timu hiyo nchini Zambia kuweka mambo sawa kabla ya kikosi kuwasili mwanzoni mwa wiki ijayo

Yanga inatarajiwa kwenda Zambia Septemba 23 kuweka kambi ya siku tano kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco ambao utapigwa Septemba 28

Mwakalebela ndiye aliyeongoza msafara wa Yanga Botswana, akihakikisha timu inakuwa na mazingira mazuri ya maandalizi wakati wote waliokuwa nchini humo

Kwa sasa Yanga inaendelea kujifua jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo ambao matokeo ya ushindi yatawapa nafasi ya kutinga hatua ya makundi.

Yangadaima27
 
NYOTA WA ZAMANI YANGA KUONGEZA NGUVU .
.
.
Nyota waliowahi kutamba na kikosi cha Yanga miaka ya nyuma wanatarajiwa kukutana na wachezaji wa timu hiyo kuwapa hamasa kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United

Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam mwanzoni mwa wiki ijayo kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Septemba 28 uwaja wa Levy Mwanawasa, Ndola, Zambia

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa Sam Mwaitenda alisema wachezaji hao watawaongezea morali ya kufanya vizuri huko Zambia

Yanga pia imetoa fursa kwa mashabiki wake kuongozana na timu nchini Zambia kuhakikisha kikosi kinapata sapoti ya kutosha siku ya mchezo

Katibu wa kamati ya Hamasa Deo Mutta alisema safari ya mashabiki hao kuelekea Ndola itakuwa na sura tofauti kwa makundi ambayo yataanzia ya yale ya Nyanda za juu Kusini Iringa, Songwe, Njombe na Mbeya ambao safari yao itanzia Tunduma kuelekea Ndola huku gharama ikiwa Sh 110,000 kwa kwenda na kurudi.

Mutta alisema kwa mikoa mingine ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani gharama za safari itakuwa ni Sh 200000 kwa kila kitu kasoro chakula na malazi.

Alisema kwa wanachama wenye hati ya kusafiria,hati ya chanjo gharama yao itakuwa ni Sh 150,000 ambapo wote watakaohitaji kwenda wanatakiwa kukamilisha malipo kabla ya Septemba 22,2019 huku safari ilitarajiwa kuanza Septemba 25.
 
Sijaongeza chumvi hata kidogo unastahili kila sifa niliyoitamka love.....ila pia gauni la red kama la hiyo emoj sina hata la kuongeza..ka.a dera lileee🤗
😍😍 🙏🙏🙏 Haya jiandae wiki ijayo twende Zambia tukawaone wa Kimataifa. Mi nishaanza kufanya mipango huku Songea love.
 
NYOTA WA ZAMANI YANGA KUONGEZA NGUVU .
.
.
Nyota waliowahi kutamba na kikosi cha Yanga miaka ya nyuma wanatarajiwa kukutana na wachezaji wa timu hiyo kuwapa hamasa kuelekea mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United

Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam mwanzoni mwa wiki ijayo kuelekea Zambia kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Septemba 28 uwaja wa Levy Mwanawasa, Ndola, Zambia

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa Sam Mwaitenda alisema wachezaji hao watawaongezea morali ya kufanya vizuri huko Zambia

Yanga pia imetoa fursa kwa mashabiki wake kuongozana na timu nchini Zambia kuhakikisha kikosi kinapata sapoti ya kutosha siku ya mchezo

Katibu wa kamati ya Hamasa Deo Mutta alisema safari ya mashabiki hao kuelekea Ndola itakuwa na sura tofauti kwa makundi ambayo yataanzia ya yale ya Nyanda za juu Kusini Iringa, Songwe, Njombe na Mbeya ambao safari yao itanzia Tunduma kuelekea Ndola huku gharama ikiwa Sh 110,000 kwa kwenda na kurudi.

Mutta alisema kwa mikoa mingine ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani gharama za safari itakuwa ni Sh 200000 kwa kila kitu kasoro chakula na malazi.

Alisema kwa wanachama wenye hati ya kusafiria,hati ya chanjo gharama yao itakuwa ni Sh 150,000 ambapo wote watakaohitaji kwenda wanatakiwa kukamilisha malipo kabla ya Septemba 22,2019 huku safari ilitarajiwa kuanza Septemba 25.
Ng'ombe hanenepei mnadani Shadeeya hayo mawaidha na mafunzo wangewapa sikunyingi kabda saivi jua limekuchwa bna Zesco washawasoma

Safari hiyo sasa mnatakiwa mkaongeze nguvu kupunguza magoli kama utalipa nauli au utaweka wese unyanyuke ili mradi mkawafariji vijana wenu wanaokwenda kuaibika
 
Mwaka huu ndio atakaponenepa sasa.

Usisahau kwamba sisi sio wale wa kupigwa khamsa khamsa ugenini ujue.:cool::cool:
 
Ushawasikia wenyewe lakini? Wanakwambia toka Chama lao Zesco lianzishwe halijawahi kupoteza mechi nyumbani, kwa hiyo mjipange tu maana hapo ni mwendo wa kupunguza idadi ya magoli ya kufungwa
 
Maneno tu haya kipenzi na hii ndio imefanya hata na nyie mkajisahau yakawakuta ya kuwakuta kwa kudhania eti Taifa ni kaburini kwa kila ajaye.
 
Nawatakia kila la heri mpenzi ila ni timu moja tu katika historia iliyowahi kufanya maajabu na kupindua meza kibabe ndani ya Zambia na mbele ya Rais wao na Wazambia wanaijua na ipo kwenye rekodi za CAF
Hata na sie tukiyafanya hayo septemba 28 , nayo mwisho wa siku yatakuwa Historia pia love. 😎😎

Amiin Insha Allah. 🙏🙏
 
Back
Top Bottom