Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Ticha wenu mumshauri shishimbi hana akili ya kucheza namba 10 hana killing pass msilaum strikers...ajifunze pia kwa Lwandamila...mchezaji akiingua kwenye match mtoe...Banka leo aliflop...
 
Du,labda Yanga ije itafte wafungaji wazuri..maana striking hamna kabisa..magoli n ya kusuasua tu.
 
Wakati mashabiki wa Simba wakiendelea kusherehekea sare ya bao 1-1 waliyopata Yanga dhidi ya Zesco United juzi, mabingwa hao wa kihistoria bado wataendelea kuwatesa watani zao hata ikitokea wameondoshwa michuano ya ligi ya mabingwa

Mashabiki wa Simba wanaiombea Yanga 'dua baya' ili iondoshwe kwenye michuano ya Kimataifa baada ya timu yao kushindwa kupenya hatua ya awali wakitolewa na UD Songo

Baada ya kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, Yanga walijihakikishia tiketi mbili

Ya kwanza ni kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo kama watapata matokeo ya ushindi Zambia

Lakini ya pili, kama wakitolewa na Zesco, watahamia kwenye michuano ya kombe la shirikisho

Utaratibu wa CAF uko hivi;

Timu 16 ambazo zitashinda raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa, zitatinga hatua ya makundi

Nyingine 16 ambazo zitatolewa raundi hiyo, zitaungana na tmu 16 zilizofuzu raundi ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho

Zitacheza raundi moja ya kusaka timu za kutinga makundi kombe la Shirikisho

Msimu wa 2015/16 Yanga walitolewa na Zanaco raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa, wakapangwa na Sagrada Esperanca ya Angola hatua ya mtoano wa kufuzu makundi kombe la Shirikisho na wakatinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1

Wakarudia tena msimu wa 2017/18 kwa kutinga makundi kombe la Shirikisho kwa kuindosha Wolayta Dicha ya Ethiopia kwa kuifunga mabao 2-1 baada ya kutolewa na Township Rollers kwenye ligi ya mabingwa

Hivyo hata kama watakosa nafasi ya kutinga makundi ligi ya mabingwa, wataendelea kubaki anga za Kimataifa wakisaka nafasi nyingine ya kutinga makundi kombe la Shirikisho
 
20190917_092228.jpg
Benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Mwinyi Zahera wameweka bayana kuwa mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United, utakuwa wa kufa au kupona

Mchezo huo utakaopigwa Septemba 28, utaamua timu itakayotinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa

Kama ilivyokuwa mchezo dhdi ya Township Rollers, wachezaji wa Yanga wameahidiwa mamilioni kama watatinga makundi

Ushindi wa ugenini dhidi ya Township Rollers, uliwaingizia Tsh Milioni 50 ambazo zilitolewa na uongozi kama shukrani kwao

Inaelezwa sasa kama watatinga makundi kwa kuiondoa Zesco United, watapokea kitita cha Tsh Milioni 150

Fedha hizo watagawana wachezaji wote kulingana na mchango wao kwenye mchezo huo

Hii ni nafasi nyingine kwa wachezaji kujiingizia mamilioni achilia mbali bonus kibao watakazopata kama timu itatinga makundi

Kama itafanikiwa kutinga hatua hiyo, Yanga itaingiza zaidi ya Tsh Bilioni moja

#Yangafulldozz
 
20190918_055152.jpg
Kiungo wa Yanga, Abdul Aziz Makame 'Bui' amesema nidhamu, kujituma na kujifunza kila wakati kutoka kwa kocha na wachezaji wenzake ndio siri inayomfanya acheze kwa kujiamini anapopewa nafasi.

Makame alionyesha kiwango cha juu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Yanga dhidi ya Zesco ya Zambia, akitawala vizuri eneo la safu ya kiungo.

Makame alisema msimu huu anataka kuonyesha kipaji chake ili kutimiza ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa katika siku za usoni.

Kutokana na uwezo wake ameiitwa katika kikosi cha Taifa Stars tangu Etienne Ndayiragije alipochukua jukumu hilo. "Soka ni kazi ninayotamani ibadilishe maisha yangu, lazima nifanye bidii ili kazi yangu iwe na thamani ya kukifikia kile ninachokifikiria kwenye maisha yangu" "Yanga ni klabu kubwa ina wachezaji wenye uzoefu lazima nijifunze vingi kupitia kwao na kile ambacho kocha Mwinyi Zahera anataka nikifanye" "Naamini hata kuitwa kwenye timu ya Taifa inatokana na kile ambacho nimekionyesha kwenye klabu yangu ya Yanga, natamani uwe msimu wenye mafanikio makubwa kwangu" alisema Makame.
 
20190918_055404.jpg

Mwinyi Zahera: Yanga itafika makundi hata kama hampendi, aahidi kuwaonyesha wanaobeza kikosi chake
. . . .

Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amekusudia kuwaziba midomo wanaobeza kikosi chake huku akidai kuwa watawatoa Zesco United, kwenye mchezo wa marudiano wa Klabu bingwa barani Afrika utakachezwa katika jiji la Ndola nchini Zambia.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wakicheza nyumbani vijana wa Zahera walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 huku Zesco United FC wakichomoa dakika ya 94 kupitia kwa kiungo wao Thaban Kamusoko.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Spoti Leo online, Kocha huyo raia wa Congo amesema anatambua kwamba watu wengi hawaipi Yanga nafasi ya kutinga hatua ya makundi kutokana na sare hiyo lakini yeye ni kocha mwenye mbinu nyingi zinazomwezesha kupata matokeo na amepania kuwashangaza watu kwa kufanya hivyo Zambia. . . . . “Nataka kuwaonyesha watu hasa wale wanaoidharau Yanga, kwamba tutacheza makundi ya Ligi ya mabingwa kwa kuwatumia wachezaji hawa hawa waliocheza mechi ya kwanza nitaongezea na mbinu zangu mbadala ambazo hatukuzitumia mchezo uliopita nina uhakika tutavuka na midomo wataifunga,” alisema Zahera.

Kocha huyo amesema Zesco siyo timu yakutisha kihivyo kama ambavyo watu wanaizungumzia ndiyo maana baada ya kuwaona na kubaini mbinu wanazotumia amepata uhakika wa kujua cha kufanya na kupata matokeo wakiwa ugenini.

Yanga ili kusonga mbele hatua ya makundi inalazimika kupata sare ya kuanzia mabao 2-2 au ushindi wowote, jambo ambalo litawalazimu kucheza kwa umakini mkubwa sababu Zesco nao wamepania kuendeleza rekodi yao ya kucheza makundi kama wanavyofanya huko nyuma.
 

Similar Discussions

97 Reactions
Reply
Back
Top Bottom