Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amekusudia kuwaziba midomo wanaobeza kikosi chake huku akidai kuwa watawatoa Zesco United, kwenye mchezo wa marudiano wa Klabu bingwa barani Afrika utakachezwa katika jiji la Ndola nchini Zambia.
Shadeeya itafika mahali mtaona huyo kocha anazingua na nyie wenyewe mtaanza kumshikia bakora na kumuonyesha mlango wa kutokea. Nitarudi tena siku zijazo kukukumbusha hili panapo majaaliwa ikiwa utakua umesahau
 
Ses hiyo ndio sifa ya kuajiriwa kama Kocha hakuna anayeondoka kwa raha na hii ndio itakavyokuwa kwa Ausem na hata Zahera pia.
 
Mwinyi Zahera: Yanga itafika makundi hata kama hampendi, aahidi kuwaonyesha wanaobeza kikosi chake
. . . .

Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amekusudia kuwaziba midomo wanaobeza kikosi chake huku akidai kuwa watawatoa Zesco United, kwenye mchezo wa marudiano wa Klabu bingwa barani Afrika utakachezwa katika jiji la Ndola nchini Zambia.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wakicheza nyumbani vijana wa Zahera walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 huku Zesco United FC wakichomoa dakika ya 94 kupitia kwa kiungo wao Thaban Kamusoko.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Spoti Leo online, Kocha huyo raia wa Congo amesema anatambua kwamba watu wengi hawaipi Yanga nafasi ya kutinga hatua ya makundi kutokana na sare hiyo lakini yeye ni kocha mwenye mbinu nyingi zinazomwezesha kupata matokeo na amepania kuwashangaza watu kwa kufanya hivyo Zambia. . . . . “Nataka kuwaonyesha watu hasa wale wanaoidharau Yanga, kwamba tutacheza makundi ya Ligi ya mabingwa kwa kuwatumia wachezaji hawa hawa waliocheza mechi ya kwanza nitaongezea na mbinu zangu mbadala ambazo hatukuzitumia mchezo uliopita nina uhakika tutavuka na midomo wataifunga,” alisema Zahera.

Kocha huyo amesema Zesco siyo timu yakutisha kihivyo kama ambavyo watu wanaizungumzia ndiyo maana baada ya kuwaona na kubaini mbinu wanazotumia amepata uhakika wa kujua cha kufanya na kupata matokeo wakiwa ugenini.

Yanga ili kusonga mbele hatua ya makundi inalazimika kupata sare ya kuanzia mabao 2-2 au ushindi wowote, jambo ambalo litawalazimu kucheza kwa umakini mkubwa sababu Zesco nao wamepania kuendeleza rekodi yao ya kucheza makundi kama wanavyofanya huko nyuma.
Boo
 
20190920_060549.jpg
Kocha Mkuu wa Zesco United George Lwandamina amekiri kuwa kiungo mkabaji wa Yanga abdul_aziz makame_ 'Bui' ndiye aliyewavuruga mipango yao jijini Dar es salaam akishukuru kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Katika mchezo huo, Makame alicheza sehemu ya kiungo pamoja na 'nduguze' kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum 'Fei Toto' na Mohammed Issa 'Banka'

Mkufunzi huyo wa zamani wa Yanga amesema alivutiwa na aina ya uchezaji wa Bui mara kwa mara akihusika kukata mawasiliano baina safu ya kiungo na washambuliaji wa Zesco

Kiwango alichoonyesha Bui kwenye mchezo huo, kimemuweka kwenye nafasi nzuri ya kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza

Kocha Mwinyi Zahera alisema Makame alitimiza vyema majukumu aliyompa katika mchezo huo

Makame ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Sudan kusaka tiketi ya kutinga fainali za CHAN

Wachezaji wengine wa Yanga walioitwa ni pamoja na mlinda lango Metacha Mnata, Kelvin Yondani, Mohammed Issa na Feisal Salum

Yangadaima27
 
Hahahaha, Mtani niko Kitwe Zambia ,naona km upepo uko vzr kwako
 
Uwiii!!! Umefanya nimetabasamu jirani mana saa ka hizi kauli za kudumaza huwa hatutaki kuzisikia 😀😀

Na mimi naamini tutawashangaza wengi Mtani.
Kumekucha Shadeeya uamke basi mamii, natumaini haya usemayo ndio uhalisia na wala sio ndoto, maana kuna ndoto zingine zinakua tamu sana kiasi kwamba unalaumu kwanini umeamshwa usingizini🤣😂😂
 
20190920_100630.jpg
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema katika kikosi chake anataka wachezaji wawe na uzito sahihi ili kuweza kutimiza majukumu yao vyema

Baada ya kufanya kazi ya kumpunguza uzito mshambuliaji David Molinga, zoezi hilo limehamia kwa Mganda Juma Balinya

Balinya hakucheza mechi dhidi ya Zesco United, Zahera amefichua kuwa Mganda huyo hakuwa tayari kwa mchezo "Balinya aliongezeka kilo nne, tulipokuwa Mwanza tulimpa program maalum ya kupunguza uzito, alipungua kilo mbili" "Kabla ya mechi ya marudiano na Zesco atakuwa sawa na pengine tutamtumia," amesema Zahera

Balinya ndiye aliyeipeleka Yanga raundi ya kwanza akiifunga bao la ushindi dhidi ya Township Rollers nchini Botswana

Balinya na Molinga sio wachezaji wa kwanza kutakiwa kupunguza uzito na kocha Zahera

Beki Juma Abdul nae aliwahi kukumbana na zoezi hilo

Yangadaima27
 
Back
Top Bottom