Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,787
- Thread starter
- #21
OMG sorry about that. Wakati mwingine ni vigumu kujua sababu za mmoja ku-walk away from a relationship and sometimes we may think that it is the end of every good moments in life, kumbe hapana life is too big. Unapoumizwa mara nyingi macho huingia ukungu kiasi kwamba huoni mbele na unafikiri kila mlango kwenye maisha yako umefungwa which is not kweli kwani Life is so sweet.
One thing that i believe in life is to be positive although is hard at the moment you are going thru a painful situation. Mkuu jitahidi kuupa moyo wako another chance , one day out there you might meet a good Samaritan who is gonna give a refuge for your heart and you will forget the past . Remember you are not the first/last person to go thru this , wengi walikutwa na yaliyokukuta lkn wali move on who knows lbd Mungu amekuandalia mtu mwema atakaethamini pendo lako. Jipe muda kwani time is a great healer.
Kuna vitu vingine katika maisha hutokea,ambavyo hatupendi vitokee, na once vitokeapo hutuachia majonzi sana na majereha yasiyosahaulika moyoni...
Ni msichana tuliyekutana naye wakati yeye akisubiri matokeo ya kidato cha sita,meanwhile nilikuwa dissappointed na Lilian Girlfriend wangu wa kwanza whom aliamua alibadilika kutokana na makundi almaaruf kampani, nikajaribu kumbadili sana ikiwa ni pamoja na mimi kujibadili ili walau tuendane but akili ya bi dada huyu huwa inachange often,nikaamua kukaa kimya na kuachia ngazi....
Tokea hapo nikawa muda mwingi ambao siko kazini naumalizia kwenye novel na wakati mwingine nikawa mhudhuriaji mzuri sana kwenye viti virefu ambako kwa kiwango kikubwa kuliniwezesha kusahau maswahibu yangu kwa Lily...Kisha ikaja hii siku ambayo siwezi kuisahau...
Alikuwa anaolewa Vai, binamu yangu,kwa kuwa ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka tukaona as family ni busara kutumia nafasi hiyo kukutana pamoja na kufahamiana kwa kuwa kutokana na pilika za kutafuta maisha tulikuwa scattered sana. Ni siku moja kabla ya send off nilipojiamulia kwenda kusabahi marafiki zangu waliokuwa wanaishi mji wa pili kwenye mkoa wangu...
Nikiwa stend ya mabasi najisomea kitabu cha Dale Carnegie ( how u can win friends and influence people) wakati huo huo nikiwa kwenye dala dala kwa mbali namwona binti mmoja matata sana ambaye kwa sala za papo kwa hapo nilikuwa naomba awe anaelekea safari moja na mimi,ukweli ukawa hivyo...
Akaingia kwenye gari nililokuwa nimepanda na kikubwa zaidi akaja kwenye seat nearby,alinisabahi huku akiachia tabasamu lililomeza umakini wangu kwa sec kadhaa kisha nikapunga mkono pasi kusema neno,punde safari ikaanza huku nikijititahidi kusoma kitabu changu of which niliacha baadaye baada ya kugundua kwamba mstari niliokuwa napitia baada ya kumwona mgeni huyu ndio huo huo nilikuwa narudia rudia though kuna kitambo kilishapita!
Mtoto wa kiume nikaamua kujilipua kwa kuanzisha mazungumzo ambayo hata hivyo sikuwa na uhakika sana kama ningepata ushirikiano kutoka upande wa pili,ila haikuwa hivyo,tuliongea mawili matatu concern maisha na kufahamiana japo kwa uchache. Ni hapo nilipogundua kwamba alikuwa amehitimu kidato cha sita na alikuwa anasubiri matokeo ili aweze kuendelea na elimu ya juu.
Kwa kuwa alikwisha nieleza kwamba safari yake ingeishia wapi na kwa kuwa mimi ningeishia midway nikaomba kama asingejali tubadilishane # of which hakusita akanipa no nami nikampa yangu! Tokea hapo ikawa ni mwanzo wa kuwasiliana na kutakiana moment njema njema...Kadiri muda ulivyoenda tukajikuta tumevuka urafiki na tayari tukaanzisha mahusiano rasmi...
Matokeo yalipotoka akachaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma huku mahusiano yetu yakipamba moto,vilikizo vidogo vidogo vyoote kipindi chote cha masomo nilivitunza,na wakati mwingine hata ikibidi nilikuwa nakoroga kazini kwa kuzingizia kifo cha mtu immaginary ama alokwisha kufariki miaka mingi ili niende Dom ama yeye aje town (Dar) Dada zangu wakajua,mama akajua na baba akabidi niwe wazi bila shuruti na kwa upande mmoja tukawa tume officialize....
Yapo mengi ila frankly tumepita moments zote nzuri nzuri ambazo kwa mbali zinaendana na hizi tamdhilia za kikorea and likely,hakuwahi kuninunia muda wote niliokaa naye,hatukuwahi kupishana lugha,hakuna hata mmoja kati yetu aliyewahi kumtendea mwenzie hiyana na kila siku kwetu ilikuwa nzuri kuzidi jana yake...Nilimpenda sana Rose,nampenda though ameshapata mwingine!
Ni juzi niliamua kusum up vitu vingi vingi na kujumlisha hapa na pale baada ya kuona kuna badiliko katika mahusiano yetu na kuhisi kuna mdudu keshaingia ambapo kwa upole nilijaribu kutaka kiini cha kunyauka huko kwa pendo letu,ndipo aliponiambia ukweli wake wa moyoni,ambao kwangu ni mchungu na umeniachia majeraha ambayo sina hakika kama yatapona...
Aidha natambua kuna mabinti wazuri sana na kwamba kila kukicha wanazidi kuchomoza wazuri kuliko wa jana ila hakuna kama Rose wangu,aliyepata kunipenda,nikampenda,daima nitaheshimu mawazo yake na nitamwombea kwa Mungu dua njema ili upendo alioupata kwangu aupate kama huo ama zaidi kwenye mahusiano yake mengine aliyoyaanzisha ambapo jana alitambulishwa rasmi ukweni kwao kwa maana kinachofuata huenda ni engagement labda na ndoa!