Yesu ni jibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yesu ni jibu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kibun'ga, Aug 26, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
1. K

Kibun'ga New Member

#1
Aug 26, 2011
Joined: Aug 26, 2011
Messages: 2
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Yule Sheikh Mtoto maarufu kama Sheikh Shariff ambaye aliitingisha Tanzania kwa ufahamu mkubwa wa Qur’an akiwa na umri wa miaka tisa hatimaye amesalimu amri na kuokoka, katika kanisa la Pentekoste Motomoto jijini Dar es Salaam .
Sheikh Shariff ambaye jina lake halisi ni Sheikh Shariff Mohamed Mikidadi tayari amebatizwa na kupewa jina jipya la Michael Sylivester Sewando, ambapo hivi sasa analelewa kiroho katika kanisa hilo lililopo Keko chang’ombe jijini Dar es Salaam .
….Licha ya Sheikh Shariff sasa Michael Sewando kuzaliwa katika familia ya kikatoliki ya mzee Sylivester Sewando na mama yake Joyce Mokiwa, alisema alisilimu baada ya kutibiwa maradhi yake na mganga muumini wa dini ya Kiislamu wakati akiwa mtoto.Katika umri mdogo, jambo hilo lilimfanya ghafla ajikute akianza kuipenda dini ya kiislamu na ndipo aliamua kujiunga nayo, ingawaje wazazi wake walimpinga vikali.Alisema ilibidi aondoke Nyumbani kwao Kawe Ukwamani na kuhamia kwa ndugu wa kiislamu na kuanza kuswali katika msikiti wa Al Shariff, International Dawas’ Islamic Centre Kawe Dar es Salaam. (SIDC) alikoingizwa rasmi katika dini ya Kiislamu.Alisema mara baada ya kujiunga na dini hiyo na kuanza kuswali katika msikiti huo, alijikuta akipata ufahamu mkubwa wa elimu ya Qu’ran pasipo kufundishwa. Sheikh Shariff alisema anachojua ni kwamba uwezo wa kuijua Qur’an aliupata kutoka kwa majini 2900, yaliyomuingia baada ya kujiunga na Uislamu.Alisema majini hayo ndiyo sababu pekee iliyomfanya awe mahiri sana katika elimu ya dini ya kiislamu. Akizungumza na wahadhiri mbalimbali nje na ndani ya Tanzania huku akifanya miujiza na kuendesha mihadhara mingi ya kiislam.Kwa mujibu wa Sheikh huyo aliyeokoka, maeneo aliyowahi kutoa mihadhara ni Kawe,Tandika , Mbagala, Njoro, Kilimanjaro, Mwembe tayari nchini Kenya , viwanja vya msikiti Mkuu wa Jijini na Kampala nchini Uganda .Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Sheikh Shariff alisema aliwahi kuishi chini ya bahari ya Hindi katika eneo la Maskati, nchini Oman , akifundishwa mambo mbalimbali na majini. Alisema akiwa chini ya bahari alikuwa akifundishwa na jini mkuu aliyemtaja kwa jina Lusifa ambalo ni la Shetani, ambapo alikuwa akilishwa mchanganyiko wa damu za binadamu na wanyama na mifupa ya farasi.Sheikh Shariff au Michael Sewando alisema Lusifa au mkuu wa majini ambaye alikuwa na umbo la mfano wa mjusi mkubwa, ndiye aliyemfundisha masuala ya uganga wa kienyeji kwa kutumia vitabu maarufu vya kijini. Mambo mengine aliyofanyiwa akiwa chini ya bahari ni pamoja na kuwekwa katika moto mkali kwa muda wa siku saba na baadaye katika baridi kali na giza totoro kwa siku hizo hizo.Nakumbuka nikiwa chini ya bahari ambako naamini ni kuzimu, Lusifa aliamuru kuwa kamwe nisilitaje jina la mtu aliyesulubiwa msalabani kwa maana yaYesu, kwa vile jina hilo ni baya na huharibu kazi za kuzimu. Pamoja na mambo mengine mengi ya ajabu aliyofanyiwa au kufundishwa na Lusifa, alisema baadaye alihitimu na kupatiwa mikoba mitatu iliyosheheni madawa ya mitishamba, viungo vya wanyama, binadamu na majoka. Unajua nilikuwa nafanya masuala ya kuagua watu kiganga huku pia nikiendesha mihadhara mbalimbali ya kiislamu’’ alisema akionyesha kitambulisho kinachoonyesha kuwa ni mganga wa kienyeji.Alisema katika shughuli zake aliwahi kuwasilimisha wakristo mbalimbali wakiwepo mapadri na wachungaji, ambapo ameahidi kuwarudisha kwa Yesu baada ya kuokoka. Aidha alibainisha kuwa aliwahi kuoa majini mawili na kusababisha ajali zilizopoteza maisha ya watu ili kupata damu na nyama za majini aliyokuwa akiyamiliki.Kuhusu jinsi alivyokutana na Yesu na kuokoka, alisema hivi karibuni wakati akielekea katika shughuli zake za uganga eneo la Mbagala Mgeni Nani, miguu yake ghafla ilinasa ardhini na akasikia sauti ya Yesu ikimwambia kwamba aachane na uchafu wake, ili atakaswe kwa damu yake Yesu lakini alitaka kupinga.Alisema akiwa katika hali ya kupinga sauti hiyo, alitokea mama mmoja aliyekuwa muislam lakini akaokoka, ambaye alimshauri aokoke na kumuongoza zaidi hadi katika kanisa la Pentekoste Motomoto lililoko Keko Chang’ombe alikomkiri Yesu na kuokoka baada ya kutolewa mapepo. Kanisa la Pentekoste Motomoto linaongozwa na Mchungaji Ibrahimu John ambaye kwa sasa ndiye baba wa kiroho wa Sheikh Shariff.Sheikh Shariff (Michael Sewando) alisema baada ya kuokoka, amekuwa akipata mashambulizi kutoka kwa majini na wachawi hivyo anaomba msaada wa maombi kutoka kwa wacha Mungu wote.SOURCE: MSEMA KWELI

2. Bujibuji

Bujibuji JF-Expert Member

#2
Aug 26, 2011
Joined: Feb 4, 2009
Messages: 35,381
Likes Received: 22,254
Trophy Points: 280
Yesu oyeeeeeeeeeeeeeeeee
Mwamedi kushney

3. Rejao

Rejao JF-Expert Member

#3
Aug 26, 2011
Joined: May 4, 2010
Messages: 9,239
Likes Received: 245
Trophy Points: 160
Full Udaku..
ngoja nipite tu

4. Bujibuji

Bujibuji JF-Expert Member

#4
Aug 26, 2011
Joined: Feb 4, 2009
Messages: 35,381
Likes Received: 22,254
Trophy Points: 280

Napo umesoma

5. eddo

eddo JF-Expert Member

#5
Aug 26, 2011
Joined: Mar 16, 2010
Messages: 291
Likes Received: 3
Trophy Points: 35
wel come back,...maaake huko ulikokua ni mmmmmmh

6. EBENEZA MT

EBENEZA MT JF-Expert Member

#6
Aug 26, 2011
Joined: Jul 4, 2011
Messages: 264
Likes Received: 3
Trophy Points: 0

kubali usikubali habari ndiyo hiyo.

7. Katavi

Katavi Platinum Member

#7
Aug 26, 2011
Joined: Aug 31, 2009
Messages: 39,475
Likes Received: 4,134
Trophy Points: 280
Safari njema...

8. Rejao

Rejao JF-Expert Member

#8
Aug 26, 2011
Joined: May 4, 2010
Messages: 9,239
Likes Received: 245
Trophy Points: 160
"Yesu alikuwa na mapungufu mengi"
Regia Mtema (Mb)- CHADEMA-25/8/2011

9. LiverpoolFC

LiverpoolFC JF-Expert Member

#9
Aug 26, 2011
Joined: Apr 12, 2011
Messages: 11,001
Likes Received: 153
Trophy Points: 160
Hillola kujaga kuokoka 2likuwa tunalisubiria tu kwa hakika Wakirsto wengi walikuwa wakimwombea sana huyu dogo kwa jinsi alivyo kuwa anawapotosha watu wa MUNGU na hakika neno hili litabakia kuwa ya kweli: KWA BWANA YESU KILA GOTI LITAPIGWA na bado wengi wataokoka tu.

10. Ringo Edmund

Ringo Edmund JF-Expert Member

#10
Aug 26, 2011
Joined: May 10, 2010
Messages: 4,895
Likes Received: 28
Trophy Points: 0
sheikh sharif,babu wa loliondo,kondoo wa quran,josee chamilion nk
bado tutaona mengi tu.
my take.hizi ni siku za mwisho.

11. Viper

Viper JF-Expert Member

#11
Aug 26, 2011
Joined: Dec 21, 2007
Messages: 3,665
Likes Received: 44
Trophy Points: 145
Sijabadili dini

sorce tanzania DAIMA!!! http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=9159

SASA TUAMINI GAZETI GANI MSEMA KWELI AU TANZANIA DAIMA...????!

may take Mods hii thread haina tofauti na ule uzsshi wa shimbo! ificheni mpaka mpate uhakika! ili kijana wa watu aije akapata usumbufu usiokuwa wa lazima

12. Washawasha

Washawasha JF-Expert Member

#12
Aug 26, 2011
Joined: Aug 7, 2006
Messages: 8,701
Likes Received: 425
Trophy Points: 180
Dah! usanii mtupu,kweli Dunia ina mambo fix kwenye siasa ,dini ma mengine mengi kumbe kifaa kilioa majini! hahahah ujue leo nimecheka mpaka basi,huyu ni msanii tu hana jipya naona kaamua atoke na style ya kuokoka inawezekana waislamu walishamshtukia kuwa ni fix

13. U

Ulimakafu JF-Expert Member

#13
Aug 26, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 18,015
Likes Received: 743
Trophy Points: 280
Kweli kabisa.

14. Kiby

Kiby JF-Expert Member

#14
Aug 26, 2011
Joined: Nov 16, 2009
Messages: 5,209
Likes Received: 1,012
Trophy Points: 280

Keshananga kwenye mikono salama ya Yesu, hivyo usumbufu kutoka kwa lewiathan aliyemkimbia ni lazima.
Lakini shetani huyo wa chini ya bahari amekwisha kushindwa vibaya kwa JINA la YESU.

15. Viper

Viper JF-Expert Member

#15
Aug 26, 2011
Joined: Dec 21, 2007
Messages: 3,665
Likes Received: 44
Trophy Points: 145
Tuache ushabiki na tutumie akili , My point ni kwamba kwa nini TANZANIA DAIMA limeletaleta habari nyingine..kukanusha hizi habari.? according to them muandishi hadi akaongea naye shekh sharif akakanusha hizo habari .

je gazeti la msema kweli limesema habari ya uongo.

je TANZANIA DAIMA .. lemeandika habari za uongo..

je shehe sharif nayeye ni kigeugeu kama yule msanii wa uganda "kinyonga" alipoona umaarufu umeshuka ..

ndio maana nikasema habari hii si ya uhakika inaweza ikachafua jina la mtu na kumsababishia usumbufu

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=9159

Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...