Yesu Kristo kwa kifo chake alimrejeshea binadamu hali ya Kimungu, yaani akili

Kifo cha Yesu pale msalabani lengo ni kutoa kafara ili Damu na maji vikitoka ndio Mungu ajipatanishe na wanadamu ili kila mwanadamu aweze kuwapata ondoleo la dhambi kupitia maji na damu ya Yesu vilivyomwagika pale msalabani, 1Petro 1:18-20,wakolintho 1:20,Efeso 1:7,
Dhambi ni nini ?
 
Umehusisha kifo cha Yesu na kupata maarifa ya ki Materials kitu ambacho Biblia haijawahi sema na Yesu hajawahi sema hivyo!
Yesu Mwenyewe alisema, Yeye ni mwanga.

Unafafanuaje hilo ?

Biblia mara zote inamsema Yesu ni maarifa. Yesu haiwezekani kumtenganisha na material au dunia.

Pasipo Yeye hakuna material wala chochote.
 
Dunia hata kabla ya Ujio wa Yesu ilikuwa na maendeleo kulikuwa na serikali,jeshi,magari ya farasi,vyombo vya usafiri majini ,barabara majumba makubwa kama Hekalu la suleimani,minara ya Babeli,ma piramidi ya misri nk hayo yoote yalihitaji maarifa kwa wakati ule
Unafahamu kama historia au taarifa kabla ya Yesu Kristo haifahamiki waziwazi hivi kwamba inategemea maarifa baada ya Kristo kuyatafiti ?
 
Adamu na Hawa ni wazazi wetu wa mwanzo, mababu zetu.

Majina Adamu na Hawa yanarejelea wazazi wetu wa mwanzo, mababu zetu.

Ni nani asiye na mababu ambao kwao naye alizaliwa ?

Watangulizi wako upande wa ukoo wa baba na wa mama yako, mnyororo wa ukoo ndiyo Adamu na Hawa.

Je, ni binadamu au mtu gani asiye na watangulizi wake ? Au je, babu na bibi yako hawakuwepo ?

Kua na mababu hiyo inathibitishaje kua adam na hawa walikuwepo?

It's Scars
 
Pasipo Yesu hakuna chochote kilichofanyika. Kwa Kifo chake kile kilichoharibu hali ya kimungu ya mtu yaani akili kiliondolewa.

Akili ya binadamu ili iwezekuwa na nguvu au hali ya kimungu ni pekee katika na kwa njia ya Yesu Kristo, Kifo chake.
Hujajibu swali langu. Pia unaposema pasipo yesu hakuna kilichofanyika kama kipi iko hakikufanyika toa mifano. Swali langu la mwisho kulikuwa na ulazima upi yeye kufa ili hiyo akili ikombolewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia unaposema pasipo yesu hakuna kilichofanyika kama kipi iko hakikufanyika toa mifano.
Mfano ni huu: unafahamu mtu ni tofauti na wanyama ? Unalijua hilo?

Kama ndivyo .

Je, ni nini kinamfanya mtu awe tofauti na wanyama ?
 
Unafahamu kama historia au taarifa kabla ya Yesu Kristo haifahamiki waziwazi hivi kwamba inategemea maarifa baada ya Kristo kuyatafiti ?
Mkubwa sisi kama wakristo hatuamini kwenye Historia nje ya biblia katika kusimamia imani Yetu,tunaamini yaliyoandikwa na sio wanahistoria kabla ya Yesu na baada ya Yesu,kabla yesu hajaja duniani tangu kuumbwa kwa adamu hadi anakuja kulipita vizazi takribani 42 na walikuwa na maendeleo,maarifa na ujuzi kwa nyakati zao,lile andiko linalosema Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa,maarifa yaliyosemwa hapo sio maarifa ya kijamii(elimu dunia) bali ni maarifa ya imani ,kujua maandiko na kuyatafasiri maana yake ili mtu asikudanganye na ndiomaana imeandikwa "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Sio wanaangamia kwa kukosa elimu za Degree,Masters na pHD hayo ni maarifa ya kibinadamu,Maarifa yaliyozungumziwa hapo ni maarifa ya Kimungu (Maandiko) ukijua maandiko yanasemaje huwezi angamia sababu utaijua kweli na kweli itakuweka huru!
 
Yesu Mwenyewe alisema, Yeye ni mwanga.

Unafafanuaje hilo ?

Biblia mara zote inamsema Yesu ni maarifa. Yesu haiwezekani kumtenganisha na material au dunia.

Pasipo Yeye hakuna material wala chochote.
Du! wewe unasoma biblia ya aina gani imesema Yesu Mwanga,maarifa nk weka hayo maandiko unayosema yesu alisema labda nianzie hapo kabla sijakujibu
 
Mfano ni huu: unafahamu mtu ni tofauti na wanyama ? Unalijua hilo?

Kama ndivyo .

Je, ni nini kinamfanya mtu awe tofauti na wanyama ?
Naona umeniuliza swali ila hujajibu maswali yangu, hii inaonesha hujui unachokizungumza. Jaribu kusoma mambo yatakayokusaidia katika maisha yako ya kila siku hizo hadithi za kwenye biblia naona zinakuchanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kosa la Adam na Hawa, mtu aliondelewa uwezo wa akili, hali ya kimungu.

Mtu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Ndiyo kusema mtu ni mwili na roho aliyeumbwa kushiriki uumbaji wa muumba wake, Mungu.

Roho au wakati mwingine huitwa akili pia moyo ndiyo maarifa yote.

Pasipo akili au roho, mtu anakuwa sawa na mnyama au mimea, hakuna maendeleo yoyote.

Kwa kosa la Adam na Hawa, wazazi wetu wa kwanza lilijeruhi roho au akili.

Kwasababu hiyo uwezo wa mtu kutenda kiakili yaani kimungu uliondoka akawa sawa na wanyama.

Binadamu kwa muda mrefu sana ameishi kama mnyama. Hakuwa na maarifa yoyote.

Kwa karne na karne mtu aliishi kwa kutumia akili ya ufahamu. Hakuweza kuendeleza mazingira.

Kwa ujio wa Yesu Kristo, kwa Kifo chake alimrejeshea binadamu hali ya sura na mfano wa Mungu yaani akili.

Yesu Kristo ndiyo chanzo cha maarifa yote. Ndiyo kwa njia yake binadamu anaweza kupata maarifa.

Maarifa tuliyonayo hii leo, maendeleo tulionayo hii leo ni kwasababu na kwa njia ya Yesu Kristo, Kifo chake.

Kabla ya Yesu Kristo mambo hayakuwa hivi yalivyo hii leo. Hakukuwa na maarifa pia maendeeleo kama haya baada ya Kristo.

Historia kabla ya Kristo haifahamiki kama ilivyo baada ya Kristo.

Hali ya mambo kabla ya Kristo ni ya kukanganya hivi kwamba inategemea maarifa baada ya Kristo kuitafiti.

Binadamu kabla ya Kristo, hata licha ya Mungu Mwenyewe kuwasaidia na wao wenyewe kumwomba Mungu kwa ajili ya ujio wa Kristo, bado hatahivyo, hali yao ya akili haikuwa imerejeshewa hadhi ile ya mwanzo ya kimungu tuliokuwa nayo kabla ya kosa la Adamu na Hawa.

Kwa ujio wa Kristo, kwa Kifo chake, tumerejeshewa hali ya kimungu yaani akili.

Pasipo Yesu Kristo, Kifo chake, mtu asingeweza kuwa na maarifa haya tuliyonayo nyakati hizi, maendeleo. Angebaki kama walivyo wanyama.

Hivyo, mtu anaekataa yale Yesu Kristo aliamuru kwa njia ya Kanisa lake yaani mitume hawezi kupata manufaa ya akili.

Kama lilivyo jua chanzo kikuu cha nishati duniani. Yesu Kristo ndiye chanzo cha maarifa na maarifa yenyewe. Yeye ndiye mwanga. Pasipo Yeye hakuna maarifa, wala maendeleo.
Ndugu umeandika habari za Yesu hata andiko la kwenye biblia moja kussuport ulichoandika hakuna.Hii inakuwa ni stori tu,mambo ya Mungu tunapoandika tunakuwa na mistari ya biblia kussuport tunachokiandika siyo maneno matupu kama ulivyofanya.Kajipange tena ukiwa tayari uje hapa JF ila vijiweni huko unaweza wapelekea hizo story.
 
Ndugu umeandika habari za Yesu hata andiko la kwenye biblia moja kussuport ulichoandika hakuna.Hii inakuwa ni stori tu,mambo ya Mungu tunapoandika tunakuwa na mistari ya biblia kussuport tunachokiandika siyo maneno matupu kama ulivyofanya.Kajipange
Kufanya rejea ili ku-support ulichoandika ni kwa aina mbali mbali.

Hivyo, nilichokiandika kinasapotiwa na biblia. Biblia ndiyo ina-support nilichokiandika.

Kwa hiyo hoja yako ni hafifu haina maana katika mada hii.
 
Kufanya rejea ili ku-support ulichoandika ni kwa aina mbali mbali.

Hivyo, nilichokiandika kinasapotiwa na biblia. Biblia ndiyo ina-support nilichokiandika.

Kwa hiyo hoja yako ni hafifu haina maana katika mada hii.
Toa maandiko ya kwenye biblia kusema generally biblia inasupport hapo si sahihi,kama huna maandiko sema sina ili tuone kama yapo yanayohusiana naulichoandika tukupatie.
 
Naona umeniuliza swali ila hujajibu maswali yangu, hii inaonesha hujui unachokizungumza. Jaribu kusoma mambo yatakayokusaidia katika maisha yako ya kila siku hizo hadithi za kwenye biblia naona zinakuchanganya
Rejea maelezo yako ya awali utaelewa kwanini nimekuuliza maswali hayo.

Aidha, maswali ni kipimo na njia muhimu na msingi katika kufahamu uelewa na ukweli wa mtu katika jambo hilo.

Uelewa au ukweli wa mtu katika mambo hauwezi kuacha kuhusisha maswali.
 
Mkubwa sisi kama wakristo hatuamini kwenye Historia nje ya biblia katika kusimamia imani Yetu,tunaamini yaliyoandikwa na sio wanahistoria kabla ya Yesu na baada ya Yesu,kabla yesu hajaja duniani tangu kuumbwa kwa adamu hadi anakuja kulipita vizazi takribani 42 na
Mtu makini hawezi kuelewa hivi.

Kosa lililowazi hapa ni suala la imani ni nini ; na biblia ni nini ?

Biblia inatokana na masimulizi au kwa lugha nyingine huitwa mapokeo.

Sasa, swali hapa, labda lingekuwa mapokeo ni nini ?

Hiki unachojaribu kueleza hakina ukweli wowote, bali upotofu.

Kwa chenyewe kinakinzana na akili pia uhalisia.
 
lile andiko linalosema Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa,maarifa yaliyosemwa hapo sio maarifa ya kijamii(elimu dunia) bali ni maarifa ya imani ,kujua maandiko na kuyatafasiri maana yake ili mtu asikudanganye na ndiomaana imeandikwa
Mtu makini atajiuliza:

Kwa vipi maarifa ya Imani hayahusiani na maarifa ya jamii au elimu dunia ?

Je, imani ni nini ; na elimu dunia maana yake ni nini ?

Mtu huyo huyo makini angeenda mabli zaidi na kujiuliza:

Kumcha Bwana ni nini ; inawezekanaje yatokanayo na kumcha Bwana yajitenge na elimu dunia ?
 
Toa maandiko ya kwenye biblia kusema generally biblia inasupport hapo si sahihi,kama huna maandiko sema sina ili tuone kama yapo yanayohusiana naulichoandika tukupatie.
Biblia yote:Agano la Kale na Jipya, kila neno la kitabu chake linaeleza hiki nilichokiandika.
 
Mtu makini atajiuliza:

Kwa vipi maarifa ya Imani hayahusiani na maarifa ya jamii au elimu dunia ?

Je, imani ni nini ; na elimu dunia maana yake ni nini ?

Mtu huyo huyo makini angeenda mabli zaidi na kujiuliza:

Kumcha Bwana ni nini ; inawezekanaje yatokanayo na kumcha Bwana yajitenge na elimu dunia ?
Basi sawa wewe endelea kuamini hicho unachokiamini
 
Toa maandiko ya kwenye biblia kusema generally biblia inasupport hapo si sahihi,kama huna maandiko sema sina ili tuone kama yapo yanayohusiana naulichoandika tukupatie.
Hajui kitu huyo ndiomaana ana rejea biblia nzima achana naye
 
Back
Top Bottom