Yesu Kristo kwa kifo chake alimrejeshea binadamu hali ya Kimungu, yaani akili

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
811
349
Kwa kosa la Adam na Hawa, mtu aliondelewa uwezo wa akili, hali ya kimungu.

Mtu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Ndiyo kusema mtu ni mwili na roho aliyeumbwa kushiriki uumbaji wa muumba wake, Mungu.

Roho au wakati mwingine huitwa akili pia moyo ndiyo maarifa yote.

Pasipo akili au roho, mtu anakuwa sawa na mnyama au mimea, hakuna maendeleo yoyote.

Kwa kosa la Adam na Hawa, wazazi wetu wa kwanza lilijeruhi roho au akili.

Kwasababu hiyo uwezo wa mtu kutenda kiakili yaani kimungu uliondoka akawa sawa na wanyama.

Binadamu kwa muda mrefu sana ameishi kama mnyama. Hakuwa na maarifa yoyote.

Kwa karne na karne mtu aliishi kwa kutumia akili ya ufahamu. Hakuweza kuendeleza mazingira.

Kwa ujio wa Yesu Kristo, kwa Kifo chake alimrejeshea binadamu hali ya sura na mfano wa Mungu yaani akili.

Yesu Kristo ndiyo chanzo cha maarifa yote. Ndiyo kwa njia yake binadamu anaweza kupata maarifa.

Maarifa tuliyonayo hii leo, maendeleo tulionayo hii leo ni kwasababu na kwa njia ya Yesu Kristo, Kifo chake.

Kabla ya Yesu Kristo mambo hayakuwa hivi yalivyo hii leo. Hakukuwa na maarifa pia maendeeleo kama haya baada ya Kristo.

Historia kabla ya Kristo haifahamiki kama ilivyo baada ya Kristo.

Hali ya mambo kabla ya Kristo ni ya kukanganya hivi kwamba inategemea maarifa baada ya Kristo kuitafiti.

Binadamu kabla ya Kristo, hata licha ya Mungu Mwenyewe kuwasaidia na wao wenyewe kumwomba Mungu kwa ajili ya ujio wa Kristo, bado hatahivyo, hali yao ya akili haikuwa imerejeshewa hadhi ile ya mwanzo ya kimungu tuliokuwa nayo kabla ya kosa la Adamu na Hawa.

Kwa ujio wa Kristo, kwa Kifo chake, tumerejeshewa hali ya kimungu yaani akili.

Pasipo Yesu Kristo, kifo chake, mtu asingeweza kuwa na maarifa haya tuliyonayo nyakati hizi, maendeleo. Angebaki kama walivyo wanyama.

Hivyo, mtu anaekataa yale Yesu Kristo aliamuru kwa njia ya Kanisa lake yaani mitume hawezi kupata manufaa ya akili.

Kama lilivyo jua chanzo kikuu cha nishati duniani. Yesu Kristo ndiye chanzo cha maarifa na maarifa yenyewe. Yeye ndiye mwanga. Pasipo Yeye hakuna maarifa, wala maendeleo.
 
Kuhusu mwendelezo wa maendeleo baada ya Yesu ningekubali ikiwa angelikuwa aliacha kizazi toka kiunoni pake kabla ya kurudi kwa baba ake.
 
Hao adam na hawa unahakika gani kwamba walikuwepo mzee?
Adamu na Hawa ni wazazi wetu wa mwanzo, mababu zetu.

Majina Adamu na Hawa yanarejelea wazazi wetu wa mwanzo, mababu zetu.

Ni nani asiye na mababu ambao kwao naye alizaliwa ?

Watangulizi wako upande wa ukoo wa baba na wa mama yako, mnyororo wa ukoo ndiyo Adamu na Hawa.

Je, ni binadamu au mtu gani asiye na watangulizi wake ? Au je, babu na bibi yako hawakuwepo ?
 
Uhusiano wa kifo cha yesu na akili ya binadamu unaunganishwa na point ipi?
Pasipo Yesu hakuna chochote kilichofanyika. Kwa Kifo chake kile kilichoharibu hali ya kimungu ya mtu yaani akili kiliondolewa.

Akili ya binadamu ili iwezekuwa na nguvu au hali ya kimungu ni pekee katika na kwa njia ya Yesu Kristo, Kifo chake.
 
Suleimani alipewa maarifa makuu ya kujenga hekalu ambalo mpka Leo linaheshimiwa, Yesu alikuwepo?
Habari ya hekima ya Suleimani kwa vipi inaweza kutenganishwa na uwepo wa Yesu ?

Biblia, hasa vitabu vya Manabii vinaeleza hili vizuri.
 
Hii mada haina usahihi wa kushabihisha Kristo na akili ya Maarifa ya kidunia, kristo hakuja kuokoa 'nguvu ya uhai' bali kuokoa nafsi.

Mwanzo 3:7 hapo utaona 'nguvu ya uhai' inaposhindwa kumudu nafsi, hawa alishindwa kumudu na baadaye unaona walijua wako uchi, why?

Kwa sababu ile nafsi ya kujua kila kitu ilionekana baada ya kuacha precaution ya Mungu.

So mtoa mada tenganisha hivyo vitu.
 
Hii mada haina usahihi wa kushabihisha Kristo na akili ya Maarifa ya kidunia, kristo hakuja kuokoa 'nguvu ya uhai' bali kuokoa nafsi.

Mwanzo 3:7 hapo utaona 'nguvu ya uhai' inaposhindwa kumudu nafsi, hawa alishindwa kumudu na baadaye unaona walijua wako uchi, why?

Kwa sababu ile nafsi ya k
Swali la kujiuliza ni "Nafsi ni nini ?

Nafsi inatoka kwa nani ?

Mtu ni nafsi yenye roho na utashi anayeweza kuanzisha na kutawala matendo yake.

Saikolojia inakubali kuna nafsi ya nje na nafsi ya ndani.

Nafsi ya nje ndiyo nafsi kuu, ambako nafsi ya ndani imetoka.

Nafsi ya nje ndiyo huitwa Mungu. Nafsi ya ndani huitwa mtu.

Nafsi ya nje yaani Mungu ndiyo imefanya au inafanya nafsi ya ndani yaani mtu.

Yesu Kristo ni Nafsi ya Pili ya Mungu, ni Mungu ambaye pasipo Yeye mtu hakufanyika.

Hivyo haiwezekani kufafanua Nafsi ya ndani yaani mtu pasipo Nafsi ya nje yaani Mungu, Nafsi ya Pili ya Mungu.

Hivi ndivyo pia haiwezekani kufafanua roho au akili ikitenganishwa na nafsi.

Ni vizuri kuelewa kwamba Yesu ndiye maarifa yaliyofanya au yanayofanya vitu vyote.

Pasipo Yeye hakuna chochote kimefanyika au kinafanyika.

Ndivyo pia mtu hawezi chochote pasipo akili au roho, anakuwa sawa na wanyama.

Mungu alimuumba mtu ili ashiriki kazi ya uumbaji wake.

Mungu hakumuumba mtu kama alivyowaumba wanyama au mimea.

Mtu kwa mwili na roho au akili. Hii roho au akili ndiyo uwezo wa kufanya kama Mungu.

Pasipo roho au akili mtu anabaki sawa kama wanyama.

Wazazi wetu wa mwanzo, Adamu na Hawa kwa kosa walilolitenda liliharibu hali ya kimungu ya mtu aliyokuwa nayo hapo kabla, "...na tumfanye mtu kwa mfano na sura ya Mungu...".

Kuja kwa Yesu Kristo duniani, Kifo chake kinashughulikia roho au akili, hali ya kimungu ya mtu iliyoharibiwa kwa dhambi.
 
Kwa kosa la Adam na Hawa, mtu aliondelewa uwezo wa akili, hali ya kimungu.

Mtu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Ndiyo kusema mtu ni mwili na roho aliyeumbwa kushiriki uumbaji wa muumba wake, Mungu.

Roho au wakati mwingine huitwa akili pia moyo ndiyo maarifa yote.

Pasipo akili au roho, mtu anakuwa sawa na mnyama au mimea, hakuna maendeleo yoyote.

Kwa kosa la Adam na Hawa, wazazi wetu wa kwanza lilijeruhi roho au akili.

Kwasababu hiyo uwezo wa mtu kutenda kiakili yaani kimungu uliondoka akawa sawa na wanyama.

Binadamu kwa muda mrefu sana ameishi kama mnyama. Hakuwa na maarifa yoyote.

Kwa karne na karne mtu aliishi kwa kutumia akili ya ufahamu. Hakuweza kuendeleza mazingira.

Kwa ujio wa Yesu Kristo, kwa Kifo chake alimrejeshea binadamu hali ya sura na mfano wa Mungu yaani akili.

Yesu Kristo ndiyo chanzo cha maarifa yote. Ndiyo kwa njia yake binadamu anaweza kupata maarifa.

Maarifa tuliyonayo hii leo, maendeleo tulionayo hii leo ni kwasababu na kwa njia ya Yesu Kristo, Kifo chake.

Kabla ya Yesu Kristo mambo hayakuwa hivi yalivyo hii leo. Hakukuwa na maarifa pia maendeeleo kama haya baada ya Kristo.

Historia kabla ya Kristo haifahamiki kama ilivyo baada ya Kristo.

Hali ya mambo kabla ya Kristo ni ya kukanganya hivi kwamba inategemea maarifa baada ya Kristo kuitafiti.

Binadamu kabla ya Kristo, hata licha ya Mungu Mwenyewe kuwasaidia na wao wenyewe kumwomba Mungu kwa ajili ya ujio wa Kristo, bado hatahivyo, hali yao ya akili haikuwa imerejeshewa hadhi ile ya mwanzo ya kimungu tuliokuwa nayo kabla ya kosa la Adamu na Hawa.

Kwa ujio wa Kristo, kwa Kifo chake, tumerejeshewa hali ya kimungu yaani akili.

Pasipo Yesu Kristo, Kifo chake, mtu asingeweza kuwa na maarifa haya tuliyonayo nyakati hizi, maendeleo. Angebaki kama walivyo wanyama.

Hivyo, mtu anaekataa yale Yesu Kristo aliamuru kwa njia ya Kanisa lake yaani mitume hawezi kupata manufaa ya akili.

Kama lilivyo jua chanzo kikuu cha nishati duniani. Yesu Kristo ndiye chanzo cha maarifa na maarifa yenyewe. Yeye ndiye mwanga. Pasipo Yeye hakuna maarifa, wala maendeleo.
Pia usiache kuwashukuru wale waliofanya juhudi ya kumkimbiza hadi wakamkamata Yesu na kumpeleka msalabani ili wewe upate akili ya kiungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya nipe uthibitisho wa kipi umeona watu waliokuwa kabla ya yesu wamekitenda au kukifanya hadi kuwaona kuwa hawana uwezo wa kutambua, kuona, kufikiri na kuhukumu
Unafafanuaje uwezo wa kutambua ?

Unafafanuaje uwezo wa kuona ?

Unafafanuaje uwezo wa kufikiri ?

Unafafanuaje uwezo wa kuhukumu ?

Haya yote yanajibu swala la maarifa.
 
UONGO MTUPU
>Umeandika weeeee mambo yanayohusu biblia umeogopa kuweka hata kakifungu kamoja kanako kusapoti hichi ulichoandika!
>Umehusisha kifo cha Yesu na kupata maarifa ya ki Materials kitu ambacho Biblia haijawahi sema na Yesu hajawahi sema hivyo!
>Dunia hata kabla ya Ujio wa Yesu ilikuwa na maendeleo kulikuwa na serikali,jeshi,magari ya farasi,vyombo vya usafiri majini ,barabara majumba makubwa kama Hekalu la suleimani,minara ya Babeli,ma piramidi ya misri nk hayo yoote yalihitaji maarifa kwa wakati ule
>Kifo cha Yesu pale msalabani hakikumaanisha Mwanadamu kurejeshewa hali ya Kiungu huu ndio uongo shetani aliowadanganyia Adam na hawa pale Bustanini kwamba wakila tunda watakuwa kama Mungu!
>Kifo cha Yesu pale msalabani lengo ni kutoa kafara ili Damu na maji vikitoka ndio Mungu ajipatanishe na wanadamu ili kila mwanadamu aweze kuwapata ondoleo la dhambi kupitia maji na damu ya Yesu vilivyomwagika pale msalabani, 1Petro 1:18-20,wakolintho 1:20,Efeso 1:7,
>Unapataje sasa Damu na Maji alivyovitoa Yesu pale msalabani??,Kwa ondoleo letu la dhambi sisi kama wanadamu ili dhambi zetu ziweze kuondolewa lazima tubatizwe kwa maji mengi na kwa jina la Yesu kristo (sio baba mwana na roho mtakatifu) "Kwa ondoleo la dhambi" Matendo ya mitume 2:38

:Kifo cha Yesu pale msalabani ilikuwa ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi kwa wanadamu ,dhambi waliyoifanya Adamu na Hawa pale bustanini na sio hicho ulicho andika
 
Kifo cha Yesu pale msalabani hakikumaanisha Mwanadamu kurejeshewa hali ya Kiungu huu ndio uongo shetani aliowadanganyia Adam na hawa pale Bustanini kwamba wakila tunda watakuwa kama Mungu!
Kuna tofauti ya kuwa Mungu na hali ya kimungu.

Unajua hilo ?

Mtu kuwa na hali ya Kimungu hakumfanyi Mungu.

Shetani aliwaambia Adamu na Hawa Wakila tunda watakuwa kama Mungu na siyo watakuwa na hali ya kimungu. Sijui unaelewa hilo.

Kwani Mungu aliwaumba watu na hali ya kimungu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom