Yericko Nyerere kizimbani

Yericko Nyerere kizimbani

Kibatala mweupe tu.Alizimwa na Tulia kwa 30 minutes kwenye hoja ya mita 200.

Halafu kuwa na mawakili wazuri sio kushinda kesi.

Angalia jopo la akina Mramba na Yona lakini walikwenda na maji.

Angalia jopo la mawakili la kina babu seya mzee wenu marando ndani lakini wamekula mvua.

Kuwa na mawakili wazuri kunaweza kukusaidia kisaikolojia usipate kiharusi wakati kesi inaendelea au kidoogo wanaweza kusababisha ukapunguziwa miaka dogo .
 
Hio ni kazi ya Mahakama.

Chunga tu na wewe usijedakwa na Dola kwa kuiona Serikali haina busara.

Huyo Bwana amesema kweli, huna haja ya kumtisha. Hayo mashtaka ni mepesi sana, hakuna kesi hapo.
 
MFANYABIASHARA Yericko Nyerere amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matano ya kutoa taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Nyerere alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka na mawakili wa Serikali, Simon Wankyo na Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Anashitakiwa chini ya Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao Namba 14 ya 2015. Nyerere anadaiwa Oktoba 25, mwaka huu katika eneo lisilojulikana, alichapisha taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook, akidai kuwa ?Piga kura leo huku ukikumbuka kifo cha Mwangosi, Mateso ya Ulimboka na Kibanda, mateso ya vijana wetu wa JKT, ukikumbuka hayo fanya uamuzi sahihi bila ushabiki?.

Wanyo alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Nyerere alichapisha taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook kuwa Taifa la Tanzania kuanzia leo halihitaji amani, linahitaji haki tu.

Inadaiwa, alichapisha taarifa za uongo kupitia mtandao huo kuwa, ?siku ya leo mpaka siku ya kuapishwa Lowassa, taifa halihitaji amani, bali taifa hili linahitaji haki tu, amani ilishatoweka siku nyingi, kilichobaki ni uvumilivu tu?, njia sahihi ya kulitibu taifa hili ni kwa dola dhalimu kutenda haki hata kama itawauma?.

Inadaiwa Nyerere aliendelea kudai kuwa ?Uchaguzi huu ni vita, anayedhani ni demokrasia apimwe akili?hii ni vita kati ya umma na dola, ni vita kati ya wema na ubaya, kati ya shibe na njaa, kati ya masikini na matajiri? umma umekosa amani na furaha, fursa pekee waliyoipata watanzania wanamjua rais wao wanayekwenda kumchagua kesho, jaribio lolote litakalofanywa na CCM na vibaraka wao la kukwamisha matakwa ya umma, litaondoa hata ule uvumilivu kidogo walionao watanzania na kisha vitazaliwa vichaa chongo ambavyo hata risasi na mabomu hayatakizima?.

Aidha, anadaiwa siku hiyo hiyo alichapisha taarifa nyingine ya upotoshaji kupitia mtandao ikisema ?mipango ya hujuma ya JK toka Ngurdoto Arusha muda huu?Kikwete yupo Ngurdoto Arusha na wakuu wote wa mikoa na wilaya Tanzania nzima pia wakuu wa vyombo vya dola na wanadhimu mbalimbali? wakuu wa mkoa wanaelezwa kuwa NEC kwa kushirikiana na CCM tayari wameshatengeneza kura bandia kwa kutumia mfumo wa kalamu za kichina? pia wanaamuliwa kuhakikisha wanahujumu kampeni za Ukawa kwa kutumia vyombo vya dola, wanaagizwa kuhakikisha kamatakamata ya vijana bodaboda wiki moja kabla ya uchaguzi na zaidi wanaagizwa wakawaagize maDC kote nchini kuhakikisha wanalinda maslahi ya CCM siku yaUchaguzi.

Katika mashitaka mengine, Nyerere anadaiwa Septemba 3, mwakahuu katika eneo lisilojulikana alichapisha taarifa za uongo kuhusu uwepo wa akaunti ya benki ya kughushi inayomilikiwa na mtanzania katika benki ya HSBC Tawi la North London, ikionesha CCM imemwekea Dk Wilbrod Slaa Euro milioni 1.5 kupitia kwa mchumba wake, Josephine Mshumbusi ikiwa ni rushwa ili kushinda uchaguzi mwaka huu.

Nyerere anadaiwa alichapisha na kusambaza taarifa hizo za uongo kupitia mtandao wa Facebook kwa lengo la kupotosha umma katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Mshitakiwa alikana mashitaka na upande wa jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, pia hawana pingamizi la dhamana kwa mshitakiwa huyo.

Nyerere aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja, aliyesaini hati ya Sh milioni tano. Kesi itatajwa tena Desemba Mosi mwaka huu.

Chanzo: HabariLeo


==========

My take.

Wacha huyu mtoto ajifunze nidhamu kidogo. Manake wakati mwingine inabidi mtu mpk achezee mikwaju japo kidogo ndio ataheshimu Dola.

Mbona siuoni ungo wake?,hayo ndio yanayotusibu
 
Yericko amechaguliwa na Taasisi kubwa duniani kwenda kuwakilisha vijana wa kitanzania kwenye kongamano la wataalamu vijana duniani wa IT ataenda Stockholm Sweden January.
 
Sio Jela za bongo kijana.
Kamuulize Yericko ndio atakupa habari kamili.
Uraiani mambo ya Wanname kuoana Ni ya Hiari.
Huko Hiari hakuna.

Ukipendwa tu we kaanze kupaka Wanja kabisa.

Ushawahi kupaka wanja nini?
 
Leo huyu fisi kawa mfanyabiashara?? Mi nilijua yeye ni jasusi

Majasusi si wajinga kiasi kile,wanafanya mambo yao kwa usiri mno na ngumu kujulikana,akija kujulikana mnaanza kushangaa ndo mnamwona,yule alikuwa mropokaji tu.
 
Ni njia nzuri Yericko kuelekea kuwa mwanaharakati kamili heshima kwako Yericko,achana nao hao ma ccm ya lumumba , Cdm ni chama makini na kinawanasheria makini na ndio maana ma ccm yanawabambikia wana chadema vijikesi vingine havina kichwa wala miguu lakini unakuta chama makini cdm kinazidi imalika.Yrecko cdm. Cdm yericko mapambano yanaendelea, mm cipendi ccm na watu wke ninajivunia kuto kuipenda ccm
 
Majasusi si wajinga kiasi kile,wanafanya mambo yao kwa usiri mno na ngumu kujulikana,akija kujulikana mnaanza kushangaa ndo mnamwona,yule alikuwa mropokaji tu.
Mkuu waswahili wanasema "hapo umegusa ndipo"
 
Teh teh teh.Mkuu hujasikia pombe magufuli kasema anataka Kufuta Ruzuku za vyama vya upinzani?Sasa hio pesa wapate wapi? Labda wazee wa viroba kina matumbo na Nicholas waanzishe mradi mpya wa Chibuku pale Mbagala.
Bahati mbaya sana mambo ccm walifanya wakidhani wana kaba upinzani yanawafanya waone ngumu ya kuongoza nchi.Bahati mbaya sana Yericko ni mfanya biashara na wengine wengi tuu humu ndani.Si km nyie mnaoishi kwa fadhila na wizi wa ccm.
 
Last edited by a moderator:
hakuna kesi hapo,Yeriko anashinda asubuhi,matamko ya kisiada hayawez kumfunga MTU kama Luna Uhuru Wa mahakama
 
Hivi kusema Watanzania wakumbuke mateso yao na wafanye maamuzi sahihi kwenye uchaguzi bila ushabiki ni kusambaza uwongo?

Kusema kwamba ccm ni lazima itende haki ni jinai?

Kutahadharisha kwamba ulaghai wowote utakaofanyika utaleta shida kwa Taifa ni uzushi?

Kuandika ukweli kwamba amani Tanzania ilishatoweka miaka mingi kilichobaki ni uvumilivu ni uwongo? Kuna amani gani katika mazingira ya watu kufa kila siku kwa kukosa huduma za jamii huku kodi wanayolipa ikigawanwa na mafisadi wanaolindwa na serikali? Uwongo uko wapi?

Dola na mitutu haijawahi kudumisha uvumilivu. Hakuna vitisho vilivyowahi kuimarisha utawala duniani. Si mnasoma habari za John Okelo aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi ya Zanziba namna alivyokwama pamoja na vitisho vyake?

Ninaomba kama kuna kosa la kweli linalompeleka Jericho kizimbani tushirikishane ndugu zangu. Tanzania ni yetu sote. Tunapaswa kupeana taarifa sahihi na kamili ilikwa pamoja tusaidiane kusimamia maslahi ya taifa letu.

JERICHO ANASHITAKIWA KWA KUSEMA CCM NA WASHIRIKA WAKE WAMEANDAA KARATASI ZA KUPIGA KURA KABLA:- NANI ASIYELIJUA HILI DUNIANI? MASANDUKU YALIYOKAMATWA NA KURA ZINGINE ZIKIWA ZIMEPGIWA HADI MARASANI NANI ALIZITENGENEZA?

MBONA NAONA KAMA SYRIA NA NCHI ZA KIARABU WATU WANATUNGIWA MAKOSA KWA KUWA WANATAKIWA KUUAWA AMBAPO NI LAZIMA WAUAWE NA TRIALS NI KAMA NJIA YA KUTIMIZA MAAMUZI YALIYOKWISHA KUFIKIWA?

NINAOMBA MWENYE KUJUA MAKOSA SAIHI YA JEERICHO ATUSHIRIKISHE. LA KAMA NI HAYA, BASI KUNA TATIZO KUBWA ZAIDI LINAKUJA.
 
Back
Top Bottom