Yapi maoni yako?

The Son

JF-Expert Member
Jul 30, 2012
461
0
Miongoni mwa ndugu, jamaa na
marafiki wanaoishi mbali mbali yupo
ambaye analazimika kuwajulia
wenzake hali au yeyote anaweza
kumjulia hali mwingine?

Nahitaji kujuzwa maana wapo
wanaoona kuwa fulani ndiye
anayepaswa kuwajulia hali. Kwa upande
wangu naona si vibaya kwa yeyote
ambaye atapata fursa kuwajulia hali
wenzake. Sioni kama kuna haja ya
kumtupia mtu lawama kuwa hakujulii
hali wakati wewe pia unakaa kimya.
Mara nyingi nikiulizwa swali la
kwanini unakuwa kimya sana nalijibu
kwa swali sababu anayeniuliza ana
uwezo na majukumu kama mimi sasa
iweje atake mimi tu nimjulie hali wakati yeye pia huwa kimya?
Kwa nini naye asinijulie hali siku
nyingine akiona niko kimya badala
yake anabaki kulaumu tu? Mtu
hujanipigia simu nikaacha kupokea
wala hujanitumia sms nikaacha
kuijibu. Pia hujanibipu nikaacha
kukupigia... lawama za nini?

QUOTE]Lawama si mzigo[QUOTE
 

joyness

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
235
195
wengine wanajiona wakubwa au wanapesa so hawastahili kutafuta wenzao mpaka watafutwe.
 

Bra-joe

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,562
2,000
Mara nyingi hali hiyo hutokea kama wewe ni mdogo halafu ndugu zako waliokuzidi umri umewashinda kimaisha, (mambo yako safi) mara nyingi wanaogopa kuonekana wanamlilia khali bwana mdogo.
 

mdida

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
1,607
1,225
mimi naona ni tabia ya mtu, sisi tuna ndugu yetu mmoja nisipompigia simu mimi hata mwaka uishe hawezi piga yeye, inafikia namwambia hata kubeep tu lakini wapi.
 

makavulaivu

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
401
0
Kunakautamaduni ka wenyepesa ndio wakubwa zako.You are the one to initiate calling, texting and visiting. Money has became the determinant factor ...!
 

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,158
2,000
sio ishu kubwa sana, inahitaji uelewa tu kuwa kutokupiga simu haina maana ya dharau aidha una pesa au la
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom