Makoye Matale wacha uwongo mzee mzima.Kibaden aliachishwa kazi baada ya mzunguko wa kwanza kwisha na sio baada ya sare ya 3-3.Stewart aliomba mwenyewe kuacha kazi baada ya kupata kazi kwenye kituo cha michezo kipya .Ulitamba sana na ohh tutawafunga 6 leo umebaki kuzua.
Hapo asingeondolewa kocha tu, kufukuzana kungeenda hadi kwa wachezaji, viongozi na wanachama... Mechi yenyewe ni bonanza, ungeshinda mechi ya ligi ingekuwaje?
Ni kweli hiyo observation yako lakini wamesajiriwa na nani? benchi la ufundi au ndio viongozi wa timu maana wakati mwingine ukimletea kocha wachezaji hata wawe wazuri namna gani bila kuomba mapendekezo yake inachukua muda kuweza ku-settle kwa kuwa anahitaji kuwazoea kwanza kila mmoja kiuchezaji lakini kama alishiriki mwenyewe inakuwa rahisi maana uchezaji wa kikosi kilichopo anakuwa anakijua hivyo wakati anatafuta wachezaji wengi tayari anakuwa anaangalia hao atakaowachukua watawezaje kucheza na kikosi kilichopoLakini tuache blah blah mimi mshabiki wa Simba lakini sioni sababu kwa kikosi cha yanga kufungwa na timu yoyote hapa Tanzania
Una
Kaseja, Mbuyu,yodan, canavaro,msuva, ngasa, okwi, kavumbagu,kiiza,chuji, dilunga yaani hapana kocha bomu...
\Aaah!jamani; hii mechi tulikubaliana isitugombanishe kwa kuwa ni ya bonanza au fete kama alivyosema manji.sasa inakuwaje tena Brandts anaondolewa?
kila mechi mtakuwa mkibadilisha makocha,wekezeni ktk soka,hususani vijana na kumbukeni soka si majina wala meneno ya vijiweni soka ni uwanjani.
Ngoja tulinganishe kipindi kile timu zote zina makocha toka Uganda.Kati ya Yanga sc na Simba nani aliyetia fora kufukuza makocha? Kweli nyani haoni kundule!
Lakini tuache blah blah mimi mshabiki wa Simba lakini sioni sababu kwa kikosi cha yanga kufungwa na timu yoyote hapa Tanzania
Una
Kaseja, Mbuyu,yodan, canavaro,msuva, ngasa, okwi, kavumbagu,kiiza,chuji, dilunga yaani hapana kocha bomu...
Lakini tuache blah blah mimi mshabiki wa Simba lakini sioni sababu kwa kikosi cha yanga kufungwa na timu yoyote hapa Tanzania
Una
Kaseja, Mbuyu,yodan, canavaro,msuva, ngasa, okwi, kavumbagu,kiiza,chuji, dilunga yaani hapana kocha bomu...
Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro.
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013
hiloo ndio soka la simba na yanga..Ngoja tulinganishe kipindi kile timu zote zina makocha toka Uganda.
Simba: Basena>Circovic>Patrick>King Mputa na sasa Loga, wanne walitimuliwa.
Yanga: Timbe>Papic>Tom>Brandts, wote hao wanne wametimuliwa.
hiloo ndio soka la simba na yanga..