Yanga yamtimua kocha wake Ernie Brandts

Yanga yamtimua kocha wake Ernie Brandts

testa

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
442
Reaction score
183
Uongozi wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.

Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.

Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.

Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.

Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.

Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.

Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix "Minziro".

Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.

Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.

Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.


Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.

DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013
 
Uongozi wa mabingwa watetezi wa Tanzani bara Yanga umeamua kuachana rasmi na kocha wake raia wa uholanzi,source bin zubeiry blog

Naamini matokeo mazuri na bora huja baada ya uvumilivu wa kutosha and not otherwise!
 
Kama wamemtimua , YANGA itakuwa imefanya kosa kubwa sana, miezi 6 ageahwa ligi iishe, Kocha alikuwa ni mzuri sana, tatizo lake ni mmoja tu kuwa wachezaji walianza kumpanda kichwani, wachezaji wa yanga hawana nidhamu kabisa kwa kipindi hiki , ovyo !
 
Naamini matokeo mazuri na bora huja baada ya uvumilivu wa kutosha and not otherwise!

Lakini tuache blah blah mimi mshabiki wa Simba lakini sioni sababu kwa kikosi cha yanga kufungwa na timu yoyote hapa Tanzania
Una
Kaseja, Mbuyu,yodan, canavaro,msuva, ngasa, okwi, kavumbagu,kiiza,chuji, dilunga yaani hapana kocha bomu...
 
Hivi huyo kocha alikuwa akicheza namba ngapi pale uwanjani? Kwa nini tu iwe kocha ndio kaboronga na siyo wachezaji waliokuwa uwanjani? This is quite unfair, otherwise pia ilitakiwa kuwa hivi:-
  1. Mgonjwa akifariki daktari wake awe anafukuzwa kazi!
  2. Mwanafunzi anapofeli basi Mwalimu afukuzwe kazi pia!
  3. Kampuni isipopata faida na ufanisi basi CEO afungashiwe virago!
  4. Serikali ikiboronga kama hivi majuzi basi Mkuu wake atemeshwe mzigo na siyo kusubiri kipindi chake kiishe!
  5. Jeshi likishindwa vita Jenerali wake aagwe!
 
Habari kutoka Club ya Yanga asubuhi hii ni kuwa wamemtimua kocha wao Ernest Brandts kufuatia kipigo cha goli 3-1 toka kwa Simba SC katika mchezo wa Nani Mtani Jembe uliofanyika Juzi jumamosi.

Bado Mizengo Pinda tu, nae atupishe.


ZlSXkbBs7lqmZrfxiho fKwSEJRZVDgUjkoLgiTFxhYeXID23menXR1qG3ocXwMY1OqOgR1LJQVrFqXdsT17DQ0bJ2dU7Tt80LC653s4ZY2Qe8v8AY7wb4bZjKZ0AAAAASUVORK5CYII=
 
Kama wamemtimua , YANGA itakuwa imefanya kosa kubwa sana, miezi 6 ageahwa ligi iishe, Kocha alikuwa ni mzuri sana, tatizo lake ni mmoja tu kuwa wachezaji walianza kumpanda kichwani, wachezaji wa yanga hawana nidhamu kabisa kwa kipindi hiki , ovyo !

umenena mkuu,kila mchezaji alikuwa zaidi ya mwalimu
 
Kama ni kweli wamemtimua bure kwa sababu Yanga ndiyo iliyonufaika zaidi ya Simba katika mechi hiyo ya nani mtani jembe, Yanga imenufaika kwa sababu zifuatazo
1. Imeweka kibindoni shs million 99 wakati wao Simba wakiambulia million 1 tu na kombe le bati
2. Makosa ya kiufundi yameonekena ambapo kocha angeyafanyia kazi kabla ya mechi ya kugombania point tatu mhimu
3. Kulingana mna matokeo ya mechi hiyo mechi ijayo piga uwa garagaza lazima Simba itafungwa tu.
Wamwache kocha huyo afanye kazi yake.
 
Basi aletwe kocha mwenye kiwango cha juu sana hasa makocha wa kijerumani hawanaga masikhara lazima wachezaji wajitume 100%.
 
Kama ni kweli wamemtimua bure kwa sababu Yanga ndiyo iliyonufaika zaidi ya Simba katika mechi hiyo ya nani mtani jembe, Yanga imenufaika kwa sababu zifuatazo
1. Imeweka kibindoni shs million 99 wakati wao Simba wakiambulia million 1 tu na kombe le bati
2. Makosa ya kiufundi yameonekena ambapo kocha angeyafanyia kazi kabla ya mechi ya kugombania point tatu mhimu
3. Kulingana mna matokeo ya mechi hiyo mechi ijayo piga uwa garagaza lazima Simba itafungwa tu.
Wamwache kocha huyo afanye kazi yake.

Yanga walipata mil.96.9 Simba walipata mil.100 + mil.3.1+ kombe +shangwe
 
Waangeanza na yule kipa sharubaro aliyejifunga goli la 3 mambo menine yangejiseti wenyewe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom