Yanga yamtimua kocha wake Ernie Brandts

Yanga yamtimua kocha wake Ernie Brandts

Inabidi Yanga waandae kabisa list ya makocha watakaokuwa wanachukua timu kila baada ya miezi michache, ili ijulikane wazi baada ya mechi ya Simba atakuja huyu !!
 
Hivi hakuna mchezo mwingine wa hivi karibuni kati ya Simba na Yanga? :becky:
 
Mimi kama mshabiki na mpenzi wa Yanga, nawaomba viongozi wa Yanga wamlete mrithi haraka na Kocha wetu wa sasa Brands apatiwe haki zake za msingi kwa wakati. YANGA MBELE DAIMA MWIKO
 
Inabidi Yanga waandae kabisa list ya makocha watakaokuwa wanachukua timu kila baada ya miezi michache, ili ijulikane wazi baada ya mechi ya Simba atakuja huyu !!

Yaani kufungwa na Simba 3-1 ndo munatimua kocha? Ingekuwa Azam ndo imewapa kichapo kile mungevumilia tu! Hata hivyo Yanga ilicheza chini ya Kiwango hata mechi na KMKM,na pia ni bahati tu kwa aliyekuwepo uwanjani Jmosi Yanga ingeweza kufungwa hata 5-1 kama Simba wangekuwa makini zaidi
 
Kama ni kweli wamemtimua bure kwa sababu Yanga ndiyo iliyonufaika zaidi ya Simba katika mechi hiyo ya nani mtani jembe, Yanga imenufaika kwa sababu zifuatazo
1. Imeweka kibindoni shs million 99 wakati wao Simba wakiambulia million 1 tu na kombe le bati
2. Makosa ya kiufundi yameonekena ambapo kocha angeyafanyia kazi kabla ya mechi ya kugombania point tatu mhimu
3. Kulingana mna matokeo ya mechi hiyo mechi ijayo piga uwa garagaza lazima Simba itafungwa tu.
Wamwache kocha huyo afanye kazi yake.
we kweli mburura, hivi 2 na 3 ni 'sababu' za yanga kunufaika
 
uongozi wa klabu ya young africans sc umempatia taarifa (notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi ernie brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana disemba 22 mwaka huu.

Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya ligi kuu, kirafiki na bonanza la nani mtani jembe dhidi ya simba sc mwishoni mwa wiki.

Hatua ya young africans sc kusitisha huduma na brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika mashindano yanayotukabili.

Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa yanga sc na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.

Young africans sc imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya ligi kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.

Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.

Ikiwa brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi fred felix “minziro”.

Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.

Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na mashindano ya klabu bingwa afrika.

Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa vpl.


Abdallah bin kleb
mwenyekiti - kamati ya mashindano
young africans sports club.

Dar es salaam
23 disemba, 2013
wamelewa fedha kagoda ltd
 
Wafukuze tu hata wachezaji ikiwezekana...timu zetu za kijinga sana hizi.
 
Hivi hakuna mchezo mwingine wa hivi karibuni kati ya Simba na Yanga? :becky:
Kuna kombe la mapinduzi sijui tutakutana na au watatolewa mapema ila tukikutana nao ndo muda wa kuwapiga zingine tano si unajua timu ameachiwa Minziro, kipindi kile aliachiwa na Papic akala tano bila na safari hii sijui kama atakwepa labda kocha mkuu awahi.
 
Km huwa tunakwenda taifa bas nh dhahil kabisa kocha hana UWEZO..!USIANGALIE MATOKEO YA MWISHO ANGALIA TEAM INAPERFOM KWA KIASI GANI!TIMU HAIONYESHI MABADIRIKO YOYOTE..!
 
Inabidi Yanga waandae kabisa list ya makocha watakaokuwa wanachukua timu kila baada ya miezi michache, ili ijulikane wazi baada ya mechi ya Simba atakuja huyu !!

Huyo mzungu wenu sidhani kama atadumu!!!
 
attachment.php
 
3-1, chezea mnyama ehe??

Hebu ninyi mashabiki wa Mnyama acheni mbwembwe, Stewart Hall wa Azam aling'olewa na 3-3 dhidi ya Mbeya City na hapo kwenu Kibadeni na Julio walipigwa out kwa matokeo ya 3-3 dhidi ya Yanga. Sasa siye 'tukitoa mtu macho' kwa kipigo cha 3-1 tuna kosa gani? Tafakarini mambo siyo kuchekacheka tu.
 
Huyo mzungu wenu sidhani kama atadumu!!!
Yeye ana mkataba wa miezi sita tu. Bin Kleb wa Yanga sasa hivi anazunguka Kariakoo na briefcase yenye hela kumvizia kocha wa Simba, Mesi na Tambwe!
 
Walimsajiri ili aifunge simba eti? Sijui kama kocha wangu Wenger angekuwa Tz sijui angekuwa amefundisha timu ngapi!!!!!!
 
Tatizola yanga si kocha bali usajili unaozingatia majina ya watu badala ya uwezo. Kaseja ameisha kimpira ameanza kucheza tangu miaka ya early 90s, kwa uzoefu uliuopo tanzania hakuna mchezaji anayecheza zaidi ya miaka 10 akabaki na kiwango kilekile. Kaseja kwisha kazi ndio maana simba walimtema, yanga wakadaka "makombo". wataendelea kufukuza makocha endapo wataendelea kung'ang'ania wachezaji aina ya kaseja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom