Yanga Yakosa Mwelekeo Mchezo Wa Kagame

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
25
Ni jambo la kusikitisha kwa timu kubwa kama Yanga kutofika uwanjani na kuwaonyesha wananchi burudani. Ninawiwa kusema kwa utaratibu huo hatutafika.

Mimi si mpenzi sana wa mpira. Ila ninapoona ujinga kama uliofanya na timu kubwa kama Yanga ninawiwa kutoa lawama zangu kwao. Mapaka sasa sijapata sababu za kuniridhisha sababu za timu kutofika uwanjani.

Yanayosemwa ni TFF kutowapa shilingi millioni thelasini walizostahili kupewa. Kama ni kweli ni kwa nini wasipewe hela hizo kama ni stahili yao. Kama sababu hiyo ni ya kweli basi TFF ndio wanaoharibu mpira hapa Tanzania. Viongozi ndio wa kulaumu.

Pia ninawalumu Yanga kwa kutoweka uzalendo mbele. Ninachouliza ni kwamba je ni kweli Yanga wanadai hizo fedha? Na je watachkuliwa sheria gani tofauti na kufungiwa.
 
kwa upande wangu swala la hela na swala la SPORTMANS SHIP hayana uhusiano kabisa.
Wachezaji walitakiwa kucheza basi.
viongozi wanatakiwa kufuatilia masilahi nk lakini sio muda wa dakika 90
Ndio nimeelewa wanaposema anatakiwa kiongozi mwenye kujua mpira.
mimi nilidhani washabiki wengi wanajua mpira, kumbe wengine wanajua HABARI za mpira.
Mchezo wenyewe hauko damuni, laiti ungekuwa damuni, wasingejali gharama, wangejali raha ya washabiki wao kwanza.
 
Vyovyote vile wajitetee hawa Yanga, mimi najua watani mmetuogopa na visingizio hivi bado ni vya kitoto. 'Muziki wetu ni mkubwa' kuucheza hamwezi nyieee! Sisi tungesingizia viti vyote pale uwanjani havina rangi hata moja ya Timu yetu mngetuona vilaza sio?

Pole zenu, sie twalijua soka ati... :)
 
Duh, Mod, kumbe nawe ni Mnazi wa SSC? Mimi mwenzie enzi zangu nlikuwa natoroka shule na kwenda kuruka ukuta U/Taifa na Karume kwa ajili ya SSC , tukifungwa nlliweza kutoa chozi lakini baadaye niligundua kuwa kuna ubabishaji mwingi sana kwenye vilabu hivyo kiasi cha kunivunja moyo kabisa!

Nakushauri uhamishie mapenzi yako Mtibwa au Kagera Sugar (sijui kama inawezekana). Simba na Yanga zinachosha; hata akiibuka Kiongozi Msomi anageuka Mjinga! Mfano ni aibu hiyo waliotutia Yanga muda si muda (haijalishi lini) Simba nao wataibua zali lingine.
 
Back
Top Bottom