Yanga SC 0-0 Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa, NBC Premier League

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,327
9,959
Leo Mabigwa wa Kihistoria Yanga Sports Club naingia dimbani kupepetana na Tanzania Prisons, mchezo unatabiriwa huenda ukawa na ushindani wa pekee ukizingatia zinapokutana timu hizi, Tanzania Prisons hukamia sana.

Game hii inaanza saa moja kamili usiku saa za Afrika Mashariki.

Yanga wakijua umuhimu wa mechi hii huenda wakawaanzusha kikosi chake kamili.


Kikosi cha Yanga kinachoanza leo Mei 9, 2022 kwenye Uwanja wa Mkapa:
FSUzUabWQAARHVR.jpg

Timu zimeshaingia uwanjani, mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.

Mchezo umeanza
2' Yanga wanapata kona tatu ndani ya dakika mbili za kwanza lakini wanashindwa kuzitumia vizuri.
4' Yanga wanamiliki mpira tangu kuanza kwa mchezo.
7' Prisons wanapata kona, hatumiki vizuri
10' Walinzi wa Prisons wanamkaba kwa ukaribu Mayele.
13' Fei Toto ana nafasi ya kufunga, anampigia pasi Mayele lakini walinzi wa Prions wanawahi na kuokoa.
16' Mchezo bado umeegemea upande mmoja.
20' Mambo bado ni magumu kwa Prisons.
25' Yanga wanaendelea kupiga pasi nyingi, wapinzani wao wanatumia muda mwingi kuzuia.
33' Prisons wanapata kona, lakini Aucho anaokoa.
37' Yanga wanapata penati baada ya mchezaji wa timu hiyo kuchezewa faulo, anaenda kupiga Mayele

ANAKOSA PENATI, Mayele napiga mpira unapaa juu kabisa ya lango.

38' Yanga wanafanya shambulizi kali Fei Toto anapiga kichwa kinapaa juu ya lango.
40' Presha bado ni kubwa, Yanga wanalisakama lango la wapinzani.
43' Mambo bado ni magumu kwa pande zote.

45' MAPUMZIKO

45' Kipindi cha pili kinaanza, Prisons wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili.
50' Timu zinashambuliana kwa zamu.
55' Yanga wanafanya mabadiliko, wanatoka Diara na Moloko, anaingia Mshery na Nkane
57' Prisons wanaonekana kutulia licha ya Yanga kupambana kutafuta bao.
63' Yanga wanamtoa Kibwana Shomari, anaingia Farid Musa.
71' Yanga wanamtoa Sure Boy anaingia Makambo, mashabiki wa Yanga wanapiga kelele kuonesha kutoafiki maamuzi hayo.
74' Mashambulizi yameelezea upande mmoja, Prisons wanatumia muda mwingi kuzuia.
77' Yanga wanaongeza kasi lakini Prisons wanakuwa wagumu kupitika.
85' Wachezaji wa Prisons wanacheza trick ya kupoteza muda.
87' Mayele anafanya kazi nzuri, anapiga krosi lakini Makambo anachelewa kuimalizia langoni
89' Kipa wa Prisons anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda.
90' Zinaongezwa dakika 5 za nyongeza.
94' Bado mchezo unaendelea.
96' FULL TIME
 
Kwenye list ya Utopolo nikiona jina Mayele najua kabisa kuna 99.9% Utopo kupata goli.
 
Back
Top Bottom