Yanga Sc 0-0 Simba SC| Ligi Kuu NBC | Benjamini Mkapa Stadium

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,991
69,381
Naaam wasalam wakuu,

Ile siku maalumu iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika..Pambano la watani wa jadi katika soka la bongo, leo mtoto hatumwi dukani

Karibuni katika matukio mubashara(live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa Soka la bongo, #KariakooDerby Yanga na Simba utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.

Huu ni mchezo wa namba 160 ligi kuu ya NBC 2021/2022 Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.. mchezo uliopita wa ligi kuu uliochezwa December 11, 2021, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/Suluhu...0-0

Pia Simba mechi ya mwisho kimashindano imetoka kupoteza Penalti 4_3 kutoka Orlando Pirates mnamo tarehe 24/4/2022 na hivyo kufurumushwa nje ya mashindano ya kimataifa yaani katika kombe la Shirikisho Afrika. CAFCC.

Yanga ilicheza mechi ya mwisho ligi kuu na Namungo Fc tarehe 24/4/2022 na kushinda 2_1.

Watabiri wa mambo wanasema huu mchezo wa watani wa jadi unaweza kutoa taswira juu ya Ubingwa wa ligi kuu msimu huu..Yanga ikiwa kileleni mwa ligi na point 54 huku Simba akiwa na alama 41 (Tofauti ya point 13). Ni mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa kasi, nguvu, akili, maarifa na uzoevu mwingi hasa ukizingatia timu hizi zinapokutana haijalishi nani yuko vizuri kwa form au kiwango, wachezaji hubadilika na kucheza soka la kiushindani sana....

Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es salaam

NB: Je 'watatetema' au 'watatetemeka' tena?

_____________________________________________________________

Updates zaidi kukujia kadiri zinavyopatikana

1655' Timu zinajiandaa kuingia dimbani hapa

01' Mpira umeanzaaaa, simba wameanzisha

05' Simba wanapata faulo ya kwanza kuelekea Simba na inazaa kona ambayo inashindwa kuleta matokeo

12' Djuma Shaaban anacheza gonga safi na Mayele kulekea lango la Yanga, Inonga anatibua mipango

14' Simba wanapata faulo karibu na 18 ya Yanga, Diara anapangua na kuwa counter kuelekea Simba, Feisal anapiga shuti linalotoka nje

20' Timu bado zinasomana kwa shambulizi za hapa na pale
Yanga wanaenda mbele, Mayele anapitishiwa anaikosaa inaokolewa na Inonga

28' 🟡Morrison anaenda nje kutibiwa, anapewa kadi ya njano pia Diarra anapewa kadi ya njano kwa kufanya malumbano uwanjani

32' Sakho anamchezea rafu Kibwana, faulu Yanga wanapata inapigwa inaokolewa

37" Simba wanapata faulu, alishika job nje ya 18..inapigwa na Chama inatoka njee

39' Onyango anatibua mpira aliokuwa nao Fiston Mayele kuelekea langoni mwa Simba, Kona.

🟡
40' Vurugu zinatokea kwa lango la Simba...Moloko na Inonga wanapewa kadi ya njano wote wawili

wakati huo ni kona,inapigwa na Saidoo inaokolewa
45+2' Mugalu anamdondosha Aucho, free kick, Refa anakuwa mkali kwa Mugalu

45+3' Half time

45' Mpira umerejea na Yanga wanasogea langoni kwa Simba bila kupata faida ya goli

46' Simba wanagonga pasi kuelekea Yanga lakini mipango yao inatibuliwa

48' 🟡Khalid Aucho anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Sadio Kanoute

54' Kibu Dennis anaingia kuchukua nafasi ya Benard Morrisson, Mzamiru anaingia kuchukua nafasi ya Kanoute.

56' Mkude anapewa kadi ya njano kwa kumuangusha Saidoo

67' Nkane anaingia kuchukua nafasi ya Moloko

71' Almanusura Mayele aandikishe bao la kwanza, shuti lake linaishia kwenye nyavu za pembeni. Yanga 0-0 Simba

73' Mugalu anapiga kichwa kutoka kwenye mpira wa adhabu ndogo, Diarra anaukamata barabara

74' Nkane anapiga mpira unaoambaa langoni mwa Simba, Feisal anashindwa kuupata.

79' Farid Mussa anaingia kuchukua nafasi ya Feisal Salum

85' Simba wanafanya jaribio maridadi baada ya Diarra kupoteana langoni

90+4' Mpira umekwisha, Yanga anapata alama 55 na kuendelea kubaki kileleni na Simba anasalia namba mbili akiwa na alama 42.

========

Mwamuzi wa Mchezo wa Leo ni Ramadhani Kayoko na wasaidizi wake ( Frank Komba [Line1] & Mohamed Mkono [Line2] bila kusahau Elly Sasii [4th Official] ) ilivyotangazwa awali

Azam Tv kupitia chaneli ya Azam sports 1 HD watakuwa mubashara (live).

Kwa wanaotaka Link ikipatikana itawekwa hapa
-----------‐-------------------------------------------------

SIO RASMI utabiri Kikosi cha Simba kinachoanza (STARTING XI)
Manula,Kapombe,Zimbwe Jr,Onyango,Inonga, Mkude,Chama,Sakho,Morrison,Kagere,Bocco

Kocha: Pablo Franco Martin/Suleman Matola

utabiri wa Kikosi cha Yanga kinachoanza (STARTING XI)
Diarra,Shaban,Kibwana,Mwamnyeto,Job,Bangala,Aucho,Moloko,Ntibazonkiza,Feitoto,Mayele

Kocha: Cèdric Kaze
(Kocha Nasridin Nabi bado anatumikia adhabu ya kadi nyekundu kwa hiyo atakuwepo jukwaani)

UPDATES SAA 1630

KIKOSI RASMI CHA YANGA KINACHOANZA

DIARA
DJUMA
KIBWANA
JOB
MWAMNYETO (CAPTAIN)
BANGALA
AUCHO
MOLOKO
NTIBAZONKIZA
FEISAL
MAYELE

SUBs: Mshery,Bacca,Yassin,Mauya,Sureboy,Ngushi,Farid,Nkane,Makambo

KIKOSI RASMI CHA SIMBA: Formation 4-2-3-1 Manula,Kapombe,Hussein(C),Onyango,Henock,Mkude,Sakho,Kanoute,Mugalu,Chama,Morrison

Subs:Beno,Israel,Kennedy,Nyoni,Mzamiru,Bwalya,Bocco,Kibu,Mhilu

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

------------------------------------------------------------------

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Izindaaba
Screenshot_2022-04-25-09-06-23-47.jpg
 
Naaam wasalam wakuu,

Ile siku maalumu iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika..Pambano la watani wa jadi katika soka la bongo, leo mtoto hatumwi dukani

Karibuni katika matukio mubashara(live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa Soka la bongo, #KariakooDerby Yanga na Simba utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.

Huu ni mchezo wa namba 160 ligi kuu ya NBC 2021/2022 Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.. mchezo uliopita wa ligi kuu uliochezwa December 11, 2021, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/Suluhu...0-0

Pia Simba mechi ya mwisho kimashindano imetoka kupoteza Penalti 4_3 kutoka Orlando Pirates mnamo tarehe 24/4/2022 na hivyo kufurumushwa nje ya mashindano ya kimataifa yaani katika kombe la Shirikisho Afrika. CAFCC.

Yanga ilicheza mechi ya mwisho ligi kuu na Namungo Fc tarehe 24/4/2022 na kushinda 2_1.

Watabiri wa mambo wanasema huu mchezo wa watani wa jadi unaweza kutoa taswira juu ya Ubingwa wa ligi kuu msimu huu..Yanga ikiwa kileleni mwa ligi na point 54 huku Simba akiwa na alama 41 (Tofauti ya point 13)

Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es salaam

NB: Je 'watatetema' au 'watatetemeka' tena?

_____________________________________________________________

Updates zaidi kukujia kadiri zinavyopatikana

Mwamuzi wa Mchezo wa Leo ni Ramadhani Kayoko na wasaidizi wake ( Frank Komba [Line1] & Mohamed Mkono [Line2] bila kusahau Elly Sasii [4th Official] ) ilivyotangazwa awali

Azam Tv kupitia chaneli ya Azam sports 1 HD watakuwa mubashara (live).

Kwa wanaotaka Link ikipatikana itawekwa hapa
-----------‐-------------------------------------------------

SIO RASMI utabiri Kikosi cha Simba kinachoanza (STARTING XI)
Manula,Kapombe,Zimbwe Jr,Onyango,Inonga, Mkude,Chama,Sakho,Morrison,Kagere,Bocco

utabiri wa Kikosi cha Yanga kinachoanza (STARTING XI)
Diarra,Shaban,Kibwana,Mwamnyeto,Job,Bangala,Aucho,Moloko,Ntibazonkiza,Feitoto,Mayele

------------------------------------------------------------------

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
Hadi unaboa yani
 
Naaam wasalam wakuu,

Ile siku maalumu iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika..Pambano la watani wa jadi katika soka la bongo, leo mtoto hatumwi dukani

Karibuni katika matukio mubashara(live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa Soka la bongo, #KariakooDerby Yanga na Simba utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.

Huu ni mchezo wa namba 160 ligi kuu ya NBC 2021/2022 Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.. mchezo uliopita wa ligi kuu uliochezwa December 11, 2021, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/Suluhu...0-0

Pia Simba mechi ya mwisho kimashindano imetoka kupoteza Penalti 4_3 kutoka Orlando Pirates mnamo tarehe 24/4/2022 na hivyo kufurumushwa nje ya mashindano ya kimataifa yaani katika kombe la Shirikisho Afrika. CAFCC.

Yanga ilicheza mechi ya mwisho ligi kuu na Namungo Fc tarehe 24/4/2022 na kushinda 2_1.

Watabiri wa mambo wanasema huu mchezo wa watani wa jadi unaweza kutoa taswira juu ya Ubingwa wa ligi kuu msimu huu..Yanga ikiwa kileleni mwa ligi na point 54 huku Simba akiwa na alama 41 (Tofauti ya point 13). Ni mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa kasi, nguvu, akili, maarifa na uzoevu mwingi hasa ukizingatia timu hizi zinapokutana haijalishi nani yuko vizuri kwa form au kiwango, wachezaji hubadilika na kucheza soka la kiushindani sana....

Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es salaam

NB: Je 'watatetema' au 'watatetemeka' tena?

_____________________________________________________________

Updates zaidi kukujia kadiri zinavyopatikana

Mwamuzi wa Mchezo wa Leo ni Ramadhani Kayoko na wasaidizi wake ( Frank Komba [Line1] & Mohamed Mkono [Line2] bila kusahau Elly Sasii [4th Official] ) ilivyotangazwa awali

Azam Tv kupitia chaneli ya Azam sports 1 HD watakuwa mubashara (live).

Kwa wanaotaka Link ikipatikana itawekwa hapa
-----------‐-------------------------------------------------

SIO RASMI utabiri Kikosi cha Simba kinachoanza (STARTING XI)
Manula,Kapombe,Zimbwe Jr,Onyango,Inonga, Mkude,Chama,Sakho,Morrison,Kagere,Bocco

utabiri wa Kikosi cha Yanga kinachoanza (STARTING XI)
Diarra,Shaban,Kibwana,Mwamnyeto,Job,Bangala,Aucho,Moloko,Ntibazonkiza,Feitoto,Mayele

------------------------------------------------------------------

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
This is SIMBA
FB_IMG_1651213665511.jpg
 
Back
Top Bottom