Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,834
- 18,837
Ki ukweli japo mi shabiki wa Simba nataka pia Yanga apite robo, sababu itakuwa heshima kwa TZ kuwa na timu mbili robo fainali, katika timu 8 (Hata Misri ni mara chache anafanikiwa kuingiza timu 2 robo fainali)
Ili Yanga awe na nafasi ya kufuzu robo sio tu amfunge Medeama bali anatakiwa kumfunga kwa goli 5 au zaidi
Likely Scenario ipo hivi
Yanga anagombea nafasi ya pili na C.R.B huku yanga akiwa na goal difference ya -3 wakati CRB ana +2
Yanga akishinda goli 5 atakuwa na pointi 5 na G.D ya +2 na CRB akitoa draw na Ahly kule Algeria (likely scenario) naye atakuwa na pointi 5 na G.D yake ikibaki +2 na Yanga kuwa nafasi ya tatu
Mechi ya 5 Yanga dhidi ya Ahly kule Misri akijitahidi akifungwa 2-1 bado atakuwa na pointi zake 5 bado na goal diffence ya +1
CRB akimfunga Medeama kule Algeria 2-0 naye atakuwa na pointi 8 na G.D ya +4
Mechi ya mwisho Yanga dhidi ya CRB anamfunga goli 3-0 kwa Mkapa anakuwa na pointi 8 na G.D ya +4 huku CRB akibaki na pointi nane pia na G.D ya +1 na Yanga anapitaa kwa kuwa na magoli mengi
So mechi ya kesho ndio mechi pekee ambayo Yanga ana nafasi kubwa ya ushindi, ushindi basi uwe mnono....