Yanga acheni hizo

Yanga acheni hizo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,400
Reaction score
872,007
Leo kulikuwa na maandamano ya wazee wa yanga yaliyozuiwa na serikali wakipinga kukatazwa kujenga football complex pale kwenye jengo lao jangwani kiongozi alikuwa mzee Akilimali
Hebu acheni hizo pale mahali hapatoshi kujenga complex yenye hadhi ya kimataifa labda kama mnataka kujenga uwanja mdogo wa mazoezi
Tafuteni eneo kubwa mjenge kitu cha maana halafu mji umeshajaa ule tanueni panueni mji pelekeni vitu kama hivyo nje ya mji si kila kitu kiwepo mjini
Igeni mfano wa Azam
 
tatizo la yanga wao wakitaka jambo lao wanataka lifanyike..kwann wasiende bunju au kibahs huko..wso bdo wanataka kuleta msongamano town
 
tatizo la yanga wao wakitaka jambo lao wanataka lifanyike..kwann wasiende bunju au kibahs huko..wso bdo wanataka kuleta msongamano town

MiYanga haina tofauti na MiCCM.
 
nilikuwa sijui matusi yanaruhusiwa baada ya kwaresma

Binadamu wamefikia hatua ya kumpangia Mungu ratiba ya kumtendea wema na ubaya. Bahati mbaya kwa Mungu ni kuwa mema amepangiwa ratiba fupi sana. Mwezi mmoja kati ya miezi 12 aliyoitengeneza mwenyewe.

Laiti ningekuwa Mungu......
 
Yanga jana hawakuandamana, kabla ya kuandamana serikali kupitia kwa rc walikutana na watu wa yanga na kuwa ahidi kutatua tatizo lao, yaani kuwaongezea sehemu ili wajenge hiyo city complex.
 
MiYanga haina tofauti na MiCCM.
Na ndiyo maana watapa kibali cha kujenga kiwanja pale jangwani na nyinyi mnaowakejeli kuwa wa kwanza kwenda uwanjani hapo.
Kwa taarifa yenu yanga ilipanga kujenga uwanja mzuri pale jangwani karibu miaka 30 iliyopita lakini tatizo kubwa ni kwamba migogoro ambayo imekuwa ikiathiri utendaji wake na viongozi wakitumia muda mwingi kulumbana/kugombana.
 
Leo kulikuwa na maandamano ya wazee wa yanga yaliyozuiwa na serikali wakipinga kukatazwa kujenga football complex pale kwenye jengo lao jangwani kiongozi alikuwa mzee Akilimali

Una uhakika kuwa hili ndilo dai kuu la malalamiko ya baraza la wazee wa Yanga?

Hebu acheni hizo pale mahali hapatoshi kujenga complex yenye hadhi ya kimataifa labda kama mnataka kujenga uwanja mdogo wa mazoezi

Wahandisi ujenzi waliobobea katika kazi yao wameona panatosha kufanya ujenzi, lakini Mr Mshana Jr anaona hapatoshi...heheheh

Tafuteni eneo kubwa mjenge kitu cha maana halafu mji umeshajaa ule tanueni panueni mji pelekeni vitu kama hivyo nje ya mji si kila kitu kiwepo mjini
Igeni mfano wa Azam

Yanga ni Yanga na Azam ni Azam...huko nje ya mji waache wafyeka vichaka Simba waende huko kusaka nyoka

Na ole wenu tukijenga uwanja wetu mje kung'oa viti kama mlivyozoea kung'oa visiki huko Bunju kama wang'oa kucha
 
Hao simba luwala wanatafuta ligi na timu ya wananchi? Wataumia ndio maana yanga hawana mpango wa kwenda kuwinda ndezi kule boko.
 
binadamu wamefikia hatua ya kumpangia mungu ratiba ya kumtendea wema na ubaya. Bahati mbaya kwa mungu ni kuwa mema amepangiwa ratiba fupi sana. Mwezi mmoja kati ya miezi 12 aliyoitengeneza mwenyewe.

laiti ningekuwa mungu......

.....teamb wote wangeenda....................
 
KWANI LILE JENGO LA YANGA NI LA MTU BINAFSI NA HATI YAKE ANAYO,KANDAMBILI WANAHANGAIKA TU.

HALAFU Mzee AKILIMAV ANASEMA WATAINYIMA KURA CCM,KWANI YEBO YEBO WOTE NI MAGAMBA?

Ngoja tuwanyoshe leo pale Taifa wawe na adabu.
 
Kafie mbali kule. Aliyekwambia hapatoshi nani? Wewe ndio architecture? Eti Bunju, kwa kuwa Simba Koko bunju basi bunju ndio umekuona wewe.

Kama hy serikali inayokataza ingekuwa na akili, ingejenga kiwanja kipya pale pale kilipo cha zamani. Sijui akili gani imetumika, yaani viwanja viwili sehemu moja.

Basi wapeni na Yanga eneo pembeni ya uwanja wa Taifa si ndio akili zenu zilipo. Mmejua Yanga watafanya kweli sasa mnakwamisha. Mueneo wote ule unaofuga mbu myuambie hapana nafasi!
 
Una uhakika kuwa hili : panatosha kufanya ujenzi, lakini Mr Mshana Jr anaona hapatoshi...heheheh

Yanga ni Yanga na Azam ni Azam...huko nje ya mji waache wafyeka vichaka Simba waende huko kusaka nyoka

Na ole wenu tukijenga uwanja wetu mje kung'oa viti kama mlivyozoea kung'oa visiki huko Bunju kama wang'oa kucha

Mkuu vijana wa Msomali hawa wanajifurahisha. Baada ya soka kuwashinda sasa wameamua wajikite kwenye mipasho..

Haya ya eneo halitoshi ni mbinu tu za huyo mpare kuikwamisha Yanga lkn akija kesho Mhindi pale anataka kujenga kiwanda cha khanga hutasikia eneo dogo, utajagutuka wakati wananchi wanalalama kiwanda kinatiririsha maji yenye kemikali kwenye makazi
 
Una uhakika kuwa hili ndilo dai kuu la malalamiko ya baraza la wazee wa Yanga?

Wahandisi ujenzi waliobobea katika kazi yao wameona panatosha kufanya ujenzi, lakini Mr Mshana Jr anaona hapatoshi...heheheh

Yanga ni Yanga na Azam ni Azam...huko nje ya mji waache wafyeka vichaka Simba waende huko kusaka nyoka

Na ole wenu tukijenga uwanja wetu mje kung'oa viti kama mlivyozoea kung'oa visiki huko Bunju kama wang'oa kucha
Hahahahahaaaa watu8 au 6+2 sikujua kaa wewe ni mtani jembe
 
Na ndiyo maana watapa kibali cha kujenga kiwanja pale jangwani na nyinyi mnaowakejeli kuwa wa kwanza kwenda uwanjani hapo.
Kwa taarifa yenu yanga ilipanga kujenga uwanja mzuri pale jangwani karibu miaka 30 iliyopita lakini tatizo kubwa ni kwamba migogoro ambayo imekuwa ikiathiri utendaji wake na viongozi wakitumia muda mwingi kulumbana/kugombana.
Abunuwasi my bro you must be kidding !!!miaka thelathini ya mipango lakini tatizo ni migogoro Omg !!!
 
Sema utakavyo lakini ukweli ni kwamba hivi sasa wanataka kujenga lakini kuna vikwazo vifuatavyo
1 eneo lao halitoshi
2. Sehemu ya eneo lao limevamiwa
3. Eneo wanaloliomba limekuwa ni la michezo tangu mwaka 1930's
4. Eneo lile halifai kwa makazi ila wao wameshafanya feasibility studies on how best to use the area in line with nemc
directives
5. petty politics ndiyo kikwazo kikubwa kwani ninauhakika kuwa yanga wakipewa eneo hilo hata simba watadai eneo lao
ambalo lipo na linajulikana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom