Goheki
JF-Expert Member
- Aug 23, 2011
- 448
- 387
Yanga Infrastructure Development Plan 2019
Ndugu yangu Jemedari Said Kazumari hebu acha kupotosha umma kwa taaluma isiyo yako.
Hebu ngoja tukuelimishe juu ya jambo hili ili records ziweze kukaa sawa kwako na wengine ambao wanaweza kupotosha kwa au kutokuelewa au kwa makusudi wanayojua wao.
1. Muongozo wa mahitaji ya uwanja wa mechi unatolewa na FIFA kupitia muongozo unaoitwa; FIFA Football; Technical Recommendations and Requirements; Mahitaji ya Uwanja wenye uwezo wa kubeba Mashabiki 20,000 au 30,000 unahitaji eneo la ardhi lenye zaidi ya hekari 10. Hivyo basi hekari 7 za Yanga zilizopo Kigamboni kwa mujibu wa muongozo wa FIFA haziwezi kukidhi vigezo hivyo kwa uwanja wa mechi kama mawazo yako finyu yanavyotaka. Mfano je utajenga uwanja bila maegesho (parking) pamoja na huduma nyingine muhimu za jamii?
Je utajenga Uwanja wa mechi bila majukwaa?;
2. Mwaka 2019/20 klabu ya Yanga kupitia Kamati ya Ujenzi na Miundombinu ambayo Rais wa Sasa wa Yanga Eng. Hersi Ally Said alikuwa ni mjumbe kwenye Kamati hiyo tena kwa TAALUMA YAKE YA KIHANDISI waliandaa Mkakati Kabambe wa uendelezaji wa Miundombinu ya klabu ya Yanga ulioitwa; Yanga Infrastructure Development Plan;
3. Ndani ya mkakati huo; kulikuwa na mkakati wa muda mrefu ambao ulikuwa ni kujenga uwanja wa mechi eneo la Jangwani;
Mkakati wa muda wa Kati ulikuwa ni kujenga kituo cha mazoezi na hostel za wachezaji eneo la Kigamboni; na zabuni iliyowahi kutangazwa wakati huo ilikuwa ni kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa hostel na uwanja wa mazoezi. Sasa wewe Jemedari Said Kazumari kwanini unapotosha umma kuwa Yanga walitaka kujenga uwanja wa mechi Kigamboni?
Hivi unapotosha umma kwa lengo lipi na faida ipi?
4. Mkakati wa muda mfupi ulikuwa ni kukarabati jengo la Yanga pale Makao Makuu ya Klabu mtaa wa Twiga na Jangwani kwa kujenga duka la kuuzia jezi la klabu;
5. Hivyo basi Eng. Hersi Ally Said kwa taaluma yale na wadhifa wake kama Rais wa Klabu anaposimama mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mh. Samia Suluhu Hasani) kuomba eneo la nyongeza litakalokidhi mahitaji kwa Viwango vya FIFA pale Jangwani hupo sawa kabisa kwasababu anajua kwa mujibu wa mahitaji ya uwanja wa mechi kwa viwango vya FIFA na ili uwanja uruhusiwe kutumika kwenye mashindano ya kimataifa kama AFCON ni lazima hekari ziwe zaidi ya 12 na kuendelea ili kukidhi mahitaji yao. Wewe Jemedari Said Kazumari unampinga Rais wa Klabu ya Yanga ambaye Kitaaluma ni Mhandisi nawe ni Mchambuzi sina uhakika kwa taaluma au la unawezaje kumkosoa wakati wewe wala sio fundi mchundo? Jikite na kutoa taarifa sahihi kwa umma badala ya kupotosha braza na kuacha taaluma zitamalaki.
6. Rais wa Yanga, Eng. Hersi Ally Said sio tu kuwa ameomba eneo ila ameelezea kwa ufasaha kuwa ndoto ya Hayati Mzee Abeid Aman Karume na waasisi wengine wa klabu ya Yanga ndoto yao ilikuwa ni kuona Jangwani kunakuwa na uwanja wa kisasa. Hivyo basi yeye akiwa kama Rais wa Klabu kijana anawiwa kusimamia ndoto hiyo leo ili kukamilisha maono ya wazee wetu. Sasa wewe Jemedari Said Kazumari unaposema hakuna haja ya Yanga kuongezewa eneo pale Jangwani unaongozwa na misingi ipi? Ya chuki au kufitinisha Yanga na Mamlaka za nchi? Acha kuingiza masuala yaliyo nje ya uwezo wa taaluma yako kaka.
7. Eneo la Jangwani lilipo ni eneo la kimkakati ambalo lipo kwenye lCentral Business District (CBD) hivyo basi kupitia mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) au Mwendokasi ni eneo linalofikika kirahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam. Hivyo basi unaweza kujenga uwanja na mechi kupangwa muda wowote hata usiku. Kitendo cha kujenga Uwanja pale ni mradi utakaolipa kwenye uwekezaji. Eneo la Kigamboni ilivyokaa ni eneo lenye utulivu hivyo panafaa kubaki kwa mipango ya hostel;
8. Wananchi tuachane na porojo za Jemedari Said Kazumari kwasababu hazina mantiki, hazina muktadha wala hazina nia njema. Ni habari za upotoshaji zenye kulenga kujenga uhasama na mtafaruku tu huenda kwa utashi wake au maelekezo ya anaowajua yeye.
9. Wananchi tuungane na uongozi wetu chini ya Rais wa Klabu yetu kwenda mbele pamoja. Tusimame na uongozi wetu tupuuze Upotoshaji wa huyu Bwana ambaye hadi natoa elimu hii hata sijui kabisa huyu mtu Klabu ya Yanga ilimkosea nini.
10. Daima Mbele, Nyuma Mwiko