Yanga 3- Ruvu Shooting 2: Ni Kweli Golikipa Metacha B.Mnata anahisiwa kuwa mzembe ama kutumika "kuiuza" timu?

Metacha ni kipa mzuri Ila tatizo haikua siku mzuri kwake ata De Gea ua anapata shutma akifanya makosa. Ukicheza timu kubwa Kama Yanga unatakiwa mchezaji uweze kuhimili presha. Ingekua timu ndogo Wala isingekua ishu.
 
Metacha hastahili lawama yeyote ni timing tu pale ambapo goal kipa yeyote anaweza kufungwa aina ile ya goal.
Daah utalaumiwa kwa hili lakini ndo hivyo na wendako Yanga

Hasa goli la kwanza cheki bunduki ilivyopigwa na ikaenda pembeni.
 
Kafungwa magoli ya kipuuzi afu anatukana mashabiki! Hakana akili kale ka jamaa!
 
Hii issue ya Metacha imekuwa bias kdg kwa kweli... Watu wanatazama matokea ila hawatazami chanzo..
Kwanini Metacha kaonyesha ile gesture kwa mashabiki? Why aangushiwe jumba bovu katika ukubwa huo bila kutazama mazingira husika?

Inakuwa kama alikuwa anawekewa mtego ateleze ahukumiwe wkt sio sahihi na inaeleweka vyema mpira ni mchezo wa makosa na ukimtafutia mtu kosa uwanjani lazima utamdaka tu.

He made a mistake kweli kama mchezaji lakini sio yeye wa kwanza kufungwa vile na pia sio kwa kwanza au pekee anaefanya makosa uwanjani pindi timu inapocheza.

Mashabiki walianza kumpa pressure akiwa bado yupo uwanjani na matusi kedekede. Je uongozi umelitazama hilo au umeamua tu kuhukumu upande mmoja kishabiki?

Wanaosema Metacha duka je hao makipa wengine hawafungwi? How many good saves Metacha kafanya akiwa ndani ya Jezi ya Yanga walisema ni duka? nadhani wengi alizisifia saves zake na mpaka kufanya aitwe Timu ya Taifa..

Mpira wetu tukiendekeza ushabiki zaidi mpaka kwenye level ya Uongozi tutakuwa tunawaua sana vijana wetu kwa utashi wetu wenyewe.. I feel sorry for him.
 
Hawa Yanga ni noma. Mara mnasema Karia anaihujumu Yanga, Sasa mmehamia kwa Metacha.

Yale magoli mbona hata Manula huwa anapopolewa tu.
 
Nawapongeza Ruvu shooting wazee wa pira papaso, wamempapasa Metacha , goli zile wanafungwa hata huko duniani
 
Issue iko kwenye meza ya maamuzi na hasa ya kinidhamu ya klabu ya YANGA,...Je maamuzi yao yalipata nafasi ya kujadiliwa uongozi (wanaohusika ndani ya klabu) na kuona inafaa kuchukua hatua waliyochukua dhidi ya Metacha (sipingani na adhabu,concern yangu ni Muda toka tukio limetokea hadi maamuzi yanatolewa...walikaa saa ngapi? Au ni kauli ya mtu mmoja?) Na je tunafanya maamuzi kufurahisha na kuwaridhisha washabiki au ni msingi wa kikanuni za klabu?
 
Issue iko kwenye meza ya maamuzi na hasa ya kinidhamu ya klabu ya YANGA,...Je maamuzi yao yalipata nafasi ya kujadiliwa uongozi (wanaohusika ndani ya klabu) na kuona inafaa kuchukua hatua waliyochukua dhidi ya Metacha (sipingani na adhabu,concern yangu ni Muda toka tukio limetokea hadi maamuzi yanatolewa...walikaa saa ngapi? Au ni kauli ya mtu mmoja?) Na je tunafanya maamuzi kufurahisha na kuwaridhisha washabiki au ni msingi wa kikanuni za klabu?
Umeongea KIWELEDI sana......

Bumbuli APITE hapa na kusoma ujumbe wako.....

Ni lazima tuendeshe soka letu "kiprofesheno" zaidi ya mihemko....
 
La pili aliruka kaona ataupata mpiraa akairudisha mikono nyuma...

Metacha ni pandikizi
 
Back
Top Bottom