RubbishDonald Trump ameamua kujitangaza mshindi wa uchaguzi wa Marekani wakati kura bado zinahesabiwa na ametangaza anenda mahakamani kupinga matokeo.
Kwa taifa ambalo wapinzani kama ACT Wazalendo na CHADEMA huwa wanalitegemea kuwa kioo cha Demokrasia sasa linatia aibu maana kama mtu anakataa matokeo ambayo hata mwisho wa kuhesabu bado, hapa picha inayoonekana ni kutokubali kushindwa kama wapinzani wa Tanzania walivyofanya.
Mpaka sasa Electoral votes ni 238 kwa Joe Bidden huku Trump akiwa na 213.
Jambo la msingi ni kuwa kumbe uchaguzi wa Tanzania ulifanyika kwa uhuru na haki lakini wapinzani hawakubali matokeo. Na pamoja kuwa ni nchi ya Kiafrika tunaanza kukomaa kidemokrasia maana habari kama za Maalim kujitangaza mshindi hatukuziona tena.
Hivi mkuu kwamba wenzetu ni tofauti kabisa na sisi waTanzania?Hizi taarifa ni janga pale mitaa ya Ufipa na Kigoma Mjini.
Trump anamtuma Balozi wake aingilie uchaguzi wa Tanzania wakati yeye mwenyewe siyo msafi.
Ni aibu
Kumbuka hapa kwetu Rais analindwa kwa kila namna asalie madarakani na vyombo vya dola tofauti na wenzetu huko vyombo vya dola hujiweka pembeni na mambo ya siasa nakuheshimu sanduku la kura.Du! Mahela wa U.S keshamfanya vibaya Trump
Yes, hiyo ndo democracy sio hapa kwetu vyombo vya dola vinaacha majukumu yake ya kikatiba badala yake vinatumiwa kuibakisha serikali madarakani kwa kila namna.Nilichojifunza ni kuwa USA tume yao ya uchaguzi haiko mfukoni mwa Rais!Ukiona mpaka Rais aliye madarakani analialia basi ujue mfumo wa USA ni baab kubwa!Hatumikiwi mtu kisa yeye ni Rais!Pia ukiangalia vyombo kama FBI viko independent,Rais anabaki na secret service!Na hao Secret service,chief wao akipata notice tu kutoka kwa AG basi mara moja wanaacha kuchukua orders kutoka kwake!Wanamweka chini ya ulinzi,hapa nazungumzia kama amefanya mambo ya hovyo na AG wao akaona kuna haja ya kumwajibisha!
Yaani mfumo wao hadi raha,kiongozi hawezi kukengeuka kuwa Mungu mtu!
Hapana sijajiingiza mkenge.Hivi mkuu kwamba wenzetu ni tofauti kabisa na sisi waTanzania?
Trump ni amiri jeshi ana kila kitu na sauti lakini polisi, wanajeshi, usalama wa taifa nakadhalika hujiweka mbali na siasa hakuna kumsaidia aliyepo madarakani eti kisa ni kiongozi wao.
Hapa kwetu tumeshuhudia polisi, na vyombo vingine vya dola vikishiriki kuhujumu maamuzi ya wananchi kisa kulinda kibarua cha boss wao aendelee kusalia.
Sasa hapo mitaa ya ufipa na kigoma wanahusikaje huoni unajiingiza mkenge mwenyewe?
Hivi unajielewa kweli? Huoni kwamba Rais wa marekan hawana control yoyote na mfumowa uchaguzi? Rais aliye madarakani analalamika tume haifanyi kazi yake vizuri. Wenzetu kuwa madaraka i sio quarantee ya kutangazwa. Yaani yeye hana uwezo wakuwafukuza mawakala kwenye vituo, anakuwa sawa. na mpinzani.Donald Trump ameamua kujitangaza mshindi wa uchaguzi wa Marekani wakati kura bado zinahesabiwa na ametangaza anenda mahakamani kupinga matokeo.