Yanayotokea USA ni dhahiri kuwa Tanzania tumekomaa kidemokrasia

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
1,773
2,000
Donald Trump ameamua kujitangaza mshindi wa uchaguzi wa Marekani wakati kura bado zinahesabiwa na ametangaza anenda mahakamani kupinga matokeo.

Kwa taifa ambalo wapinzani kama ACT Wazalendo na CHADEMA huwa wanalitegemea kuwa kioo cha Demokrasia sasa linatia aibu maana kama mtu anakataa matokeo ambayo hata mwisho wa kuhesabu bado, hapa picha inayoonekana ni kutokubali kushindwa kama wapinzani wa Tanzania walivyofanya.

Mpaka sasa Electoral votes ni 238 kwa Joe Bidden huku Trump akiwa na 213.

Jambo la msingi ni kuwa kumbe uchaguzi wa Tanzania ulifanyika kwa uhuru na haki lakini wapinzani hawakubali matokeo. Na pamoja kuwa ni nchi ya Kiafrika tunaanza kukomaa kidemokrasia maana habari kama za Maalim kujitangaza mshindi hatukuziona tena.
 
Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,783
2,000
Tume ipindue meza kama vipi.

Mwaka 2015 kule Zanzibar, babu madevu(kwa mjibu wa Polepole), alijitangazia ushindi na ndipo Jecha akaingilia Kati kwa kufuta matokeo.
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
13,549
2,000
Ninaamini hata nchi fulani kama wangefuata haki ya ballots boxes kuna mbabe angetoka kujitangazia ushindi na kupoka maboxes yote na kukimbia. Ninaamini ndivyo iliyokuwa.
 
  • Thanks
Reactions: cmp

Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,279
2,000
Hizi taarifa ni janga pale mitaa ya Ufipa na Kigoma Mjini.

Trump anamtuma Balozi wake aingilie uchaguzi wa Tanzania wakati yeye mwenyewe siyo msafi.

Ni aibu
 
MTOTO WA KUKU

JF-Expert Member
May 3, 2012
2,573
2,000
Usijiongopee wizi uliofanyika hapa kwetu tena waziwazi huwezi fananisha na ndugu zake mungu(wazungu)....sisi labda baada ya miaka 20000 ijayo tunaweza kuikaribia
 
  • Thanks
Reactions: cmp

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
9,652
2,000
Donald Trump ameamua kujitangaza mshindi wa uchaguzi wa Marekani wakati kura bado zinahesabiwa na ametangaza anenda mahakamani kupinga matokeo.

Kwa taifa ambalo wapinzani kama ACT Wazalendo na CHADEMA huwa wanalitegemea kuwa kioo cha Demokrasia sasa linatia aibu maana kama mtu anakataa matokeo ambayo hata mwisho wa kuhesabu bado, hapa picha inayoonekana ni kutokubali kushindwa kama wapinzani wa Tanzania walivyofanya.

Mpaka sasa Electoral votes ni 238 kwa Joe Bidden huku Trump akiwa na 213.

Jambo la msingi ni kuwa kumbe uchaguzi wa Tanzania ulifanyika kwa uhuru na haki lakini wapinzani hawakubali matokeo. Na pamoja kuwa ni nchi ya Kiafrika tunaanza kukomaa kidemokrasia maana habari kama za Maalim kujitangaza mshindi hatukuziona tena.
Rubbish
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,632
2,000
Hizi taarifa ni janga pale mitaa ya Ufipa na Kigoma Mjini.

Trump anamtuma Balozi wake aingilie uchaguzi wa Tanzania wakati yeye mwenyewe siyo msafi.

Ni aibu
Hivi mkuu kwamba wenzetu ni tofauti kabisa na sisi waTanzania?

Trump ni amiri jeshi ana kila kitu na sauti lakini polisi, wanajeshi, usalama wa taifa nakadhalika hujiweka mbali na siasa hakuna kumsaidia aliyepo madarakani eti kisa ni kiongozi wao.

Hapa kwetu tumeshuhudia polisi, na vyombo vingine vya dola vikishiriki kuhujumu maamuzi ya wananchi kisa kulinda kibarua cha boss wao aendelee kusalia.

Sasa hapo mitaa ya ufipa na kigoma wanahusikaje huoni unajiingiza mkenge mwenyewe?
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,632
2,000
Du! Mahela wa U.S keshamfanya vibaya Trump
Kumbuka hapa kwetu Rais analindwa kwa kila namna asalie madarakani na vyombo vya dola tofauti na wenzetu huko vyombo vya dola hujiweka pembeni na mambo ya siasa nakuheshimu sanduku la kura.

Joe Biden hana polisi, jeshi wala vyombo vya dola lakini bado ameshinda na anayelia ni yule aliyepo madarakani.

Hiyo tu ni tofauti kubwa democracy ya kwetu na wenzetu.
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,632
2,000
Nilichojifunza ni kuwa USA tume yao ya uchaguzi haiko mfukoni mwa Rais!Ukiona mpaka Rais aliye madarakani analialia basi ujue mfumo wa USA ni baab kubwa!Hatumikiwi mtu kisa yeye ni Rais!Pia ukiangalia vyombo kama FBI viko independent,Rais anabaki na secret service!Na hao Secret service,chief wao akipata notice tu kutoka kwa AG basi mara moja wanaacha kuchukua orders kutoka kwake!Wanamweka chini ya ulinzi,hapa nazungumzia kama amefanya mambo ya hovyo na AG wao akaona kuna haja ya kumwajibisha!
Yaani mfumo wao hadi raha,kiongozi hawezi kukengeuka kuwa Mungu mtu!
Yes, hiyo ndo democracy sio hapa kwetu vyombo vya dola vinaacha majukumu yake ya kikatiba badala yake vinatumiwa kuibakisha serikali madarakani kwa kila namna.
 
Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,279
2,000
Hivi mkuu kwamba wenzetu ni tofauti kabisa na sisi waTanzania?

Trump ni amiri jeshi ana kila kitu na sauti lakini polisi, wanajeshi, usalama wa taifa nakadhalika hujiweka mbali na siasa hakuna kumsaidia aliyepo madarakani eti kisa ni kiongozi wao.

Hapa kwetu tumeshuhudia polisi, na vyombo vingine vya dola vikishiriki kuhujumu maamuzi ya wananchi kisa kulinda kibarua cha boss wao aendelee kusalia.

Sasa hapo mitaa ya ufipa na kigoma wanahusikaje huoni unajiingiza mkenge mwenyewe?
Hapana sijajiingiza mkenge.

Ninazungumza ukweli kwa sababu nafahamu oparesheni za siri zinazoendelea ndidi ya nchi za afrika hususani zinazoonyesha mwelekeo mzuri kwenye kujikwamua kiuchumi.

Tukubali kwamba kosa la wanasiasa wwtu wa upinzani nibkujiaminisha kuwa watapata msaada kutoka nje ili washinde madaraka ya nchi ilihali wanajaribu kuwatumia wapigakura kama daraja lisilo na umuhimu wowote.

Jenga ndani kwanza ili nje kuimarike.
Simama na nyumba yako kujenga heshima kwa jirani

Mkuu.
Marekani ameaibika nankuaibisha demokrasia feki aliyoijenga duniani.

Aje Afrika ajifunze demokrasia
 
crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
938
500
Donald Trump ameamua kujitangaza mshindi wa uchaguzi wa Marekani wakati kura bado zinahesabiwa na ametangaza anenda mahakamani kupinga matokeo.

Kwa taifa ambalo wapinzani kama ACT Wazalendo na CHADEMA huwa wanalitegemea kuwa kioo cha Demokrasia sasa linatia aibu maana kama mtu anakataa matokeo ambayo hata mwisho wa kuhesabu bado, hapa picha inayoonekana ni kutokubali kushindwa kama wapinzani wa Tanzania walivyofanya.

Mpaka sasa Electoral votes ni 238 kwa Joe Bidden huku Trump akiwa na 213.

Jambo la msingi ni kuwa kumbe uchaguzi wa Tanzania ulifanyika kwa uhuru na haki lakini wapinzani hawakubali matokeo. Na pamoja kuwa ni nchi ya Kiafrika tunaanza kukomaa kidemokrasia maana habari kama za Maalim kujitangaza mshindi hatukuziona tena.
Hivi unajielewa kweli? Huoni kwamba Rais wa marekan hawana control yoyote na mfumowa uchaguzi? Rais aliye madarakani analalamika tume haifanyi kazi yake vizuri. Wenzetu kuwa madaraka i sio quarantee ya kutangazwa. Yaani yeye hana uwezo wakuwafukuza mawakala kwenye vituo, anakuwa sawa. na mpinzani.
 
Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
5,204
2,000
Unaona wanaotuhumiwa kufanya faulu kule si tume wala state apparatuses, na wako radhi km kuna ishu mahakama ina-intervene. Vyumba vya kuhesabu kura wanaruhusu mawakawala, waandishi wa habari na wanasheria wa vyama kuwemo ndani.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom