101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,121
Wanachama na Wafuasi wa Chama cha Republican Nchini Marekani wamelalamikia uamuzi wa uliotolewa na Mahakama Kuu ya Colorado wa kuondoa jina la Rais wa zamani wa Nchi hiyo Donald Trump katika karatasi ya kura ya uchaguzi wa awali wa Republican unaotarajia kufanyika mwakani 2024
Mahakama hiyo imesema uamuzi huo ni kutokana na ushiriki wa Trump katika kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa Rais wa mwaka 2020
Uamuzi huo umesimamishwa baada ya kuwasilishwa kwa rufaa katika Mahakama ya Juu ya Marekani lakini haujazuia wengi ndani ya Chama hicho ikijumuisha baadhi ya wapinzani wa Rais huyo wa zamani kujadili uamuzi huo na kusema si wa Kidemokrasia na ni miongoni mwa majaribio ya kuondoa uamuzi wa kuchagua mgombea Urais wa Republican mikononi mwa wapiga kura
Kutokana na Trump kuwekewa pingamizi na zaidi ya dazeni ya majimbo, Mwenyekiti wa Republican Ronna McDaniel ametumia mtandao wa kijamii wa X (zamani ikijulikana kama Tweeter) kueleza kutokubaliana kwake na uamuzi huo na kudai ni kuingilia mambo ya uchaguzi wa ndani ya Chama cha Republican
Sent from my 21061119AG using JamiiForums mobile app