Yanayojiri Uzinduzi wa ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo. Serikali ya Oman, China & TZ wapo

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewathibitishia wakazi wa Bagamoyo kuwa wale wote watakaoguswa na mradi wa ujenzi wa bandari mpya watalipwa fidia na wengine watajengewa nyumba kwenye maeneo ya mji huo.

"Mradi huo ni mkubwa sana unaoshirikisha kampuni hii ya China Merchants Group, wawekezaji kutoka Oman ambao wataalamu wao pia wameshafika na Serikali ya Tanzania. Tunatarajia kuwa utaibadilisha Bagamoyo kwa kiasi kikubwa na kuufannya kuwa mji wa viwanda, hatua itakayovuta wawekezaji wengi zaidi na kuzalisha ajira nyingi," alisema.

Mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya awali ya maandalizi kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo, katika sherehe inayotarajiwa kuongozwana Rais Jakaya Kikwete leo.

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka jana, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi huo.

Eneo hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

Dk Turuka alisema mradi huo pia utahusisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, umeme, gesi na mitandao ya mawasiliano.

Mradi huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.

Kwa mujibu wa Dk Turuka, wazo la kuwepo mradi huo, limetokana na uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza ajira nchini.

mwaka 2008, Rais Kikwete alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na kuafikiana kujenga bandari hiyo.

Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.

Wengine wanoatarajiwa kuhudhuria ni wanadiplomasia na ujumbe kutoka kwa Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo

Tutawaletea live coverage ya uzinduzi wa ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Bagamoyo viongozi wa Serikali ya Oman, Serikali ya China wakuuu wa serikali, raisi Jakaya Kikwete, Mh Sitta, Waziri mkuu na Mkuu wa Wilaya Bagamoyo, watakuwepo zoezi la uwekaji jiwe la msingi.

Raisi Jakaya Kikwete kuweka jiwe la msingi.
BAG1.jpg


View attachment Preparatory Survey Report for Grant Aid Project.pdf
 
Hiyo bandari haitakuwa beneficial kwetu kama nchi zaidi ya jina la bandari....
Hadi hao wamalize pata hela ya uwekezaji wao JK atakuwa kashakufa, sote tutakuwa tumekufa
 
Week naona mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu Tazara na huyo ujenzi wa Bandari Bagamoyo vinafanyika. Isije kuwa siasa, kasi ya utekelezaji ni bora ikaendelea hata baada ya uchaguzi kwisha.
 
Hiyo bandari hata kiuchumi haitakuwa productive... Tunapaswa kuiimarisha bandari ya Dar hata iwe na gati 20 kuliko kuingia garama nyingine kubwa za kujenga bandari mpya. Upuuzi mtupu iyo bandari ya Bagamoyo.
 
Hiyo bandari haitakuwa beneficial kwetu kama nchi zaidi ya jina la bandari....
Hadi hao wamalize pata hela ya uwekezaji wao JK atakuwa kashakufa, sote tutakuwa tumekufa
Haiwezi kuwa beneficial maana Mchina ata operate miaka 100, huku wakiendelea kuiba mali ghafi zetu.
 
JK anaiuza nchi Taratibu sana
Ninachojua ni kuwa wangewekeza kwenye bandari ya Tanga ili mizigo ya kaskazini ipitie huko....
Bandari ya Dar pia irekebishwe zaidi
Mtwara pia itengenezwe zaidi
Afrika tuna safari ndefu ya kuendelea. Bila shaka ungekuwepo miaka ya 1970 ungelisema hivihivi juu ya ujenzi wa TAZARA
 
BAHARI:
1.Bandari ya Dar Es Salaam
2.Bandari ya Tanga
3.Bandari ya Mtwara.
4.Bandari ya ....

ZIWA VICTORIA:
1. Musoma
2.Mwanza.
3.Bukoba
4. ....
Hizi bandari zoote hazina utendaji yakinifu wa katika upakiaji na usafirishaji wa mizigo, labda kidooogo bandari ya hapo Dar, sasa kuanzisha mradi mkubwa kama huo wa bagamoyo maana yake (imejificha wapi) ni nini makusudi?
 
Afrika tuna safari ndefu ya kuendelea. Bila shaka ungekuwepo miaka ya 1970 ungelisema hivihivi juu ya ujenzi wa TAZARA

Tanga, Dar zinatosha sana bora serikali ingewekeza hela kwenye hizo mbili kabla ya kukimbilia kuwapa wachina eneo
 
uzinduzi umepamba moto mwezi huu...mabasi ya mwendo kasi yaliyozinduliwa yako wapi???
 
Hiyo bandari haitakuwa beneficial kwetu kama nchi zaidi ya jina la bandari....Hadi hao wamalize pata hela ya uwekezaji wao JK atakuwa kashakufa, sote tutakuwa tumekufa
Watoto wako na wajukuu wako watafaidi. Siyo lazima ufaidi wewe, jifunze kuandaa mazingira mazuri ya watoto wako na wajukuu. Acha kuwa selfish.
 
Back
Top Bottom