Yanayojiri uwanja wa vita Israel Vs Palestine, taarifa za hivi punde

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
HABARI ZA MOJA KWA MOJA KUTOKA MEDANI YA KIVITA TEL AVIV NA GAZA PALESTINE

4084f470-7874-4c49-a57a-3467578fcb85.jpg

Kombora likilipuka eneo la Gaza usiku wa jumapili

09 Oct 2023
Wakuu heshima kwenu.
Habari Za hivi punde kutoka uwanja wa kivita zinadokeza kuwa watu 700 wameuliwa upende wa Israeli huku watu 400 wakithibitika kuuliwa upande wa Palestine. Hospitali za mjini Gaza zimefurika maelefu ya majeruhi. Mpaka kufikia asubuhi ya Leo tayari zaidi ya wapalestina laki moja wamekimbia makazi yao.

KUTOKA TEHRAN HIVI LEO
Iran "haikuhusika" katika shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa Hamas kusini mwa Israel, ujumbe wake katika Umoja wa Mataifa umesema.

"Tunasimama kwa nguvu katika kuunga mkono Palestina; hata hivyo, hatuhusiki katika shambulio la Palestina, kwani linatekelezwa na Palestina yenyewe," ilisema katika taarifa ya Jumapili, kulingana na Reuters

MELI YA KIVITA KUTOKA MAREKANI IMEWASILI KARIBU NA ISRAELI LEO
c5b63200-fc0b-441a-9797-a03bc9af7733.jpg

Meli ya kubeba ndege ya USS Gerald R. Ford inaelekea eneo hiloImage caption:

Marekani inasema inahamisha shehena ya ndege, meli na jeti hadi mashariki mwa Mediterania na pia itaipa Israel vifaa na risasi zaidi.

Hii inafuatia shambulio la Hamas kusini mwa Israel, ambalo Rais Biden aliliita "shambulio lisilokuwa na kifani na la kutisha".

Marekani pia ilikuwa ikifanya kazi ya kuthibitisha ripoti kwamba raia wake walikuwa miongoni mwa waliouawa na kuchukuliwa mateka, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amesema.

Israel inasema zaidi ya watu 700 wameuawa na 100 kutekwa nyara.

Mjini Gaza, zaidi ya watu 400 wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi ya Israel, kulingana na maafisa wa Palestina.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alisema meli ya kubeba ndege ya USS Gerald R. Ford, meli ya kubebea makombora na zana za kuharibu makombora vimepelekwa katika eneo hilo. Ndege za kivita za Marekani pia zinapelekwa Gaza.

Misaada zaidi ya kijeshi kwa Israel itatumwa katika siku zijazo, Ikulu ya White House ilisema.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi ameeleza kuunga mkono shambulio la Hamas akisema Israel inapaswa kuwajibika kwa kuhatarisha eneo hilo.
October 11, 2023

Hali ya kibinadamu ya Gaza inazidi kuwa mbaya, huku Israel ikitarajiwa kuanza mashambulizi ya ardhini​

Huku Gaza sasa ikiwa imezingirwa kikamilifu na wanajeshi wa Israel na baada ya siku tano za mashambulizi ya mabomu, hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya.
Umeme ulikatika leo baada ya kituo pekee cha umeme katika eneo hilo kukosa mafuta. Hospitali, ambazo zimejaa maelfu ya majeruhi, zinasema zinakosa dawa.
Umoja wa Mataifa unasema watu nusu milioni wa Gaza hawajapata mgao wao wa chakula tangu Jumamosi. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuanzishwa eneo la kibinadamu. Afisa mmoja wa Misri aliiambia BBC kwamba serikali mjini Cairo ilikuwa katika majadiliano na pande zote kujaribu kuruhusu msaada kuingia Gaza kupitia Misri hata kama ni kwa saa chache tu.
Wakati huo huo, kuna matarajio makubwa kwamba Israel hivi karibuni itaimarisha zaidi operesheni yake kwa mashambulizi ya ardhini.
Msemaji wa Israel alisema vikosi, ikiwa ni pamoja na askari wa akiba 300,000, walikuwa karibu na mpaka wakijitayarisha kwa kwa mashambulizi, ili kuhakikisha kwamba kunakuwa na "mwisho wa vita hivi Hamas hawana tena uwezo wowote wa kijeshi".
Kwa idadi ya watu waliouawa na Hamas mwishoni mwa juma ambayo sasa inajulikana kuwa zaidi ya 1,200, ujumbe huo utakuwa na uungwaji mkono mkubwa wa umma wa Israeli
 
HABARI ZA MOJA KWA MOJA KUTOKA MEDANI YA KIVITA TEL AVIV NA GAZA PALESTINE

View attachment 2776340
Kombora likilipuka eneo la Gaza usiku wa jumapili

09 Oct 2023
Wakuu heshima kwenu.
Habari Za hivi punde kutoka uwanja wa kivita zinadokeza kuwa watu 700 wameuliwa upende wa Israeli huku watu 400 wakithibitika kuuliwa upande wa Palestine. Hospitali za mjini Gaza zimefurika maelefu ya majeruhi. Mpaka kufikia asubuhi ya Leo tayari zaidi ya wapalestina laki moja wamekimbia makazi yao.

KUTOKA TEHRAN HIVI LEO
Iran "haikuhusika" katika shambulio lililotekelezwa na wanamgambo wa Hamas kusini mwa Israel, ujumbe wake katika Umoja wa Mataifa umesema.

"Tunasimama kwa nguvu katika kuunga mkono Palestina; hata hivyo, hatuhusiki katika shambulio la Palestina, kwani linatekelezwa na Palestina yenyewe," ilisema katika taarifa ya Jumapili, kulingana na Reuters
Aache uoga, hii vita itafika hadi kwake safari hii.
 
Upande wa Israel vifo vimesha fika 1000
 
Upande wa Israel vifo vimesha fika 1000
Lazima vitazidi. Hao wanaongezeka ni wale majeruhi zaidi ya 2,000, maana kuna wale waliokutwa kwenye tamasha la muziki kule vilimani mpakani, on the spot walidondoshwa watu zaidi ya 200, majeruhi wakawa wengi zaidi.
Ilikua ni siku ya mapumziko, watu walikua wamepumzika majumbani na familia zao, wengine wakiwa wametembeleana, mitaa ikiwa kimya, wakajikuta wanapigwa ambushi na kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya. So death toll lazima iongezeke.
 
Lazima vitazidi. Hao wanaongezeka ni wale majeruhi zaidi ya 2,000, maana kuna wale waliokutwa kwenye tamasha la muziki kule vilimani mpakana, on the spot walidondoshwa watu zaidi ya 200.
Ilikua ni siku ya mapumziko, watu walikua wamepumzika majumbani na familia zao, wengine wakiwa wametembeleana, mitaa ikiwa kimya, wakajikuta wanapigwa ambushi na kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya. So death toll lazima iongezeke.
Aisee! Kama Hamas waliua raia, ina maana wametoa tiketi ya Israel kuua raia pia?
 
Huwa tunaikuza sn israel hila bila misaada na mikopo hata mishahara ya wafanyakazi itawashinda sasa km battle na hamas wameomba msaada halafu ndio huwa wanataka kushambulia iran
Unafikiria kwa kutumia ubongo ama unatumia Lokasa ya mbongo, hao matajiri wanaoshikiria uchumi wa USA ni Jews. Hii mijamaa inamiliki technology ni mitajiri haswaaa, ipo katika jangwa ila ni hodari kwenye kilimo.
 
Aisee! Kama Hamas waliua raia, ina maana wametoa tiketi ya Israel kuua raia pia?
Vifo vinavyo ripotiwa kutokea gaza ni maiti zikizopatikana, kumbuka kuna nyumba, mahorofa na misikiti vimeshushwa vizima kama vilivyo na vimebaki vifusi na hakuna uokozi unaoendelea. Siku ya kuja kuvufukia ndiyo namba ya waliofarika itapatikana.

Hali ni tete na mbaya sana, huko Israel nao jeshi limetanda mtaani likiendelea kufagia, raia wa Israel nao wameungana na jeshi kutafuta hamasi na sasa raia hata wakiona Mpalestina hawamuachi.

Hapa Hamas wamewekwa guard

Huwa tunaikuza sn israel hila bila misaada na mikopo hata mishahara ya wafanyakazi itawashinda sasa km battle na hamas wameomba msaada halafu ndio huwa wanataka kushambulia iran
Akili za CCM hizi jamani, mnaikuza Israel na nani? ebu tuwekee hapa GDP yao tulinganishe na yetu
 
Back
Top Bottom