MmasaiHalisi
Senior Member
- Jan 15, 2009
- 192
- 23
kuna ndugu zetu huko hatuna raha mtujuze,ccm wameamua kuua ila mwisho wao unakaribia
kuna ndugu zetu huko hatuna raha mtujuze,ccm wameamua kuua ila mwisho wao unakaribia
Nilijaribu kufuatilia mambo yaliyojiri huko shinyanga ambapo inasemekana kuwa Chadema wameshinda bali mheshimiwa akawaambia wabadili matokeo ndipo mgombea wa CCM alipotangazwa kiasi ambacho kimesababisha vurugu jengo la Manispaa nasikia limechomwa moto
...Ila tushukuru mungu anazidi kutuonyesha aina ya viongozi tulionao..Mwakilishi wa NEC Mkoani hapa huenda akajiuzulu.
Na bado wali beep tu. HawajapigaFracas za Shinyanga mjini ni tip of iceberg.
Ujumbe:huwezi kudanganya watu milele.
Watu wa CHADEMA walipoenda ofisini kwake kudai atangaze matokeo...akasema mgombea wa CHADEMA Kashinda..Baadae wa CCM alivyoenda akawaambia wa CCM Kashinda tena kwa tofauti ya Kura Moja.. Kisha akatoka na kufunga Ofisi....
Nina mashaka sana na habari yako mkuu. Labda nina matatizo. Kwamba, mwanzo kabisa alikuwa peke yake ofisini and then wagombea/wafuasi wa CHADEMA na CCM wakawa wanamfuata kila mtu kwa wakati wake!??
Na Wananchi wengi wa Shinyanga Mjini HAWAMTAKI Mbunge mteule bwana Stephen, Na inasemekana Ametishiwa kuwa akionekana mitaani watamfanyia Kitu Mbaya.... Ni Hasira ...Chuki ...dhidi ya DHULUMA!
Zitaisha na kutulia. Tufanye kazi tupate mlo wetu wa kila siku. Tuachane na wanasiasa wapige domo wao wanalipwa wakati sisi tunaacha kazi zetu za kila siku za kutafuta mkate wetu na familia zetu