Yanayojiri Bungeni leo Tarehe 26 May 2014

Peter jaluo

JF-Expert Member
Nov 10, 2013
1,751
1,195
leo ni bunge la 1o mkutano wa 15 kikao cha 18. Waziri wa uchukuzi aliwasilisha hotuba ya Bajeti ya makadilio na matumizi katika wizara ya uchukuzi ya mwaka wa fedha 2014-2015 na majadiliano yanaendelea.

katika maswali na majibu, Jamani huyu waziri AGrey mwanri .huyu waziri anawajibu wabunge wezake.kwa ukali sana.unafikiri kalazimishwa kujibu maswali hayo.
 

mmaranguoriginal.

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,058
1,195
Wadau, kwa wabunge wanaoibana kisawa sawa SERIKALI YA CCM kwa matamko mazito na makali ni huyu tundu lisu wa chadema na kangi lugola wa ccm ,nataka tujadili nani anajua kujenga hoja kati ya hawa mafahali wawili toka vyama tofauti.karibuni
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,080
2,000
Wewe unamjua Lissu? yaani akiongea Lissu tu bunge zima linachanganyikiwa baada ya hapo kila mtu (mbunge) anam-refer yeye tu.
 

duchi

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,766
0
Wadau, kwa wabunge wanaoibana kisawa sawa SERIKALI YA CCM kwa matamko mazito na makali ni huyu tundu lisu wa chadema na kangi lugola wa ccm ,nataka tujadili nani anajua kujenga hoja kati ya hawa mafahali wawili toka vyama tofauti.karibuni
Wote ni pasua kichwa hawana cha maana

 

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,635
2,000
Hivi ni kweli Mbunge anaoamba laki tano kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo? Si wanapewaga hela kibao siuji 20 m. Sasa laki tano za nini. Ni aibu sana kwa viongozi uchwara kama hawa kjifanya matonya kila mahali ilhali wanalipwa fedha nyingi sana. Wajue hiyo mifuko imechoka na mabakuli yao ndio maana wametoa data kwa upinzani. Shameful
 

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,264
2,000
Hii ni kauli ya Hawa Ghasia leo ndani ya Bunge.....


Sasa kama kweli itaundwa kamati ya bunge kufuatilia jinsi mifuko ya jamii inavyoliwa kiharamu na viongozi basi pasipo shaka tutaona jinsi Ramadhani Dau alivyonunua cheo chake kwa kutoa fedha zetu nyingi kwa NGO ya mke wa mkulu iitwayo WAMA!!! Ili kula fedha za NSSF vizuri wakampa Dau kuwa mjumbe wa bodi ya WAMA; huu ni ufisadi wa hali ya juu.
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Moses Machali ashindwa kutamka UHOLANZI badala yake ametamka ULANZI. Hawa UKAWA wanawaza kulewa tu
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Sasa kama kweli itaundwa kamati ya bunge kufuatilia jinsi mifuko ya jamii inavyoliwa kiharamu na viongozi basi pasipo shaka tutaona jinsi Ramadhani Dau alivyonunua cheo chake kwa kutoa fedha zetu nyingi kwa NGO ya mke wa mkulu iitwayo WAMA!!! Ili kula fedha za NSSF vizuri wakampa Dau kuwa mjumbe wa bodi ya WAMA; huu ni ufisadi wa hali ya juu.
Umesahau kuwa hata NGO ya Mchumba wa Dr Slaa iitwayo INGETA imepewa kiasi kikubwa na NSSF
 

Kilala Makusaro

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
688
500
Wote ni pasua kichwa hawana cha maana
y
[/QUOeTE]

Acha kuweweseka intarahamwe. Hivi ni vilima viwili ila Lugola ni mlimameru na Lisu ni kilimanjaro. Inaelekea ccm wamechanganyikiwa. Nimesikia Komba akikana, Luykuvi na Kabaka wakikiri na Hawa akaja kuhamisha hoja kwenda kwa Mbowe. Hoja iliyoletwa ni kuomba omba si kukopa maana wakopaji ni wengi na sheria inasema ukikopa unaweka rehani mali zako na ukishidwa kulipa zinakatwa. Hoja ya kuomba omba inakufanya uwe na haya kumuwajibisha mfadhili wako, hii ndio hoja kuu ya Lisu na hakuna aliyejibu hoja hiyo. Hii imefanya muongozo aliomba kuwa mwiba tena kwao.
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,551
2,000
Umesahau kuwa hata NGO ya Mchumba wa Dr Slaa iitwayo INGETA imepewa kiasi kikubwa na NSSF

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana amewalipua baadhi ya mawaziri na wabunge kwa kugeuka ombaomba katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Akizungumza bungeni jana katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa mwaka 2014/15, Lissu alisema kuwa atawasilisha hoja binafsi katika Ofisi ya Spika ili iundwe tume kwa ajili ya kuwachunguza wabunge na mawaziri hao.

Huku akionyesha baadhi ya nyaraka ambazo wabunge hao wameiandikia mifuko hiyo ya jamii kuomba fedha, Lissu alisema kitendo hicho kimewafanya viongozi hao kusifia kila jambo linalofanywa na mifuko hiyo, hata kama ni baya.

Lissu alitoa kauli hiyo huku wabunge watano kati ya wanane waliomtangulia kuchangia mjadala huo, kuisifia mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, huku wakimtaja kwa jina Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau kwamba ni mfano wa kuigwa.

"Sifa hizi zina sababu yake. Kuna nyaraka na barua zinazoonyesha wabunge mbalimbali waliochukua fedha za mifuko hii kwa sababu mbalimbali," alisema Lissu na kuongeza;

"Naomba baadaye Bunge liunde kamati teule ili kuichunguza mifuko hii na viongozi hawa."

Hata hivyo, Lissu hakumalizia hoja yake hiyo baada ya muda wake wa kuchangia kumalizika na kutakiwa kukaa chini na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu.

Wahusika

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho cha Bunge, Lissu alilionyesha gazeti hili nyaraka za vigogo hao zikionyesha wote wameomba kati ya Sh500,000 hadi Sh10 milioni.

Kati yao wapo mawaziri, naibu mawaziri ambao wameomba fedha hizo kwa ajili ya matumizi mbalimbali, huku baadhi yao wakieleza kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo katika majimbo yao, ikiwa pamoja na kununua jezi na mipira.

Sakata hilo pia linaihusisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo kigogo mmoja wa wizara hiyo (jina tunalo) ameomba mfuko mmoja wa jamii kumnunulia vifaa vya ofisi ikiwamo kompyuta kwa ajili ya matumizi ya wizara.

"Unaweza ukajiuliza maswali mengi. Wizara inaomba fedha katika mfuko wa jamii ili kununua kompyuta na vifaa vingine vya ofisi wakati ina bajeti ya ununuaji wa vifaa hivyo.
Ni wazi kuwa mhusika alikuwa akipeleka vifaa hivyo nyumbani kwake," alisema Lissu.

Alisema atawasilisha hoja yake ili kuomba Spika aunde tume kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Awali, Lissu wakati akichangia mjadala huo alisema Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa miaka mitatu mfululizo ripoti yake inailalamikia mifuko ya hifadhi ya jamii kutumia fedha kuwekeza katika miradi isiyo na tija kwa mifuko yenyewe na pia wafanyakazi.

"CAG anaeleza katika ripoti zake kwamba Sh661 bilioni, ambazo mifuko ya jamii imewekeza katika miradi mbalimbali mpaka sasa hazijalipika. Fedha hizi zilitakiwa kuwekezwa katika miradi harafu zirudishwe kwa riba na CAG anasema fedha hizo hazilipiki" alisema Lissu.

Alisema kuwa taarifa ya CAG mwaka 2013/14 inaonyesha kuwa Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali (PSPF) una nakisi ya uwezo wa kulipa wanachama wao ya Sh6.4trilioni, kwamba fedha hizo ni za wafanyakazi na zimewekezwa katika mambo mbalimbali.
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,551
2,000
Hawa jamaa wanapokea halafu wanasahau ni watu wa ajabu sana kwenye hii nchi.

Umeshampa pole huyu mjinga mwenzio?

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom