Yanayojiri Bungeni Dodoma: Tarehe 20, Juni 2014

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,782
336
Kikao cha bunge la bajeti kinaendelea hivi sasa ambapo kwa mujibu wa orodha ya shughuli za leo, yafuatayo yatajiri.
1. Kipindi cha maswali kwa serikali kutoka kwa wabunge
2.majadiliano ya hotuba ya bajeti kuendelea...

hivi sasa maswali kwa serikali yanaendelea, tafadhali fuatilia uzi huu kwa updates...stay updated.

======
UPDATES:
======

Swali la kwanza kwa leo limeulizwa na mh. Kuruthum mchuchuli kwa ofisi ya pm, kwamba je serikali ina mpango gani wa kulipa madai ya walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani rufiji na nchini kwa ujumla....

- Waziri amejibu kwamba serikali imelipa madai mengi ya waalim lakini yanaendelea kuzalishwa kutokana na waalim kuomba likizo kila mwaka na kutibiwa. Hivyo serikali itaendelea kulipa madai hayo mara nyaraka za madai zikiwasilishwa kwa wakurugenzi wa halmashauri

Mh. Vita Kawawa anauliza:
Je, serikali inayoa ufafanuzi gani kwa walimu wa leseni kukatwa kodi hali ktk mkataba wao walikubaliana kuwa hawatakatwa.

- Waziri anasema hawakutakiwa kukatwa, ila kulitokea makosa...tatizo hilo limerekebishwa na hawatakatwa tena..watarudishiwa kile walichokatwa. Aidha walimu hao wanatakiwa wajiendeleze kusoma.

Wizara ya nishati na madini:

Mh. David Kafulila anauliza, kwanini utafutaji mafuta katika ziwa tanganyika unasuasua? Hatua gani govt inachukua kutokana na makosa yaliyofanywa na TPDC ktk kupatikana mwekezaji?

- Waziri anaeleza. Aidha anasema kuwa zipo kampuni kadhaa za kimataifa zimejitokeza kuwekeza/ kufanya kazi hiyo ya kutafuta mafuta na utangazaji wa mshindi wa zabuni hiyo utafanyika hivi karibuni, tpdc ilisitisha mkataba na mwekezaji wa awali baada ya kugundua kuwa hana uwezo.

===++=wizara ya ardhi
===mh sara msafiri anauliza, kwanini kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kutokulipwa fidia zao mapema pale wanapolazimika kupisha uwekezaji kwenye maeneo yao?????
.....waZiri anajibu.

====wizara ya mambo ya ndani
mh.faida bakari anauliza je serikali ina mpango gani kuboresha nyumba za askari polisi wilaya na mkoani pemba ambazo ni chache,hazirishi na ni chakavu mno
--- waziri anasema nyumba hizo zitakarabatiwa na nyumba mpya zitajengwa. Aidha anawapongeza askari wanaoishi kwenye nyumba hizo kwa uvumilivu.
======wizara ya maliasili na utalii
mh. Jerome bwanausi anauliza.
je, mpango wa serikali wa kupunguza mamba ktk mto ruvuma utaendelea lini?? Mana wananchi wanakufa mno na kujeruhiwa mara kwa mara.
---- wazirinanasema mamba kadhaa wamevunwa na kampuni za uwindani zilizo na vibali halali zimepewa ridhaa ya kuvuna mamba mto ruvuma...anasema kuwa tawiri imehakiki idadi ya mamba wanaotakiwa kuvunwa ili kampuni zenye sifa ziweze kupewa ridhaa ya kuwavuna....aidha serikali itaendelea kulipa kifuta machozi kwa wananchi wanajeruhiwa au kuuawa na mamba wakali....pia wizara imechimba visima 5 kusaidia wananchi kupata maji badala ya kwenda mtoni na pia imejenga hospitali ktk kijiji cha mnavira.
======mh malocha anamuwakia waziri wa mali asili kuwa anatoa majibu yasiyoridhisha kwani mamba wameuwa watu mno katika ziwa rukwa na jambo hili nyalandu ameanza kupiga siasa kwenye hili jambo tangu akiwa naibu waziri...

===wizara ya habari utamaduni na michezo.
mh sabreena sungura anauliza, je serikali ina mpango mkakati gani wa kuzitaka sekta za umma na sekta binafsi nchini kuwekeza katika michezo.
naibu waziri juma nkamia anaeleza kuwa ili sekta za umma na binafsi ziwekeze katika sekta ya michezo huwa zinahakikisha zimejirisha kuwa sekta hiyo inalipa...hata hivyo anazipongeza taasisi zilizojitokeza kuwekeza kweney michezo kama vile kampuni ya bakhresa, crdb bank, makongo,shule ya ....huko mwanza nk..anasema serikali imeanzisha mashindano mbalimbali kama vile umiseta, umishumta nk ili kupata wachezaji imara.
mh. Sungura anaiamusha serikali toka usingizini iamke sasa na kurejea enzi za mashirika ya umma ambayo yalileta changamoto kubwa nchini...timu kama pamba ya mwanza, coastal union ya tanga,sigara,cda,zimanimoto nk
waziri anasema kinavhochangia ni kubadilika kwa sera za kiuchumi duniani, wawekezaji wengi wamejikita kwenye sekta zingine zaidi na sio michezo.

======mh idd azzan anauliza mbona serikali inajikita kwenye football tu????????????? Wakati kuna riadha nk ambayo iliiletea nchi sifa kubwa kimataifa???? Vp wanariadha mhm kutoka mikoa ya singida,manyara na mikoa ya dodoma hawaendelezwi???????? Wapi juma ikangaa wapya??
----- waziri anasema kuna kituo kipya cha wanamichezo kinaanzishwa hapa dom kuendeleza michezo hiyo.

=====updates===
=====miongozo imeombwa hapa hebu tufuatilie.
waziri kivulinwa ujenzi mkosamali anaomba muongozo kwa wizara ya ujenzi kwa majibu yasiyoridhisha kwanini wizara isilete bajeti nyingine kwa sababu hii ya sasa haileti majibu ya kero za wananchi...waairi anasema majibu yanayotolewa ni kutokana na maswali yanayoulizwa...hawajibu jumla jumla
====susan kiwanga anauliza jana wakati anachangia aliitaka serikali itoe ufafanuzi kwamba itv imetangaza wizara inatoa hisa kwa wawekezaji kwenye miradi ya gesi huko kilombero....anamshangaa mwijage kupotosha kwa kujifanya mjuaji na mtaalam kuliko waziri hali leo waziri amesema wazi kuwa kupata gesi kilombero kuliko ziwa tanganyika
--- waziri anasema hakuna haja ya kulumbana, kampuni ya swala haijakatazwa, wanatakiwa kuleta maombi tpdc sio kuomba kijiji...waziri anasema hajibu malumbano anajibu taratibu za utafutaji gesi na mafuta hapa nchini.
--- mh mwijange anaomba radhi kwa susan kiwanga na kueleza kuwa yeye hakumpuuza susan ila aliongeza ufafanuzi kulingana na utaalam wake wa eneo hilo...anasema ana uzoefu na utaalm wa miaka zaidi ya 20 ktk industry ya gesi na mafuta.
====waziri kivuli wa chakula na ushirika
anasema hadi sasa msimu wa pamba umeanza lakini wanunuzinwa pamba hawajapeleka fedha...anaomba muongozo wa spika
waziri zambi anajibu kuwa kumekuwa na mkanganyiko kidogo kweney soko ,anatoa maelekezo kuwa bei ya pamba mwaka huu ni 750, bei ilitangazwa kuwa 720, wizara na serikali itaongeza hiyo 30 inayopungua na maelekezo ya kimaandishi yanafuata.
===susan lyimo
anauliza wakati wizara ya madini inawasilisha hotuba yake mh masele alimtuhumu balozi wa uingereza na baadae waziri wa mambo ya nje akakanusha kauli hiyo...nvhi hiyo inafadhili sana nchi hii...nini kauli ya serikali
===waziri mkuu anaeleza kuwa 30 may lilijitokeza hilo. Kiutaratibu mambo haya yalitakiwa yawnde wizara ya mambo ya nje..nilimwagiza membe akutane nao wote..ametekeleza na wamemalizana...hakuna tatizo la kidiplomasia.

===updates=====
Majadiliano ya bajeti yameanza sasa,
===mh.mbatia anachangia hivi sasa
---anazungumzia kodi
---amejikita kwenye real estate sekta
___anahoji je wabunge na viongozi wa juu wa nchi tunalipa kodi ya nyumba zao????
---anazungumzia bandari...kwamba kuna mapato mengi sana kwenye eneo hili.

----/////----updates
=====vicky kamata sasa,yule ambaye ndoa yake ilileta utata hivi majuzi
anakoroma kuwa haungi mkono hoja
sababu ni kwamba geita haina maji, hakuna umeme,hakuna kitu kinachofanyika...siungi mkono hoja mie.
====anawatetea wachimbaji wadogo, kwann wamepewa maeneo ambayo hayana madini,wananchi wamechimba futi kibao lakininhawajapata kitu..maeneo yenye madini wamepewa wenye pesa na akili nyingi...vipi????? Wachimbaji wadogo wanateseka mno
kuna kampuni ameitaja inabadolisha tu majina hailipi kodi wala nn muhongo mulika hapo.
====anahoji kwa nini ahadi z rais zinapuuzwa?????? Kwann hazitekelezwi??? Anasema hata kama kuna watu wengine watasema kuna mambo mengine sijui nn i don care.

====anne kilango malecela sasa.....mwanamke wa shoka
anazungumzia suala la afya hasa vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua pamoja na watoto wanaozaliwa
===afya vijijini baaaadoooo, kina mama wanajifungulia nyumbani kwa sababu hakuna hospitali,mm nimetafuta vitanda, msipoongeza fedha wizara ya afya mpaka mlete wahudumu wa afya 15 kwangu....haiwezekaniii wizara ya afya fedha nipewe wakinga wangu 15
===govt ielewe kuwa wabunge tupo apa kikatiba na kisheria kusimamia na kushauri serikali, kwann govt haichukui ushauri wa wabunge?????
kamati ya bajeti inalalamika haisikilizwi,vp hapaaaaaa
=======anazungumzia maslahi ya wafanyakazi
+_++__++_+_+_paye kwa wafanyakazi iwe 9% nchi za afr mash zinakata kodi kwa wafanya kazi 6%

===madini
kuna mzungu alikamatwa akitotosha madini uwanja wa ndege lakini hayakurudishwa govt....anaitwa daniel edrivk..mmarekani...yenye thamani ya sh bilioni 8, tusiwakamue wananchi maskini hasa wafanyakazi, kusanyeni kodi kwenye madini...

=====updates===
deo filikunjombe.....anawashangaa wabunge wanaowatetea wawekezaji na kuwatelekeza wananchi waliowachagu,anashauri wananchi wasiwachague wabunge wanaotetea wawekezaji
====anamtetea mfanyakazi...paye ni kubwa mno...ipunguzwe jamani,wabunge nao walipe kodi
===deni la taifa ninkubwa mno haya madeni ya je ni mngi mno na makubwa
===michango kwa wanafunzinshule za sekondati ni mikubwa mno...
====sheria za kodi tufute misamaha yote ya kodi
=== usimamizi wa fedha zetu ....kitambulisho cha nida kifanye kazi zote hizi,hakuna haja ya kitambulisho cha kutra wakati kuna cha taifalazima.

====updates.....
kangi lugola....anatambulisha maadui wakubwa wa bajeti na umaskini nchini
1.ufisadi
2.bajeti michepuko kwamba vipaumbele vinaachwa,mara mkurabita,mkukuta,big result now
3.madeni ya nje
4.rushwa kwenye mikataba,manunuzi,hakuna nidhamunya matumizi,makampuni ya mafuta mf lake oil,
5.misamaha ya kodi
=====anamtaja mwigulu kuwa anasemwasemwa anautaguta urais...wawe na uzalendo kuanZia usoni kwa kumtazama.
...kweney maji,umeme,
====futeni misamaha ya kodiiiiiiiiii serikali futeni misamaha ya kodiiiiiii
--- tuachane na soda,bia ,sigara
====ubaunsa wangu huu nitautumia kupambana na wabunge wanatetea misamaha ya kodi...
====siunginmkono hotuba hii hadi misamaha ya kodi itakapofutwa na maafui wa bajeti watakapokemewa hadharani.

======updates=====+++*
mh. Muhonga said ruhwanya amemaliza kuchangia hivi sasa ambapo amewasilisha salam za shukran kutok kwa mh. zitto kabwe kwa wabunge na watanzania kwa ujumla ambao wamefarijinna kutoa michango yao ya hali na mali wakati wote tangu amefiwa na mama yake mzazi shida salum..
.===amezungumzia masuala kafhaa ya kitaifa na mkoa wa kigoma ikiwa ni pamoja uvuvi ziwa yanganyika,kodi kubwa kwa mfanyakazi,kilimo,afya na elimu.
 
Wana JF
Ni Tundu Lissu wa Chadema tena na Mzalendo wa Nchi hii kasimama na kusema kwamba CCM na pesa za rada juu ya madawati .Kweli nimeamini CCM they are ever serious wanadhani wanaishi miaka 60 .Ni ajabu sana kusimama na kusema serikali ya CCM na maendeleo ya Watanzania .Kuna haja gani ya mawaziri kudanganya watanzania namna hii ?Je ni madaraka na siasa za kijinga ?

Wewe unasemaje maana umemsikia Tundu Lissu live labda kama kuna mtu ana majibu .
 
Wana JF
Ni Tundu Lissu wa Chadema tena na Mzalendo wa Nchi hii kasimama na kusema kwamba CCM na pesa za rada juu ya madawati .Kweli nimeamini CCM they are ever serious wanadhani wanaishi miaka 60 .Ni ajabu sana kusimama na kusema serikali ya CCM na maendeleo ya Watanzania .Kuna haja gani ya mawaziri kudanganya watanzania namna hii ?Je ni madaraka na siasa za kijinga ?

Wewe unasemaje maana umemsikia Tundu Lissu live labda kama kuna mtu ana majibu .

Kwani tunatatizo la madawati tanzania?kinachotakiwa hapa ni watu wamalize shule,wamekalia nini,that is not an issue here,na ndo sababu watu wa vyama vingine wakijidai kuchangia madawati tunayakataa coz tuko kamili
 
Wana JF
Ni Tundu Lissu wa Chadema tena na Mzalendo wa Nchi hii kasimama na kusema kwamba CCM na pesa za rada juu ya madawati .Kweli nimeamini CCM they are ever serious wanadhani wanaishi miaka 60 .Ni ajabu sana kusimama na kusema serikali ya CCM na maendeleo ya Watanzania .Kuna haja gani ya mawaziri kudanganya watanzania namna hii ?Je ni madaraka na siasa za kijinga ?

Wewe unasemaje maana umemsikia Tundu Lissu live labda kama kuna mtu ana majibu .

Jawabu ni rahisi sana, chukua maamuzi magumu uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuitokomeza ccm, wewe na wa nyumbani kwako, ndugu zako, jamaa zako na wote ambao bado wamefunikwa na blanketi la ujinga la ccm wote waelimishe waizike ccm. Na pia tumia muda wako pia kuwaamsha waliolala wote mijini na vijijini ili waondokane na laana ya ccm kwenye chaguzi zijazo, kamwe usiwaachie akina Lisu peke yao ukategemea kuondokana na ibilisi ccm.

Tafakari na Chukua hatua mara moja.
 
... H'shauri 40 zapatiwa Sh.500m kujenga nyumba za walimu wanaofanyakazi katika mazingira magumu, Waziri Tamisemi K. Majaliwa aliambia Bunge punde.
 
Wana JF
Ni Tundu Lissu wa Chadema tena na Mzalendo wa Nchi hii kasimama na
kusema kwamba CCM na pesa za rada juu ya madawati .Kweli nimeamini CCM
they are ever serious wanadhani wanaishi miaka 60 .Ni ajabu sana
kusimama na kusema serikali ya CCM na maendeleo ya Watanzania .Kuna haja
gani ya mawaziri kudanganya watanzania namna hii ?Je ni madaraka na
siasa za kijinga ?

Wewe unasemaje maana umemsikia Tundu Lissu live labda kama kuna mtu ana
majibu .

"ccm they are ever serious" ndio nini icho?
 
wakuu jana alikuwa anaongea bungeni kwenye muda wa jioni mbunge mteule wa geita (ccm )jina lake limenitoka akawa anasifiwa na kuishukuru serekali kwa kupekeka maji geita.
_sasa hivi anaongea wa viti maalumu mh Vicky Kamata na anasema haungi hoja mkono kwa kuwa Geita hakuna maji toka ameanza kuunga mkono hoja za serekali 2011 .
#nani anasema kweli na wote ni chama moja?
 
... H'shauri 40 zapatiwa Sh.500m kujenga nyumba za walimu wanaofanyakazi katika mazingira magumu, Waziri Tamisemi K. Majaliwa aliambia Bunge punde.

Story tu hizo mkuu.. hata madawati kupitia chenchi rada walisema yameshapelekwa mashuleni jana Lisu kawaumbua kumbe story tu.. yani walishatufanya mandondocha hawa watu
 
Wameshayamaliza kivipi?
Mbona hii nchi inaongozwa kama familia?
Upumbavu huu mtu anatuhumu mbele ya vyombo vya habari wananchi tunajuzwa sasa wanamalizana kimya kimya!! Hii nchi vipi!? Hivi tukimchagua pinda si itakuwa shida kila kitu chumbani!!??? Kweli serikali ya wezi na waongo!! Kama ni uwajibikaji mtu awajibishwe!! Araaaa!!
 
Akichangia kwenye bunge la bajeti leo mbunge Kangu Lugola amewaweka hadharani maadui wa kubwa wa bajeti tanzania.Lugola amewachora maadui hao kwa staili ya katuni
Na amemwomba waziri mkuu Pinda maadui hao amkabidhi pamoja na wabunge wote ili picha zao ambazo amezitengeneza tayari ziwekwe kwenye ofisi zote za serekali
Baada ya ile ya baba wa taifa na ya raisi picha zingine zote zitolewe na kuwekwa picha hiyo ya maadui ili kila mtendaji awe anaiona
Maadui wakubwa wa bajeti yetu: 1. Bajeti mchepuko 2. Rushwa 3. Matumizi makubwa 4. Misamaha ya kodi 5. Deni la Taifa 6. Ufisadi 7. Bajeti tegemezi.
Mchango wa Mhe. Kangi Lugola umelenga katika tatizo lililopo.CCM wamefikia kuhalalisha
Majeneza kutozwa VAT!! Kweli akili ndogo kutawala akili kubwa ni shida. Tunahonga madini, tunatoza kodi majeneza
heshima kubwa kwa mbunge huyu wa CCM anayeendelea kuwa jasiri juu ya serekali yake dhaifu pamoja na kuwa anakutana na vikwazo vingi.
 
1 hr ·
WALIMU WATOAJI WA KODI.
Nimemsikia Mhe Anna Kilango Malecela akisema kuwa walimu ndio walipa kodi wakuu Tz. Ni zaidi ya 50% ya watumishi wa umma. Maslahi yao ni kiduchu sana.
Nimebahatika kukutana na walimu wengi wa kiume wakipiga biashara ya bodaboda. Je ni kwa sababu ya kipato kiduchu?
Ufundishaji umekuwa hafifu sana na walimu wamekuwa hata hawataki kujituma kufanya kazi. Hii pia ni kwa sababu ya ujira mdogo?
UnlikeUnlike · · Share
You and 5 others like this.
 
Nimeupenda mchango wa vicky kamata, "hata kama watu watasema sijui nini au nini i don't care" mnaohusika acheni kupuuza ahadi na Mh rais zitekelezeni!
 
Ila kama kweli hii serikali ni sikivu basi tunaomba PAYE ipunguzwe, watu wameongea jamani, nitashangaa kama hawatapunguza
 
Back
Top Bottom