sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Sakata la waziri wa michezo na serikali yake dhidi ya mashabiki wa mpira mbali na kutikisa mahusiano ya kidiplomasia yameiweka serikali njia panda kwa kuingilia Uhuru wa michezo hususani mpira wa miguu.
Moja ya kauli mbiu kubwa ya kimichezo ni michezo huleta furaha,ujenga udugu na mshikamano,lakini serikali hii ya CCM bila weredi imemruhusu waziri wake mwenye dhamana hiyo,badala ya kunadi sera ya michezo anatangaza enemity na discrimination kwa mashabiki.
Maanake anawagawa raia wa nchi hii kwa misingi ya utaifa kutokana na jezi,kwa kuwataka wakiva jezi ya Mamelodi na Ahly wake na passport kinyume kabisa na taratibu za michezo duniani na Afrika.
Mbaya sana hata Rais wa TFF bila tafakuri pamoja kutoa taarifa ya kupinga kauli hiyo aliingia kwenye mfumo wa waziri kupigia chapuo kauli hiyo.
Serikali iliyobebeshwa mzigo wa lawama za mashabiki na Mtendaji wake mkuu wa wizara inayosimamia michezo nayo haikupinga kauli ya waziri wake japo aliitoa maradufu. Maanake serikali inapokuja Leo na Maelezo ya msemaji wao kuwa ni utani wa waziri,unaifanya serikali kukosa weredi na umakini Mkubwa katika kuwaongoza wananchi.
Hii inatoa picha hata goli la fedha za rais hazina tija zaidi ya ubadhilifu na kutafuta sifa,kwa kuwa haliendani na mantiki ya kuimarisha mahusiano ya kimichezo.
Matinyi kauli yako imeongeza wigo mpana wa wanamichezo duniani kuiona serikali yetu isivyo thamini na isiyojua chochote kuhusu michezo,ni Bora mngenyamaza kimya mkaiachia TFF kuendelea na double standard yake kwa kutokuwa na msimamo kwa ubendera wake unaozingatia upepo.
Michezo ndiye imeleta mshikamano na umoja wa wanyarwanda jifunzeni hata kwa picha kuliko ukanjanja huu unaokwenda kuzitesa timu zetu ugenini. Msiliangamize Taifa kwa upungufu wa maarifa yenu.
#makalioyasufuriahayaogopimoto