Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

Leo asubuhi mh Lusinde akichangia ameponda sana watu wanaotetea rasimu ya Jaji Warioba mwishowe akapongezwa na mwenyekiti wa bunge mh Sita akasema huyo ndiye Lusinde na hizi ndio NONDO ZA CCM. Je huyu ni mwenyekiti wa BMK au wa bunge la CCM?
 
Lusinde alikuwa akimaanisha kuwa masuala ya dini kuingizwa ama kutoingizwa kwenye dini, bado dini itakuwa juu ya Katiba. LUSINDE ametolea mfano kuwa katika sherehe za dini kama Maulid, Krismasi na Pasaka, watu hupika pilau na kuvaa nguo mpya tofauti na sherehe za seikali kama sikukuu za uhuru, Muungano, mapinduzi ya zanzibar. Hivyo dini itabaki kuwa juu siku zote.
 
Huo ni utata wa kikatiba kabla hata Katiba yenyewe haijapatikana,ukishaitambua na kuelekeza mahakama nyingine zifuate au zitambue uamuzi wa mahakama hiyo kinachofuata ni kdumamaza mahakama nyingine maana itakuwa kama mahakama ya rufaa hivyo maamuzi yatakayotolewa na mahakama za mwanzo mhusika asiporidhika ataenda kwenye mahakama ya kazi na kwakua Katiba imeelekeza maamuzi ya mahakama hiyo yatambuliwe kinachofuata ni nini?
 
Amesema ameshambuliwa katika hotuba ya Maalim Seif Sharif Hamad kuwa yeye ni msaliti na kwamba anawahujumu CHADEMA, CUF na vyama vingine. Amesema yeye ni mjumbe wa TCD, na walikubaliana kuwa Hakuna sheria Inayomruhusu Rais Asitishe Bunge.
DOVUTWA amesema suala la kusitisha Bunge lisimhusishe Rais, CCM wala chama chochote, bali TCD kwa kwenda kwa wananchi na kuwaeleza sababu za kuwafanya bunge lisitishwe na baadaye warudi BUNGENI kuwaeleza Wabunge kusitishwa bunge, jambo ambalo UKAWA hawalitaki kwa sababu wanaona kama kurudi Bungeni ni kula matapishi yao.
 
Lakini kama umemuelewa vizuri Mzee Sitta, ni kwamba maamuzi yanayofanywa na Mahaakama ya Kadhi nchini hayatambuliki na Mahakama zingine, so Kitakachofanywa na Katiba ni kuzielekeza Mahakama zingine kutambua maamuzi yanayofanywa na mahakama ya Kadhi,

Kwa maana nyingine ni chombo kamili cha kufanya maamuzi.HAKIKA MWISHO WAKE ULEEE UNAKARIBIA
 
Hayo yamesemwa na Mchangiaji wa mijadala wa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea. Amesema Rais Kikwete anastahili tuzo kwa kazi nzuri anqyoifanya ya kusimamia mchakato wa Katiba Mpya. Amependekeza na Spika wa Baraza la Wawakilishi , Pandu Ameir Kificho naye apewe tuzo kwa kuendesha Bunge Maalum bila ya kanuni.
 
Huyu naye hana jipya - Alishawahi kusema akiwachaguliwa kuwa Raisi atajenga windanda vya silaha sijui alitaka kutupeleka wapi!
 
Mh Dovutwa amesema Prof. Lipumba alikuwa wa kwanza kuchukua pipi za kwenye bakuli kiganja kizima na kuziweka mfuko wa koti wakati wanaagana na Mh Rais. Amesema kama hataki kurudi bungeni arudishe na pipi za Rais!!!!!!! Juisi na kahawa ya maziwa walishaimaliza. Aaaahhaaaa UKAWA majanga tupu. Wameshindwa kueleza kilichowapeleka kwa Rais na wametoka na nini, sasa wanawadanganya mazwazwa kuwa wameambia wakaandamane. Mazwazwa jitambue
 
Huyu nae njaa zake zinamsumbua miaka yote hii ya chama chake hana hata mwenyekiti wa mtaa
 
Amesema ameshambuliwa katika hotuba ya Maalim Seif Sharif Hamad kuwa yeye ni msaliti na kwamba anawahujumu CHADEMA, CUF na vyama vingine. Amesema yeye ni mjumbe wa TCD, na walikubaliana kuwa Hakuna sheria Inayomruhusu Rais Asitishe Bunge.
DOVUTWA amesema suala la kusitisha Bunge lisimhusishe Rais, CCM wala chama chochote, bali TCD kwa kwenda kwa wananchi na kuwaeleza sababu za kuwafanya bunge lisitishwe na baadaye warudi BUNGENI kuwaeleza Wabunge kusitishwa bunge, jambo ambalo UKAWA hawalitaki kwa sababu wanaona kama kurudi Bungeni ni kula matapishi yao.
Alipositisha kupisha bunge la bajeti alitumia sheria gani? ya Ukawa?
 
mzee 6 aache kutupotosha UKAWA hawakuandaa hii rasimu achana na ukawa rudi kwenye rasimu.
 
Kuna watu ambao hawana hadhi ya kuitwa kiongozi. Huyu jamaa 2010 alichukua hela za kugombea urais kaingia mitini. Hakufanya kampeni. Leo ndio anatunga katiba badala ya kuwepo magereza. Huu ni usanii mtupu. Na ni kweli ni kibaraka wa ccm.
 
naunga mkono kuingizwa kwa mahakama ya,kadhi ila lazma iwekwe general kama DINI ZOTE ZINAO UHURU WA KUABUDU NA KUENDESHA MAMBO YAO YA KIIMANI KAMA NDOA VIFO MIRATHI NA MENGINEYO WANAYOABUDU KWA GHARAMA ZAO NA SI KWA NJIA YOYITE ILE KUINGILIA GHARAMA ZA SERIKALI.....kwa tamko hilo wao wajiachie na kujenga mahakama kila msikiti

Unaporuhusu jambo moja na kulikubali ujue umetoa nafasi ya kuletewa jambo lingine na huwezi ukalikataa lazima utalikubali tayari unakuwa umeshaweka mwanya wa kupitia.Kama waislamu wamepewa mahakama ya kadhi kitakachofuata watataka mahakama ya kadhi igharamiwe na serekali na mwisho watataka nchi iwe ya kiislamu na hakuna atakaye wapinga.
 
Back
Top Bottom