Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

Wanabodi,

Hatimaye ile Simtofahamu juu ya hatima ya Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba mpya, imemalizika leo, baada ya M/Kiti wa BMK, Mhe. Samuel Sitta, kupokea mchango wa maandishi wa Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Harold Jaffu, na alipouna umekaa vizuri, akaupeleke mchango huo moja kwa moja kwenye kamati ya uandishi, kuiingiza mahakama ya Kadhi moja kwa moja ndani ya katiba mpya bila kuupitishia kwenye kamati ya Uongozi, kama kanuni zinavyoeleza.

Hivyo sasa Mahakama ya Kadhi, iko rasmi ndani ya Katiba Mpya!.

Akifafanua, Mhe. Sitta amesema kumbe mzizi wa fitna kuhusu Mahakama ya Kadhi ni kitendo cha Mahakama hiyo kutotambuliwa rasmi na katiba ya nchi, na maamuzi ya mahakama ya kadhi, kutotambuliwa na mahakama za kawaida, sasa mahakama ya kadhi, itatambuliwa rasmi kuwa ni moja ya mahakama halali nchini Tanzania, na uamuzi wake sasa utatambuliwa na mahakama za juu, ili waathirika wa maamuzi ya mahakama ya kadhi, waweze kukata rufaa kwenye mahakama za juu.

Hata hivyo, bado mahakama hiyo ya kadhi, itaendeshwa na Waislamu wenyewe, itagharimiwa na Waislamu wenyewe na sio kodi za Watanzania!.

Hivyo kinachofanyika sasa kwa mahakama ya kadhi kuingizwa kwenye katiba, ni kwa ajili ya kutambuliwa tuu, na sii zaidi ya hapo, na maamuzi yake kutambuliwa ni maamuzi halali ndani ya JMT.

My Take.

Kwa vile Mahakama ya Kadhi ilikuwepo tangu enzi ya mkoloni, na tulipopata uhuru, mahakama hizi zilikuwepo, baadae zikafutwa, kiukweli hakuna tatizo lolote kwa Waislamu kupewa haki hii katika katiba mpya!.

Source: Sitta akizungumza live BMK-Dodoma.

Thanks.

Pasco
Asante Pasco!
Kuna Jambo la kujiuliza. Mahakama ya kadhi au za Kiraia ni ipi ina mamlaka juu ya nyingine kwa ngazi ipi. Mfano, kadhi ya wilaya ni sawa na mahakama ya wilaya? Je jambo likihukumiwa kwenye mahakama ya kadhi (za ngazi zote) linaweza kurudishwa kwenye mahakama za kiraia iwapo upande mmoja hautaridhika? au ndo itakuwa ntolee? Na kwa ngazi ipi? mfano umetoka kadhi wilaya unaweza kwenda mahakama ya wilaya au utarudi mahakama ya mwanzo. Endapo mahakama za kiraia zikibatilisha hukumu ya kadhi ni nini itakuwa athari kwa mahusiano na amani ya nchi? Nachelea kuona tunaandaa mazingira ya vita vya muungano wa mahakama za kiislamu za somalia.
 
Leo nimeamua kupoteza muda wangu adhimu kwa kulisikiliza Bunge maalum la Katiba baada ya Muda Mfupi nikaconfuse na kuzima TV yangu.
Uelewa wangu ilikuwa ni kwamba kutunga katiba mpya kwa tafasiri halisi ni kuzaa nchi mpya na yenye mambo mapya na nina amini hata Tume ya Rais iliyoongozwa na Mh Jaji Joseph S.Walioba ileelewa ni kuzaa nchi mpya na yenye mambo mapya.
Loooh!leo nilivyoamua kulicheck BMT nilishangaa na kuchoka nilichosikia

Please Wasomi tusaidie maana ya neno-MPYA or Brand New
Aksanteni
ALL THE BEST SSC kwenye mechi yenu ya leo-SIMBA Vs URA-Taifa-Nikifanikiwa kupata flight ya mapema nitakuwa taifa pia
 
Sitta ameelezea UKAWA walivyofeli vibaya kwenye mchakato wa Katiba mpya kuanzia kudai hati ya Muungano mpaka wanatoka nje. Amewafananisha UKAWA na Waigizaji wa MAREKANI.
 
Sitta ameelezea UKAWA walivyofeli vibaya kwenye mchakato wa Katiba mpya kuanzia kudai hati ya Muungano mpaka wanatoka nje. Amewafananisha UKAWA na Waigizaji wa MAREKANI.

atasema kila kitu but yeye ndo kachemsha,popularity kwishey
 
Hana jipya huyo kilaza tena ajiangalie raia wana hasira nae akikatiza mtaani kiboya atapigwa mayai viza,Mzee laanakhum kabisa.
 
Kama kawaida yake, Livingstone Lusinde , wakati akichangia mjadala , amesema kigezo cha kwamba Mbunge awe na angalau elimu ya kidato cha nne hakina msingi wowote kwa vile Prof. LIPUMBA anashindwa kila uchaguzi.
 
Nimempenda sana Lusinde kwa jinsi anavyochangia
 
Tamaa mbaya sana,alifikiri kuongoza BMK ni kazi rahisi.Ona sasa anawayawaya,mpaka anataka kuchakachua kura baada ya kususiwa mpaka na wanaccm wenye akili
 
Nimemsikia pia akishauri kuwa kama elimu ndiyo kigezo cha kuchaguliwa, kigezo hicho hicho ndicho kiwe kigezo cha watu kupiga kura.
 
Kati ya wabunge wa BMK walioongea vizuri na logic japo elimu zao n ndogo,mh.lusinde is the best
 
Back
Top Bottom