Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

Kwanza itakuwa ni kosa kubwa sana kwa mahakama ya kadhi kutajwa kwenye katiba, pili wakristo watakuwa ni wajinga wa kufa na kupona kama wataipigia kura katiba hiyo, kwa hiyo lengo la ccm siyo kuleta katiba bali anataka tubaki na katiba ya zamani.
 
Mjumbe huyo alikuwa anahoji uhalali wa sifa ya Dereva kupata ajira kuwa kidato cha nne wakati wabunge wanapendekeza sifa ziwe kujua kusoma na kuandika
 
Kwanza itakuwa ni kosa kubwa sana kwa mahakama ya kadhi kutajwa kwenye katiba, pili wakristo watakuwa ni wajinga wa kufa na kupona kama wataipigia kura katiba hiyo, kwa hiyo lengo la ccm siyo kuleta katiba bali anataka tubaki na katiba ya zamani.
Katiba Mpya inapatikana tu mtake msitake
 
huyu Lusinde kwa kweli ijapokuwa inasemekana hana elimu lakini jamaa ana akili sana. anajua sana kujenga na kutetea hoja kwa kweli elimu sio kila kitu.
 
Amesema ameshambuliwa katika hotuba ya Maalim Seif Sharif Hamad kuwa yeye ni msaliti na kwamba anawahujumu CHADEMA, CUF na vyama vingine. Amesema yeye ni mjumbe wa TCD, na walikubaliana kuwa Hakuna sheria Inayomruhusu Rais Asitishe Bunge.
DOVUTWA amesema suala la kusitisha Bunge lisimhusishe Rais, CCM wala chama chochote, bali TCD kwa kwenda kwa wananchi na kuwaeleza sababu za kuwafanya bunge lisitishwe na baadaye warudi BUNGENI kuwaeleza Wabunge kusitishwa bunge, jambo ambalo UKAWA hawalitaki kwa sababu wanaona kama kurudi Bungeni ni kula matapishi yao.
Mzee Abdallah Fundikira (R.I.P) alikuwa ni mtu anayeheshimika sana na hata alivyoanzisha chama cha UMD wengi walijua watakuwa wanachama wake. Alijimaliza mwenyewe siku alipopokea cheque ya ruzuku na kuamua kuwakimbia wanachama wenzake na kujificha. Matokeo yake ni kuwa historia imemsoma vibaya na sote tu mashahidi.
Hawa wanaosaliti mawazo sahihi kwa ajili ya kupata ruzuku haramu wanaangalia karibu sana na hakika hawajui ni heshima kiasi gani wanastahili kwa kuwa wajumbe wa mkutano huu wa kuboresha katiba.
Huyu bwana nilimjua pale alipojitoa kugombea urais eti kumuunga JK mkono na inaelekea akili aliyoitumia wakati huo haijabadilika hadi leo!

 
UKAWA wenyewe wanatamani kurudi, wanaona aibu tu, sheria zote zimewabana wanatapatapa tu sasa
 
Ndo kwanza nakusikia kuwa Biblia ina sheria

Kama hujawahi kusikia kwa taarifa yako Torati iliyoko ndani ya Biblia ni kitabu cha sheria.Makatazo yote ya makosa ya wizi,kuuwa,kubaka n.k yamejikita zaidi kwenye amri kumi zilizoko kwenye Biblia.Kwa faidi yako zaidi mabalozi ambao wako hata kwenye chama chako CCM wametokana na Bibilia waliwekwa maalumu kwa ajili ya kumsaidia Musa kutoa hukumu na kuwapatanisha waisrael wanapokosea,waliwekwa kila baada ya watu kumikumi,ndiyo maana wanaitwa nyumba kumikumi.Mabalozi wa nchi na nchi nalo ni la kibiblia,Ilijengwa miji iliyojulikana kama miji ya makimbilio ili kuwa ni sheria kuwa mtu akikosa auwawe kwa kupigwa na mawe,huyo mtu anaye takiwa kuuawa akifanikiwa kukimbia na kuingia kwenye miji hiyo ilikuwa ni marufuku kuingia kwenye miji hiyo na kumdhuru kwani amekuwa ameshaingia kwenye miji ambayo hairuhusu mtu kudhuriwa,tayari sheria za hapo zinakuwa zinamulinda.
 
Naona Tanzania yetu ikiwa vipande vipande muda si mwingi kwa 6 kuruhusu hili la mahakama ya kadhi kuwa sehem ya katiba.... anatafuta sympathy kutoka kwa waislam lakini misingi iliyo jenga Tanzania ni tofauti na nchi nyingine.... serikali yetu haina dini.... kama kutakuwa na mahaka ya kadhi na kutambuliwa na mahaka zetu rasmi je waweza sema serikali haina dini?? Watanzania tunaishi pamoja, waislam kwa wakristu, tumeoleana.... hapa kazi ipo...Katika jambo baya ulilo fanya 6 ni hili na umeua Tanzania yetu....
 
Naomba Mods mnitendee haki nipate ruhusa japo ya dk chache niseme Kum'mako Six, Wewe umebakiza siku chache sana hapa dunia hivyo usitake kutiachia majanga hapa duniani! Six atambue kwamba yeye naye yuko kwenye orodha ya watu wanaosubiri kufa (Nape 2014)!!!! Hivi anafikri ikiingizwa kwenye katiba waslamu ndo wataishia hapo? Kama kura ndo zinatafutwa hivi, basi kazi tu nayo!! Kwanza hataingia hata kwenye duru za kura ya maoni, maccm yatamchinjia baharini mapemaaaaa!!
 
Anatafuta support ya waislamu ila ndio anazidi kuharibu!

Sawa kabisa. Kama kuna kukataa rufaa kwenye mahakama za juu, jee maamuzi ya mahakama za juu yatazingatia sheria ipi? Pili kwa nini mahakama ya kadhi isipate fedha serikalini kama mahakama hizi zitaamua mashauri ambayo kama hazingekuwepo zingekwenda kwa mahakama za kawaida? Kwa maana nyingine mahakama ya kadhi itapunguza kesi ambazo zingekwenda katika mahakama za kawaidi hivyo na gharama za uendeshaji.
 
Pinda aliwambia zanzibar si nchi na hili limejidhirisha leo Rage kawajibu hawezi kuwa wanachama wa FIFA kwani hawatambuliwi UN.

Wanaotambuliwa ni Tanganyika ambao hakuna ubishi ndo wamejivika koti la TANZANIA na Muungano.

Katiba ya Zanzibar inasema Zanzibar ni nchi.Napenda niwaambie hata saccos wana katiba.

Kama wanataka watambulike suluhu ni serikali tatu au wajitenge vinginevyo tutawatawala milele kwani naamini mpaka dunia itaisha Rais wa muungano atatoka TANGANYIKA tu.
 
Haa haa naona tanganyika inajiandaa kuvaa joho rasmi la muungano, huku zanzibar ikiachiwa kandambili.
 
Nasubiri uzinduzi wa single ya Ccm toka Dom chini ya sita anaye sita. Wameongezewa 60days yaani ni full shangwe
 
Back
Top Bottom