Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

Yanayojiri bungeni Dodoma: Ijumaa tarehe 12 Septemba, 2014

BungelaKatiba2014tz

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,231
Reaction score
649
Taarifa za Kamati juu ya Rasimu ya Katiba zinaendelea kujadiliwa. Leo Sura zinazojadiliwa ni pamoja na sura za 9, 10, 11, 12 na ibara mpya za Tume ya Jinsia, Takukuru na sheria ya uhujumu Uchumi. Mchangiaji wa kwanza ni Mh. LUCY NKYA..
 
Mwenyekiti Samwel Sitta, amesema amepeleka Mchango wa Mbunge wa Kisarawe, SULEIMAN JAFO kjhusu Mahakama ya Kadhi yamesaidia sana na ameyapeleka kwa Kamati ya Uandishi na kesho yatatolewa uamuzi.
 
Wanabodi,

Hatimaye ile Simtofahamu juu ya hatima ya Mahakama ya Kadhi kwenye Katiba mpya, imemalizika leo, baada ya M/Kiti wa BMK, Mhe. Samuel Sitta, kupokea mchango wa maandishi wa Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Harold Jaffu, na alipouna umekaa vizuri, akaupeleke mchango huo moja kwa moja kwenye kamati ya uandishi, kuiingiza mahakama ya Kadhi moja kwa moja ndani ya katiba mpya bila kuupitishia kwenye kamati ya Uongozi, kama kanuni zinavyoeleza.

Hivyo sasa Mahakama ya Kadhi, iko rasmi ndani ya Katiba Mpya!.

Akifafanua, Mhe. Sitta amesema kumbe mzizi wa fitna kuhusu Mahakama ya Kadhi ni kitendo cha Mahakama hiyo kutotambuliwa rasmi na katiba ya nchi, na maamuzi ya mahakama ya kadhi, kutotambuliwa na mahakama za kawaida, sasa mahakama ya kadhi, itatambuliwa rasmi kuwa ni moja ya mahakama halali nchini Tanzania, na uamuzi wake sasa utatambuliwa na mahakama za juu, ili waathirika wa maamuzi ya mahakama ya kadhi, waweze kukata rufaa kwenye mahakama za juu.

Hata hivyo, bado mahakama hiyo ya kadhi, itaendeshwa na Waislamu wenyewe, itagharimiwa na Waislamu wenyewe na sio kodi za Watanzania!.

Hivyo kinachofanyika sasa kwa mahakama ya kadhi kuingizwa kwenye katiba, ni kwa ajili ya kutambuliwa tuu, na sii zaidi ya hapo, na maamuzi yake kutambuliwa ni maamuzi halali ndani ya JMT.

My Take.

Kwa vile Mahakama ya Kadhi ilikuwepo tangu enzi ya mkoloni, na tulipopata uhuru, mahakama hizi zilikuwepo, baadae zikafutwa, kiukweli hakuna tatizo lolote kwa Waislamu kupewa haki hii katika katiba mpya!.

Source: Sitta akizungumza live BMK-Dodoma.

Thanks.

Pasco
 
ni haki yao kabisa ila uwendeshaji wake usije leta malalamiko mlango wa pili
 
Kweli na mimi nimesikia live kuwa ameagiza kamati ya uandishi kuliratibu vizuri ili likiingizwa lisilete utata
 
hawa ambao hawapo bungeni na wakati wanafanya maridhiano hawakuulizia bunge lita terminate vipi mbona kama wanachezewa trick?sitta anaendelea tu kuyoyoma na mpango wao wa kuzitafuna kodi za wananchi
 
naunga mkono kuingizwa kwa mahakama ya,kadhi ila lazma iwekwe general kama DINI ZOTE ZINAO UHURU WA KUABUDU NA KUENDESHA MAMBO YAO YA KIIMANI KAMA NDOA VIFO MIRATHI NA MENGINEYO WANAYOABUDU KWA GHARAMA ZAO NA SI KWA NJIA YOYITE ILE KUINGILIA GHARAMA ZA SERIKALI.....kwa tamko hilo wao wajiachie na kujenga mahakama kila msikiti
 
Itakuwa inatajwa tu na mambo mengineyo wataachiwa wenyewe Waislamu kuisimamia na kuiendesha. Si jambo baya. Lakini,nasi wakristo vipi jamani?
 
Lakini kama umemuelewa vizuri Mzee Sitta, ni kwamba maamuzi yanayofanywa na Mahaakama ya Kadhi nchini hayatambuliki na Mahakama zingine, so Kitakachofanywa na Katiba ni kuzielekeza Mahakama zingine kutambua maamuzi yanayofanywa na mahakama ya Kadhi,
 
6, kaamua ajinusuru kwa ngalawa ya mahakama ya kadhi - duh "kua uyaone mziwanda wangu!!"
 
Mbunge Asha Mtwangi amechangia kwa kumshukuru spika kwa kuwakumbuka waislamu juu ya kuingizwa kwa suala la mahakama ya kadhi ktk katiba
 
Ni haki yao kupewa haki yao kama makundi mengine yanavyo pewa haki zao!
 
Back
Top Bottom