Ambacho hukisemi hapa moja kwa moja, lakini kama kawaida yenu watu wa huku ni kwamba hutamki wazi kwamba Samia anayumbishwa tu kama bendera. Mara useme Kikwete hivi; na huku unazunguka na ya Nchimbi na Makonda; na bado husemi lolote juu ya 'mastermind' mkuu Kinana!Kinachofikirisha ni ukweli kwamba Kikwete akiwa Rais hakuingiliwa kwa namna yoyote ile na Hayati Mkapa, haonekani kuondoka kabisa kwenye duru za kisiasa akihitajika kwa uzoefu wa ushauri wake na wakati huo huo akiwa na hulka ya kupenda kuhusika kwenye mengi zaidi ya ustaafu wake.
Samia hana uwezo wowote wa uongozi, ndiyo maana hata huwezi kuchambua anakosimamia katika jambo lolote katika maelezo yako marefu.