Yametimia: Wenye nyumba sasa kulipa kodi

Yametimia: Wenye nyumba sasa kulipa kodi

kwa maoni yangu kodi iwekwe, lakini iundwe bodi itakayo regulate bei za pango kulingana na hadhi ya nyumba .kama sumatra wanavyo regulate bei za mabasi na wameziwekea amadaraja
Bora hisiwepo hiyo bodi unayosema, unaweza ukapatana na mwenye nyumba ili mkataba uonyeshe bei ndogo, ili mlipe kodi ndogo, mfano kodi market price laki mbili, ww unaweza ukamuomba mwenye mkataba mwandikiane laki moja ili kupunguza kodi ambayo automatically atailipa mpangaji,lakini ikiwepo bodi bei itajulikana hivyo huwezi kuunder value price( of course hii kodi anatakiwa alipe aliyopokea hela lakini practically haitokuwa hivyo)
 
wewe bila shaka huna nyumba. mbona wenye nyumba siku zote wanadaiwa kodi ya jengo ie property tax.
nadhani hii ni tafauti na inayo jadiliwa hapa, kodi kutoka kwenye pato la kupangisha nyumba.
 
kwa hiyo hata mimi mwenye kajumba kangu kule kijijini kwangu mpapa. nitalipa kodi? hapo ufafanuzi unahitajika...
 
Kodi wakusanye maana nayo ni mapato. Lakini hoja ya kupanga bei sikubaliani nazo kabisa! Hii ni kasumba ya ujamaa.! Hapo naomba nitofautiane na wewe mkuu. Mimi ni miongoni mwa watu tunaopinga ujamaa, na kasumba zake zote. Hata udikteta unaoendelea sasa hivi nchini ni kasumba ya ujamaa. Tazama demokrasia na haki za binadamu kwenye mataifa yote yaliyokuwa ya kijamaa!
Mtu anadaiwa ada ya mwanae anaamua kupandisha kodi.Je,ni sahihi?
 
Mie nahic anazungumzia pasent fulan kwenye kodi za nyumba iwe inaingia serikarin
Kama kodi ni sh.200000 labda 20% inaingia kwa gvt
 
Serikali ya ze mbululaz, yaani haifikirii vyanzo vipya kwenye Madini, Utalii, na natural resources zingine wao wanawaza kumlundikia kodi mwananchi tu

Jamani hili si la kushangilia tu kwa sababu sisi si wenye nyumba lakini tujiulize nani ataumia ktk haya? In short hapo ni wote

Mtu huyo huyo ulipe KODI YA KIWANJA, KODI YA JENGO (Property Tax), na bado awekewe KODI YA NYUMBA kwenye KODI YA NYUMBA, let's rethink on this
Corporate tax, VAT, withholding tax, property tax kampuni moja inalipa, ukija kwa individual mfanyajazi ndiyo usiseme, PAYE up to 30%, Skills &Development Levy 5%, workers compensation fund 1% bado indirect taxes ambazo unalipa ktk kila kitu utakachonunua kama mlaji wa mwisho.

Sasa unashangaa ni kipi ambacho huyu mlaji halipi kodi?

Wamebaki kutoa misamaha ya kodi kwa watu wakubwa na wao viongozi wanaofanya biashara then unataka kuja kufidia kutoka kwa muuza nyanya za mafungu gengeni, StupiDITY to the extreme.
 
Mtu anadaiwa ada ya mwanae anaamua kupandisha kodi.Je,ni sahihi?
Hawezi kupandisha kati kati ya mkataba ila ana mamlaka ya kupandisha term mpya itakapoanza. Na kwa ustaarabu wamekuwa wanawapa taarifa ya kusudio la kupandisha kodi ya nyumba. Mbona nyumba za bei rahisi sana zipo kulingana na nyumba yenyewe na mahali ilipo. Mkuu nikwambie, mfumo wa uchumi ndiyo unaoathiri hata kodi ya nyumba. Mtu ujenge nyumba kwa milioni 100, lazima utatoza kodi kubwa tu. Hebu sema kwa mfano ulitaka kodi elekezi iwe shilingi ngapi?!
 
Mie nahic anazungumzia pasent fulan kwenye kodi za nyumba iwe inaingia serikarin
Kama kodi ni sh.200000 labda 20% inaingia kwa gvt
Yote sawa tu hao nao walipe kodi.Mtu majukumu yakimbana kesho yake anaamu kupandisha kodi kiholela tu.Huu ni uharamia na unyonyaji.
 
Hawezi kupandisha kati kati ya mkataba ila ana mamlaka ya kupandisha term mpya itakapoanza. Na kwa ustaarabu wamekuwa wanawapa taarifa ya kusudio la kupandisha kodi ya nyumba. Mbona nyumba za bei rahisi sana zipo kulingana na nyumba yenyewe na mahali ilipo. Mkuu nikwambie, mfumo wa uchumi ndiyo unaoathiri hata kodi ya nyumba. Mtu ujenge nyumba kwa milioni 100, lazima utatoza kodi kubwa tu. Hebu sema kwa mfano ulitaka kodi elekezi iwe shilingi ngapi?!
Kwenye swala la kodi ya kupangisha,wenye nyumba ni wakandamizaji kuliko hata serikali.Kwa mfano,mwenye nyumba anajua mwakani mwezi January nina ada ya watoto,nataka kununua gari n.k,anachofanya anakupa tu taarifa mapema ya ongezeko la kodi huwezi unahama.Niambie mwenye nyumba wa aina hii na serikali ni yupi mkandamizaji katika swala zima la kodi?Tufikirie kwa mapana katika hili.
 
kwa hiyo hata mimi mwenye kajumba kangu kule kijijini kwangu mpapa. nitalipa kodi? hapo ufafanuzi unahitajika...
Utakayolipa wewe ni Kodi ya Kiwanja na Property tax (kodi ya Jengo). Wenye nyumba wanaozungumziwa hapa ni wale wanaopangisha, kama na wewe umepangisha basi utatozwa Kodi
 
Nafikiri hii kodi itawahusu wenye nyumba zenye hati,kwa mtu wa uswahilini utamwambiaje alipe kodi kutoka kwenye nyumba ambayo iko kwenye eneo isiyo rasmi? Alipe hiyo kodi kwa document gani? wakitaka kukusanya kodi hizo warasimishe maeneo kwanza,sio leo unamwambie alipe kodi alafu baada ya miaka kadhaa unamwambia bomoa maana eneo lako sio rasmi!Ila kwa sasa hii itawahusu wenye maeneo rasmi na wenye hati
 
Kwenye swala la kodi ya kupangisha,wenye nyumba ni wakandamizaji kuliko hata serikali.Kwa mfano,mwenye nyumba anajua mwakani mwezi January nina ada ya watoto,nataka kununua gari n.k,anachofanya anakupa tu taarifa mapema ya ongezeko la kodi huwezi unahama.Niambie mwenye nyumba wa aina hii na serikali ni yupi mkandamizaji katika swala zima la kodi?Tufikirie kwa mapana katika hili.
Sasa mkuu kama taarifa umepewa mapema kuna ubaya gani?! Ujue ana haki katika taarifa hiyo kukwambia kuwa hapangishi tena nyumba yake na kwa hiyo hatakupangisha tena, tafuta mahala pengine. Na lazima uhame.! Kaka cha maana hapo ni kujenga yako tu. Mtu kwao! Mtu kwako! Kwingineko mateso! Mkuu nimeomba upendekeze bei elekezi. Naomba ukija uje na hilo tafadhali.
 
Yaani hii nchi maranyingine ukifikiria kwa undani mambo yanayoamuliwa na kufanyika unaweza kujikita unachanganyikiwa na kuhama nchi kwenda penye angalau maamuzi ya kiwango cha kumuangalia mwananchi mnyonge. Hii kodi inakuja wakati wananchi hawajui hata hatma ya vipato vyao kupitia Kazi halali kama vile vibarua na waaajiriwa. Ninachokiona hapa kuna mambo mabaya sana yatatokea kuhusu Uchumi mkubwa na mdogo katika nchi yetu katika miaka ya 2022-2035. No strategic long term national policies in the country's economic, social and political arenas. Kweli naanza kuamini Waafrika tuna matatizo makubwa ua kimfumo na si umaskini wetu. Haifurahishi........
 
Ngoja nidikree interest, mimi nina nyumba za kupangisha. Naisubiri tu hiyo kodi itakayokatwa itangazwe ili na mimi niwabambikie wapangaji wangu kwenye kodi yao maana tayari nimeishawapa maelezo ya mdomo kwamba kodi hiyo ikiwekwa wataigawana wao asiyetaka atafute chumba ahame, ila kwa kauli moja wote wamekubaliana kulipa.

Kama wauza sukari wanaouza sukari hadharani wameweza sisi tunaolipana majumbani tutashindwaje?
 
Mimi ni mpangaji, lakini sijapenda kuwatesa wananchi. Ile Tanzania ya viwanda inaanza lini....gesi inatusaidiaje, Madini Je.??!
 
Sheria ya withholding tax na property tax ipo kitambo. Issue ni usimamiaji wa hiyo sheria na infrastructure
 
Hii ni kodi ya mapato ya pango

Serikali inachanganya tu itakuwa ni hiyo hiyo, sehemu nyingine property tax kwa nyumba ya makazi ni 2% ya value ya nyumba, makazi na biashara ni 4% na biashara ni 6% so nadhani kodi ya mapato tayari imo humo ndani vinginevyo bei zisingetofautiana
 
Mtoa post atakuwa anadaiwa kodi. Ikiwekwa kodi hiyo kodi itapanda, hamna kodi elekezi. Labda waanze elekezi kwenye vifaa vya ujenzi, gharama za mafundi, usafiri wa vifaa vya ujenzi, bei za viwanja, nk. Kama ikija kodi say kwa asilimia 10 na kodi itapandishwa kwa asilimia 10 wapangaji waisome namba

Mkuu ongezea na Costs of renovation kila mwaka, maana sasa watu nchi hii wanakurupuka tu na kodi kama fasheni. .na watu wanashangilia maadam anaona hajaguswa moja kwa moja. Kama kodi itakuwa calculated basing on income, basi na cost pia za hiyo investment zitazingatiwa. Vinginevyo mwenye nyumba atalipa kodi, the same amount anaitupa kwa mlaji.

Kwa hiyo tukishangilia kwa kuwa tumepanga, jua pia utakutana na hiyo kodi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom